Zitto asafishiwa njia mbio za urais 2015 na wabunge vijana akiwemo Nasaari na Filikunjombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto asafishiwa njia mbio za urais 2015 na wabunge vijana akiwemo Nasaari na Filikunjombe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Jul 23, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,378
  Likes Received: 8,537
  Trophy Points: 280
  Source Mwananchi

  Mbio za urais kwa vijana na hasa ndani ya vyama unamwelekea vizuri Zito Kabwe hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya katiba kupunguza umri wa kugombea na kuruhusu vijana kuwa na sifa za kugombea nafasi hiyo ya juu ya kiungozi.


  NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS

  Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar

  IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.

  Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.

  Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

  Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.

  Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.

  "Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

  "Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."

  Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

  Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.

  Kauli ya Nassari
  Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

  "Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nassari.

  Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.

  Mdee amliza Zitto
  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe' katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.

  Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.

  ‘Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee.

  Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.

  Zitto akiri kutoa machozi

  Zitto alipoulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na kushindwa kujizuia jukwaani.

  "Kwa kweli Halima Mdee alizumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto.

  Alisema amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya Kigoma.

  Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya eneo hilo.

  ‘Wapo watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.

  Wabunge waliohudhuria

  Wabunge waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee, Amina Mwidau wa viti maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi), Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti maalumu kutoka Pemba.

  Kauli ya Nape
  Alipoulizwa Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.

  "Nyie andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwasababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo," alisema Nape
   
 2. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Subiri uone wafuasi wa malaika mkuu Gabriel'a.k.a Slaa waje wakushambulie hapa'
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hatuna muda wa kuchagua rais kibaraka 2015
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  mbona hata slaa ni kibaraka? Hujui kama anawatumikia kwa moyo wote usalama wa ccm?
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  NINAMPENDA SANA KIJANA HUYU KWA SABABU ANAJUA TANZANIA INAKWENDA WAPI. Aliwahi kuielezea vizuri sana high unemployment kwa vijana wa tanzania siku aliozongwa na vijana wa kigoma kutaka ajira. Mungu mbariki kabwe!
   
 6. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hatuhitaji rais kijana 2015
  tunahitaji Rais anayejua atalifanyia nini Taifa.
  Hata hivyo bado Zitto hajakomaa kushika nafasi kubwa kama ya Urais wa nchi kubwa kama Tanzania. Labda Zanzibar.
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujua mtu ni mdini
  1. Ukimwambia serikali ya sasa ni tofauti na ya awamu ya 1,2 na 3.Atakwambia kivipi wakati Jk kachukua nchi haina shule nyingi,wahitimu shule za juu sasa large in number..Ukimwamibia katika utawala wa Nyerere palikuwepo uhadirifu kazini. ATABISHA.
  2. Ukimuuliza mwanasiasa gani msomi na mwenye uwezo wa kuitoa Tz hapa ilipo baada ya Jk atakwambia Lipumba, ukimuuliza sababu,utasikia Mwanauchumi bora, aliwahi kusema kila mtz anatakiwa kila mwezi kuwa analipwa takribani 4laki kila mwezi.Lakini ukiuliza kuhusu Slaa na sela ya cement 5000 atakwambia muongo.
  3. Mwanasiasa gani unamkubali Chadema? Atakwambia Zitto Zuber Kabwe.
  4. Vipi mwamuko wa watanzani katika siasa na jinsi walivyo kipokea chama cha CHADEMA? Atakwambia,tuliwahi kumwona Kaburu,Cuf na Mrema
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dr. anajiandaa wengine wanataka kuharibu sherehe! Yaani watu wabaya, Dr. anapata first lady watu wengine wanasema Zitto ndio agombee!
   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Nyie vijana, mkiivuruga CDM mtaishia pabaya, hata huko 2015 hamtafika kwa matumaini. Sidhani nyie vijana mnaweza kuisimamia CDM wazee wenu wakijitoa. Yangu macho, badala ya kukijenga chama kwa muda uliobaki mnakimbilia urais, vijijini hamjulikani inajulikana CCM!!! Ndio maana nasema vijana mnastahili kucheza bongo fleva!!!
   
 10. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Zito bado, busara zaidi zinahitajika katika nafasi ya urais. ndio maana hata JK ameshindwa maana hana busara inayotumainiwa. ni ujana tu na cheap populality!!! Zito hana busara, hana maono! hawezi kuona mbali wala kuhisi ajali ya mbali!!!
   
 11. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hahahaaaa ndoto za mchana, hii ni mikakati ya waislamu ili mdini mwingine zitto agombee, Kama wakiona mambo Hayako sawa Nyinyiem, mkakati mwingine ni kulazimisha hoja ya rais ajae atoke Zanzibar ili mradi tu successor aw ****** awe mwislamu. Huhuhuuuuuuuuu! Nakuunga mkono Precise pangolin
   
 12. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hatusumbuliwi na kelele zenu, kwani itakayoamua mgombea wa uraisi wa cdm ni nec ya cdm na co wana-ccm
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kwani 2015 zito atakuwa na miaka mingapi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Zitto anaweza, by 2015 atakuwa amekomaa vya kutosha. Kura zetu zipo ajipange vizuri atazipata.
   
 15. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Hata kikwete tulimshadadia tukidhani kwa nchi kupata kijana tutasonga mbele kwa haraka .Na kweli kikwete akaja na sera ya ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA matokeo yake akashindwa kufikia rekodi ya mzee mkapa tuliemuona mzee.Zitto hawezi tena kwa taarifa yeniu zitto hataweza kwani hata utaratibu tu wa movement ya documents ofisini hajui yeye kaanza na ubunge hajawahi kutumwa na boss yeyote, zitto hajui kazi za mhudumu nini kwani hajawahi kufanya kazi ofisini.Atakachofanya ni kuvuruga utaratibu mzima wa utendaji kazi serikalini na matokeo yake mabaya sana.

  Kithibitisho ni juzi alipotaka kuitisha kikao cha POAC kutka kumtetea mhando wa TANESCO eti kwa kigezo kuwa kamati yake haikuridhishwa na jinsi alivyosimamishwa.Swali dogo kwa zitto je anajua kama ana kazi ya kuisimamia serikalikama mbunge??? haoni kwa kumtetea mhando ni kuingilia kazi za kila siku za serikali.na je ikija kuonekana kweli mhando ana makosa zitto atapata wapi nafasi ya kuishauri seikali???

  Ndioyo maana nasema zitto si mzuri sana kwani kuna step aliiruka ni ile ya utumishi ajue system ya serikali inafanyaje kazi>
  Yeye hajui hata kwa nini kuna fungu la chai ofisini.
  Nawashauri wanaompigia debe wafikirie mara dufu Zitto ni tatizo kama ataingia ikulu ni bora akabaki back benchers tuuuu.vinginevyo watanzania tutalia
   
 16. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Wakuu nachoweza kuwaambia hawa CDM wakianza mgogoro kwenye mgombea Urais 2015 basi CDM we are Dead.
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Umeongea point ya msingi sana, inawezekana wengi wasiione!
  "huwezi kuwa good manager, kama hujawahi kuwa managed"

  Hoja ya "ujana" katu siiungi mkono sababu sio hoja wala sio sifa ya msingi sana linapokuja suala la UONGOZI WA JUU kabisa wa nchi.
  Hii kwangu haijalishi kama ni Zitto au mwingine awaye yeyote!
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu uko sahihi, lakini wenye mawazo ya namna hii wengi ni watu wa kwenye vijiwe vya kahawa!
  Ukitoka kwenye ban utakuta notification mkuu Precise pangolin*
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 180

  Nadhani wakati kama huu chama kinatakiwa kuwa makini sana vyombo vyetu vya habari. Kwa mwendo huu wa kutafsiri mambo hivi chama hakitajengwa.
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Hivi vitu vinashangaza sana,kuna wakati unaiona CDM ambayo haijafikia hata nusu ya umri wa CCM wakianza kuelekea kwa kasi walipo sasa CCM! Kibaya zaidi sisi wenyewe vijana ndio waharibifu (nafuu CCM imeharibiwa kwanza na wazee).

  Mtu anautaka URAIS na sasa mtandao wake umekomaa tunaanza kuaminishana vile vile kama ilivyokuwa 1995! Inashangaza sana kwakweli!
   
Loading...