Zitto asema : ' Bajeti 2010/11 hiyo ni sawa na barua ndefu ya CCM kutaka kujinyonga'

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,274
24,140
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto ameishambulia CCM kwa kushindwa kuondoa umasikini nchini katika kipindi cha miaka minne iliyopita, licha ya serikali yake kuidhinishiwa bajeti inayoomba kila mwaka.Akichangia hoja ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/11 bungeni jana, alisema haijalenga (bajeti hiyo) katika shughuli za maendeleo, badala yake imejikita zaidi katika kuwashibisha watu wenye uwezo na kuzidi kuangamiza walalahoi.

“Hii ni bajeti mbaya. Ni kwa ajili ya tumbo. Ina faida zaidi kwa wenye uwezo,” alisema Zitto.

Alisema kutokana na ubaya wa bajeti hiyo, watakaoumia zaidi ni walalahoi wanaofikia 13 milioni nchini ambao wanaishi kwa dola moja ya Marekani (Sh 1,400) kwa siku.

“Ni bajeti ambayo ina faida zaidi kwa wenye uwezo,” alisema Zitto akichambua kuwa imeshindwa kujitosheleza kutokana na mapato ya ndani.

Ili kuendesha nchi kwa bajeti hiyo, Zitto alisema: “Itabidi serikali ikope kwa wahisani kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi, kulipa posho na kununua mafuta kwa ajili ya magari”
Endelea kwenye link:Zitto aifyatua CCM, ASEMA IMESHINDWA KUONDOA UMASIKI
 
Nimemsikiliza Mheshimiwa Zitto. Nampongeza kwa aliyoyasema kutetea haki za wanyonge wa nchi hii. Wanaoishi kwa hiyo dola moja kwa siku ni wachache ukilinganisha na wengi ambao hata Sh. 200 kwa siku ni taabu kuipata.
Zitto, asante kwa kuwatetea walalahoi wanahitaji watetezi wengi zaidi labda wataanza kuona mwanga mwisho wa 'tunnel'.
 
Back
Top Bottom