Zitto arudishiwa uongozi wa Bunge na CHADEMA, wamtambua Kikwete

Nimeipenda ya MJJ aliyotoa hapo juu. Tanzania ngumu Bwana. Yaani unaweza soma maneno ya watz hapa JF mwishoni ukabakia kuita Mungu!
 
NCCR MAGEUZI wamemuahidi Uenyekiti wa Chama na agombee urais mwaka 2015 kama walivyofanya kwa AL.Mrema. Dogo bado analitafakari hili ingawa kuna nguvu kubwa ya marafiki zake wa CCM wanaotaka kumsajili kwa udi na uvumba!! CUF nao wanamtaka kwa mgongo wa udini, wanapiga chapuo eti waislamu hawako salama wakiwa CHADEMA!!!! Kwa kweli nchi hii imelaaniwa kama mambo yenyewe ndiyo haya!!

Huyu dogo mwisho atachanganyikiwa na sijui mtasema nani kamloga!

2015 Zitto atakuwa na umri wa miaka 39 ambayo inamkosesha sifa ya kugombea urais! Usitufunge kamba hapa!
 
2015 Zitto atakuwa na umri wa miaka 39 ambayo inamkosesha sifa ya kugombea urais! Usitufunge kamba hapa!
Mbona tunaongelea sana umri wa Zitto nasema hata angekuwa na miaka 60 mwaka huo hafai kuwa kiongozi wa kitaifa anavyopenda pesa huyu kwa tamaa zake anaweza hata kutuuza wazima wazima.
 
Kwa maoni yangu naona Chadema imfukuze Zitto katika chama mara moja bila ya kusita. Zitto anaonesha wazi kwamba hana mapenzi tena na Chadema, anaweza akawa amesilimu na kuwa CCM ama chama kingine cha upinzani hapa Tanzania.
Chadema wachukue uamuzi wa kumfukuza haraka bila ya kumuhofia wala kumchelewesha. Hawawezi kuwa na nyoka ndani ya nyumba, kwa mtu mwenye upeo utaona wazi kabisa kwamba Zitto anaweza kutumiwa na CCM na akauza ama akatoa siri za Chadema. CHADEMA FUKUZA ZITTO MARA MOJA.
 
Everyday narudia mtu amesha kusaliti, what are you going to question him? fukuza, what is natural justice kwa msaliti? na si kwa tukio moja, hata kafikia hatua ya kutaka serikali inunue Dowans, wamfukuze, we are here sooooooo brilliant, tough, intellectuals, wa CDM, formula makers, think tank, mentors, mtoeni
haraka, huyu kalewa umaarufu na harufu nyingi za ufisadi ananukia, get him out CDM, na iwe mwisho kuongelea Zitto, Zitto...... who is he by the way so far? amefanya nini sana, lipi? hata 10% ya Dr Slaa hana, mtoeni huyu, plse msipoteze muda wetu, then tusonge mbele, ndio maana tunaibiwa kwa mikataba mibovu, mafisadi tunaendelea kucheka, we are very hard to make a decision hata kwa vitu viko wazii, hii hatari sana, toa huyu
 
Get him out huyu ni Yuda Eskariot, no delay please we are feed up oof him wazuri CDM wengiiiiii mno, na niseme CDM ina wana CCM wengi wa kweli mno under cover wenye uchungu na nchi yao, mtoeni huyu Zitto kaonyesha mwenyewe kwa matendo hafai, Dunia(maisha) ni mwalimu wa mwisho usifikiri umemaliza kusoma
 
Chadema in reconciliation trend

By DAILY NEWS Reporter, 12th December 2010 @ 22:00, Total Comments: 0, Hits: 19

WHILE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) is on Monday expected to reveal the resolutions made by the party's central committee on Saturday, information from insiders shows that the party had resolved to recognise Mr Jakaya Kikwetes as the President of the United Republic of Tanzania.

The committee had also resolved to suspend a decision made by the party's Members of Parliament last week to strip Kigoma North MP Mr Zitto Kabwe of his position as Deputy Opposition Leader of Parliament.

Soon after the elections, CHADEMA refused to recognise Mr Kikwete as the president alleging that he was declared winner in a ‘flawed election.' The party's' legislators walked out of the parliament, moments after President Kikwete had started his speech to inaugurate the National Assembly in Dodoma last month.

Sources from the committee told this newspaper that the party had resolved to recognize President Kikwete after a heated debate and weighing the possible repercussions of not recognising him.

On Zitto's issue, the sources said, veteran and powerful members of the committee defended him and ruled that the legislator was not given right to a fair hearing as he had not been given chance to defend himself.

Chadema's MPs met in Bagamoyo last week and cast a vote of no confidence against Mr Kabwe, allegedly for acting contrary to the party's decision to walk out when President Kikwete was addressing Parliament last month.

Mr Kabwe who did not answer his phone when contacted yesterday, had been admitted to Aga Khan Hospital since Thursday last week for food poisoning.

Chadema central committee also formed a four-member special committee led by Prof Mwesiga Baregu to ‘put the house in order.' When contacted, Prof Baregu confirmed, noting that the special committee had been tasked with ensuring harmony is restored in the party.

"Yes, there is a special committee comprising the elderly in the central committee, to ensure unity and harmony is restored in the party," Prof Baregu said.

"We will talk with party members who have complaints against the party. We do not want to lose public trust," he said.

Ms Shida Salim, Mr Kabwe's mother, is among Chadema's special committee. The party's Secretary General Dr Willbrod Slaa declined to comment, saying he would brief journalists on Monday.
 
Chadema wamtambua Kikwete

Imeandikwa na Waandishi Wetu; Tarehe: 13th December 2010 @ 06:31

JAKAYA Kikwete aliwaambia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba hawana mwingine wa kumlilia kwa masuala yao, isipokuwa yeye; na kwamba watakwenda na kurudi kwake kwa sababu yeye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Novemba 18, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma wakati akihutubia Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 10,na sasa aliyoyasema yametimia.

Baadhi ya wabunge wa Chadema walitoka katika ukumbi wa Bunge wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe walitoka nje mara tu Rais Kikwete alipoanza hotuba yake, sasa wamekubali yaishe. Wanamtambua ndiye Rais halali wa Tanzania.

Lakini katika kauli iliyowalenga moja kwa moja wabunge wa Chadema wakati akimalizia hotuba yake bungeni, Rais Kikwete alisema wabunge hao hawana wa kumlilia zaidi yake, kwani yeye ndiye Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Watakwenda watarudi, hawana mwingine wa kumlilia kwa yao, isipokuwa Serikali ya CCM ambayo mimi ndiye Rais wake; Dk. Mohammed Gharib Bilal ndiye Makamu wake. Serikali ambayo Dk. Ali Mohammed Shein ndiye Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa Rais na Balozi Seif Ali Idd ni Makamu wa Pili wa Rais,” alisema Rais Kikwete, Novemba 18, mwaka huu na kushangiliwa na wabunge.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho katika siku za karibuni, kilitangaza kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, kimebadili msimamo.

Kimekubaliana kwamba Kikwete ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kinatarajiwa siku yoyote kuanzia leo kutangaza maazimio ya Kamati Kuu iliyokutana mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, ambayo moja ya maazimio yake, ni kumtambua kiongozi huyo wa nchi.

Kamati Kuu ya Chadema pia imeamua kusitisha uamuzi wa wabunge wa chama hicho kwa kumvua nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, mbunge mwenzao, Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini.

Baada ya Rais Kikwete kutangazwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Chadema ilikataa kumtambua, ikidai alichaguliwa kutokana na uchaguzi uliokuwa na udanganyifu.

Novemba 18, mwaka huu, wakati akianza hotuba ya kulihutubia Bunge jipya mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wa Chadema waliokuwa ndani ya ukumbi wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, walitoka nje ya ukumbi huo.

Lakini sasa, vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kamati Kuu ya Chadema, vimeliarifu gazeti hili kuwa wamekubaliana kumtambua Rais Kikwete baada ya mjadala mzito na baada ya kupima athari za kutomtambua Rais Kikwete aliyeshinda kwa zaidi ya asilimia 60.

Kuhusu suala la Zitto, chanzo hicho cha habari, kilieleza kuwa wajumbe wakongwe wa Kamati Kuu walimtetea na kueleza kuwa mbunge huyo machachari hakupewa nafasi ya kujitetea.

Wabunge wa Chadema walikutana Bagamoyo wiki iliyopita na kupiga kura ya kutokuwa na imani na Zitto, wakimtuhumu kwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama hicho wa kumsusa Rais Kikwete bungeni.

Zitto hakupatikana kuzungumzia hatua hiyo mpya ya chama chake jana, kwa sababu simu yake iliita bila kupokewa, ikiwa ni siku moja baada ya kutoka Hospitali ya Aga Khan ambako alikuwa amelazwa tangu Alhamisi iliyopita, kwa kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, ikidaiwa alikula chakula chenye sumu.

Kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa ndani ya chama hicho, Kamati Kuu iliamua pia kuunda kamati maalumu ya watu wanne ikiongozwa na Profesa Mwesiga Baregu, kwa nia ya kurejesha amani kundini.

Kamati hiyo kwa maudhui, inafanana na ile iliyoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juni mwaka huu, ikiongozwa na Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi kupatanisha makundi hasimu yaliyokuwa yameibuka ndani ya wabunge wake.

Alipoulizwa kuhusu kamati hiyo, Profesa Baregu alithibitisha na kueleza kuwa Kamati yake imepewa jukumu la kuhakikisha amani inarejea katika chama hicho.

“Ndiyo, kuna kamati maalumu inayowahusisha wajumbe wakongwe wa Kamati Kuu iliyoundwa kwa ajili ya kuhakikisha umoja na amani zinarejea katika chama,” alisema Profesa Baregu.

Alisema kurejeshwa kwa umoja na amani katika chama hicho, pia kutahakikisha umma haupotei imani yao kwa chama hicho cha upinzani.

“Tutazungumza na wanachama ambao wana malalamiko au wana matatizo, ili kumaliza tofauti zao na kurejesha tena mshikamano, amani na upendo katika chama…hatutaki kupoteza imani ya umma kwetu,” alieleza Profesa Baregu.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Shida Salim ambaye ni mama mzazi wa Zitto, Kitila Mkumbo ambaye ndiye Katibu na mjumbe mwingine aliyetajwa kwa jina la Shilungushela.

Katibu Mkuu wa Chadema, alikataa kuzungumzia maazimio hayo jana alipotafutwa kwa simu, lakini akaeleza kuwa watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho.
 
Maneno mazito sana haya, kwa mwenye kuelewa:

“Watakwenda watarudi, hawana mwingine wa kumlilia kwa yao, isipokuwa Serikali ya CCM ambayo mimi ndiye Rais wake; Dk. Mohammed Gharib Bilal ndiye Makamu wake. Serikali ambayo Dk. Ali Mohammed Shein ndiye Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa Rais na Balozi Seif Ali Idd ni Makamu wa Pili wa Rais,” alisema Rais Kikwete, Novemba 18, mwaka huu.
 
Zitto, Shibuda waundiwa kamati


Na Mwandishi Wetu
Zitto, Shibuda waundiwa kamati


Na Mwandishi Wetu


WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikitarajiwa kutoa msimamo wa chama hicho juu ya masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini na ndani ya chama hicho, imeelezwa kuwa Mbunge wa
Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe ametakiwa kujipima mwenyewe kisha ajiuzulu, baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wa chama hicho.

Imeelezwa kuwa kura za kutokuwa na imani naye, zilizopigwa wiki iliyopita na wabunge wa CHADEMA katika kikao cha kamati yao, kilichofanyika Mjini Bagamoyo, hakizumwondoa moja kwa moja katika cheo chake cha naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, bali ilikuwa ni ishara ya kuwa watu anaowaongoza bungeni hawana imani naye tena hivyo kumtaka afikirie mwenyewe kisha achukue uamuzi wa kujiuzulu kabla wabunge hao hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zimebainisha pia kuwa Kamati Kuu iliyoketi mwisho wa juma katika kikao maalumu, imeunda kamati kwa ajili ya kumshauri Bw. Zitto, baada ya wajumbe kuona kuwa kuna umuhimu wa kumsaidia ushauri nasaha kutokana na mwenendo wake ndani ya chama hicho.Vyanzo mbalimbali vimesema kamati hiyo inajumuisha Profesa Mwesiga Baregu, Dkt. Mkumbo Kitila, Shida Salum na mwanachama mwingine wa chama hicho.

Mbali ya kubainika kwa suala hilo, pia habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika zimeeleza kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA, imeunda kamati nyingine kumchunguza Mbunge wa Maswa Magharibi, Bw. John Shibuda, kutokana na tuhuma zilizowasilishwa na kamati ya wabunge, iliyokutana wiki
iliyopita Mjini Bagamoyo.

"Nafikiri hilo la Zitto waandishi wamwelipotosha kwa kiasi kikubwa, mimi ninavyojua walichofanya wabunge wale ni kupiga kura ya kutokuwa na imani naye (Zitto), kisha mwenyewe apime uzito wa uamuzi huo kuwa watu anaowaongoza hawana imani naye, kisha mwenyewe ajiuzulu, kabla wabunge wenyewe hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

"Hata hivyo uamuzi huo wa kuchukua hatua za kinidhamu ikiwemo hata kumwondoa katika cheo hicho, imo katika mamlaka ya Kamati ya Wabunge wa CHADEMA, yaani Party Caucus, wanayo mamlaka hayo kabisa wakiona kuna haja ya kufanya hivyo, baada ya yeye kushindwa kuchukua hatua yoyote hasa kujiuzulu maana ni kiongozi wao wenyewe, hivyo haihusiani na chombo kingine ndani ya chama."Kumbuka pia kuwa naye ataitwa kama alivyoitwa wengine kuhojiwa juu ya kutotekeleza maamuzi halali ya kikao ya kuingia ukumbini siku ya ufunguzi wa bunge kama
ilivyokuwa imeamuriwa...lakini cheo hajavuliwa, mwenyewe apime kisha ajiuzulu," kilisema moja ya chanzo chetu cha habari.

Chanzo chetu kikiwa na tahadhari ya kutotaka kufafanua masuala mengi, pia kilisema kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imeona kuna umuhimu kukaa na Bw. Zitto kisha apatiwe ushauri juu ya mwenendo wake wa kisiasa akiwa kama mmoja wa viongozi waandamizi wa chama hicho, ambapo mbali ya kuwa ni naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara.

Nafasi hiyo ya naibu katibu mkuu bara, inamfanya kuwa mmoja wa watu wawili wanaomsaidia Katibu Mkuu Dkt. Willibrod Slaa, mwingine akiwa ni Hamad Mussa Yusuf, kwa Zanzibar, lakini nafasi ya naibu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, inamfanya kuwa msaidizi wa Mkuu wa Kambi, Bw. Freeman Mbowe.

Kwa upande wa suala la Bw. Shibuda, vyanzo vyetu vilieleza kuwa mbunge huyo ambaye alihamia CHADEMA kutoka Chama Cha Mapinduzi, siku chache kabla ya kampeni za uchaguzi kuanza, baada ya kubwagwa katika kura za maoni, atachunguzwa kwa tuhuma kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutotii maagizo na maamuzi kikao halali cha chama, kulaumu na kulalamikia nje ya chama maagizo na maamuzi hayo, kujaribu au kutaka kuleta mgawanyiko ndani ya chama.

"Bw. Shibuda alisema hana kosa wala hana haja ya kuomba msamaha, chanzo hicho kilisema wabunge walikuwa wazi kabisa kwake, wakimwambia asifikiri wanamwogopa, asifikiri kuwa wao hawakushinda uchaguzi...maana amekuwa akijigamba kuwa yeye ametumwa na watu wa Maswa.Juhudi za gazeti hili kuwapata viongozi wa chama hicho kuzungumzia taarifa hizo hazikuzaa matunda jana.
 
Kama alivyosema mwenzetu mmoja hapo juu "this is a new thread with old story".

Gazeti la CCm na habari leo wameandika kwa ushabiki na baadhi wa wana Jf wanaanza kudiscuss bila kurejea theads za hapo mwanzo.

Mimi sijaona tatizo katika hili maana inabakia kuwa CHADEMA WANATAMBUA JK NA URAISI WAKE toka siku ya kuapishwa LAKINI HAWATAMBUI MATOKEO YALIYOMUWEKA MADARAKANI. This is clear and no more!
 
Let me put short and simple- Chadema inataka kuongoza mabadiliko lakini haiko tayari kulipa gharama yake. Kwamba watapoteza imani na baadhi ya watu hilo halina ubishi. Wanachohitaji sasa ni kuwaomba radhi watanzania.
 
Back
Top Bottom