Zitto asafishiwa njia mbio za urais 2015 na wabunge vijana akiwemo Nasaari na Filikunjombe

Hata kama atanunuliwa kurasa za mbele za magazeti na kupambwapambwa kila mara,bado Zitto Zuberi Kabwe hawezi kuwa Rais wa nchi hii.Namheshimu sana Zitto Kabwe.Namkubali kwa uwezo wake wa kiuongozi.Lakini kwa la Urais,bado hajakomaa. Kuchagua kijana/handsome tumekoma. Zitto labda anafaa kuwa Waziri au Naibu Waziri.Basi.Nasisitiza,urais hauwezi.Hafai.

CCM watajitahidi kuhakikisha kuwa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA,vinasimamisha wagombea dhaifu ili wao apite hata kwa kuchakachua tena. Huu ndio mtego pekee ulibakia kwa CCM. Chokochoko ndio zimeanza hizo...

anhaa kumbe ulimchagua handsome eeh??bora umejuta..kama wewe ndio mnajuta vizuri sasa hhivi.
 
Sure.. Hata yeye mwenyewe anajua kuwa Hawezi kuwa Rais wa Tanzania. Hizi harakati za ccm kuanza kumnadi ili kuivuruga kichwa Chadema zimeshashindwa kwa sababu by the way maamuzi ya Chadema yanafanywa kwenye vikao mahsusi vya chama na si JF.

Perfect, rafiki. Zito anashirikiana na CCM kuiua CDM. Huwezi kusema urais sasa wakati chama bado hakijawa na mizizi vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Utakuwa unajidanganya. Vijana hawapigi kura ni ushabiki tu, huwa hawajiandikishi. Zito kijenge chama kwanza then fikiria hayo madaraka.
 
Watu bana.. yani wewe asubuhi yote hii umeaka na Zitto? una lako jambo wewe
 
mnasubiri aliyeandikiwa na mungu awe rais au tunatumia akili zetu kuangalia uwezo wa mtu??watanzania bado tupo nyuma sana
Pole yako mwenzangu mtangulize mwenyezi mungu kwenye kila jambo lako,hata kwenye kuchagua kiongozi...
 
gazeti la mwananchi nalipenda sababu huwa linamkampenia sana zitto..this is good for the opposition..keep it up mwananchi kwa kumpendelea zitto!!!
 
hata JK aliutafuta urais kwa bidii kama zitto na matokeo yake kaishia kuwapaka matope wenzake ili aupate mwisho wa siku umemshinda sasa anatapatapa tu uchumi dollolo, heshima kwisha , muungano umemshinda na utamfia mikononi mwake, ccm nayo inamfia mikononi mwake.

Cha ajabu zitto naye kaanza kwa staili ya JK ATAWACHAFUA SANA WENZAKE TUSUBIRI TUONE
 
Kwani Nyerere aliongoza Tanganyika akiwa na miaka mingapi? Vipi kuhusu maono, haiba na weledi wa kiungozi kati ya Zitto na mwalimu? Kwa wataalamu wa chambuzi linganishi (comparative analysis) naomba mnisaidie ikiwa haya mambo yana-matter kwenye uongozi wa nchi.
 
hata JK aliutafuta urais kwa bidii kama zitto na matokeo yake kaishia kuwapaka matope wenzake ili aupate mwisho wa siku umemshinda sasa anatapatapa tu uchumi dollolo, heshima kwisha , muungano umemshinda na utamfia mikononi mwake, ccm nayo inamfia mikononi mwake.

Cha ajabu zitto naye kaanza kwa staili ya JK ATAWACHAFUA SANA WENZAKE TUSUBIRI TUONE


Hamna lolote udini tu unawasumbua!
 
Zitto ANAWEZA kuwa rais wa nchi hii, ila sio 2015 au 2020 ni miaka ya huko mbele kabisa baada ya kupikwa na kuiva. Kwa sasa tunataka rais jasiri atakayepambana na rushwa. Atakaye mpeleka mtu yeyote mla rushwa mahakamani hata kama ni Rostam au JK. Zitto ni victim wa mfumo wa CCM ulioshindwa ambao umemteka na ameishakaa meza moja na akina Lowassa na Rostam na wamemfundisha namna ya kuishi kijana. Kwa hiyi aishi kwenye system iliyonyooka hadi nchi ikae kwenye mstari ndio aombe kugombea. Kwa sasa Zitto kama Zitto huyu kibaraka hawezi kuiweka hii nchi kwenye mstari, hawezi kamwe kwani hata yeye anatakiwa kuwekwa kwenye mstari
 
Hata kama atanunuliwa kurasa za mbele za magazeti na kupambwapambwa kila mara,bado Zitto Zuberi Kabwe hawezi kuwa Rais wa nchi hii.Namheshimu sana Zitto Kabwe.Namkubali kwa uwezo wake wa kiuongozi.Lakini kwa la Urais,bado hajakomaa. Kuchagua kijana/handsome tumekoma. Zitto labda anafaa kuwa Waziri au Naibu Waziri.Basi.Nasisitiza,urais hauwezi.Hafai.

CCM watajitahidi kuhakikisha kuwa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA,vinasimamisha wagombea dhaifu ili wao apite hata kwa kuchakachua tena. Huu ndio mtego pekee ulibakia kwa CCM. Chokochoko ndio zimeanza hizo...

Urais si kusema sana kwenye vikao kama anavyofanya Zito na Anne Kilango Malecela, hapana, busana , hekima ndio nguzo kubwa ya kiongozi hodari. zito hana sifa hizo!
 
Hata kama atanunuliwa kurasa za mbele za magazeti na kupambwapambwa kila mara,bado Zitto Zuberi Kabwe hawezi kuwa Rais wa nchi hii.Namheshimu sana Zitto Kabwe.Namkubali kwa uwezo wake wa kiuongozi.Lakini kwa la Urais,bado hajakomaa. Kuchagua kijana/handsome tumekoma. Zitto labda anafaa kuwa Waziri au Naibu Waziri.Basi.Nasisitiza,urais hauwezi.Hafai.

CCM watajitahidi kuhakikisha kuwa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA,vinasimamisha wagombea dhaifu ili wao apite hata kwa kuchakachua tena. Huu ndio mtego pekee ulibakia kwa CCM. Chokochoko ndio zimeanza hizo...
Mtajitahidi sana kuwakingia kifua SLAAN na MBOWE lakini mwisho wa siku dogo ZITTO atakuwa juu. Hivi unafikiri ZITTO huyo PADRI ukiwanadi kwa watanzania nani angalau atatoa upinzania kwa Magamba? SLAA wa 2010 siyo wa sasa, huyu kachoka kwanza 2010 atakuwa na familia mbili tena zinazohasimiana, itabidi awe na muda wa kutatua matatizo ya kifamilia. ZITTO itabidi kabla ya 2015 apate jiko kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro.
 
Habari yenyewe hii hapa....

Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015 Send to a friend
Monday, 23 July 2012 08:18




0diggsdigg

0000000kabwe.jpg
Mbunge Zitto Kabwe

NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS
Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar
IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.

Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.

Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.

Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.

"Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

"Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.

Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

‘Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.

Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.

Mdee amliza Zitto
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe' katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.

Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.

‘Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee.

Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.

Zitto akiri kutoa machozi

Zitto alipulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na kushindwa kujizuia jukwaani.

" Kwa weli Halima Mdee aluzumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto.

Alisema amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya Kigoma.

Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya eneo hilo.

‘Wapo watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.

Wabunge waliohudhuria

Wabunge waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee , Amina Mwidau wa viti maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi), Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti maalumu kutoka Pemba.

Kauli ya Nape
Alipoulizwa Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.

"Nyie andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo," alisema Nape.
 
Kama ZITTO hawezi kuwa rais, basi CHADEMA hakiwezi kutoa Rais. Seriously mtu pekee mwenye uwezo na anayekubalika na makundi yoye ya watu ni ZITTO! Hakuna mwingine ndani ya CDM!
 
kama zitto hawezi kuwa rais, basi chadema hakiwezi kutoa rais. Seriously mtu pekee mwenye uwezo na anayekubalika na makundi yoye ya watu ni zitto! Hakuna mwingine ndani ya cdm!


zitto ni ccm c, hakiwa rais zito hakuna tofauti na ccm iliyopo madarakani full stop.
 
Pamoja na agenda kuu kuwa ni kuondoa walaji 2015 matokeo ni muhimu zaidi .
 
Najua kuna mbinu nyingi zitatumika ili kudhoifisha nguvu za upinzani,na kuna kamchezo katachezwa kabla ya 2014, ili kuharibu dira ya vyama vya upinzani vyenye nguvu.wanamageuzi wa upinzani wawe makini kuyapokea na kuyafanyia kazi haya yote.mwalimu alisema kiongozi lazima awe amekomaa katika safu ya uongozi kwa muda wa kutosha.sasa tupime uwezo,uzoefu,maadili,utashi na weledi
 
Zito sio kijana mtetea wanyongealikuwa hivyo kabla hajanunuliwa...aah haha aahha...shv zito anatengenezewa umaarufu hata kelel anazopiga juu ya ccm anatumwa na zinaratibiwa na kumalizwa na CCM ....ulishaona wapi duniani kote mtu aliye threat kwa serikali tawala hapati misukosuko kama zito???mambo yake yananyooka tuu na offer za kutembelea mataifa makubwa kila siku funguka akili zitooo sio mpinazni tena eh eh ehehe nashangaa hata chadema bado wanamuendekeza nn piga chini huyo ndio wanawapunguza speed ya kwenda ikulu lol...politics mabaya sn
 
Ndio maana mimi namkubali sana John Mnyika, huyu kijana yupo makini sana na kauli zake, yupo busy kutumikia wananchi na kukieneza chama chake, hauwezi kumsikia ktk mambo ya uraisi huyu kijana. viva Mnyika.
 
Back
Top Bottom