Zitto arudishiwa uongozi wa Bunge na CHADEMA, wamtambua Kikwete

japo zityo kashanitoka rohoni, nadhani wametumia busara. ngongano ni fursa ya kujenga. tujenge CHADEMA yenye kutoa fursa sawa kwa wanachama wake wote. tujenge CHADEMA salama yenye taratibu zinazoeleweka. si umeona jinsi ccm walivyomute kumtimua makamba? simply wamesema uchaguzi ufike....isije kuwa ile ya sitta kunyimwa kugombea wakati ashajaza fomu...CHADEMA OYEEEEEE!!
 
HAHAHAHA hiyo ni retreat! KATIBA haiwezi kufutwa ili jk asiwe raisi kwa sasa! yeye ni raisi, japo aliupata kwa kuchakachua....

methodology ya kuingia ikulu ndiyo ya kubadilisha!!!!

chadema bado wana akili!
 
CUF kiwe chama cha upinzani tanganyika hata chadema nao wawe wapinzani? Wapi na wapi? Chama cha promotion tu wakati wa uchaguzi. Uchaguzi ukipita kwisha. Mtambueni ccm mwenzenu kikwete. Mmeanza lini kuwa wapinzani? Kelele tu.
 
Umenichanganyia hiyo hoja kama ambavyo kuuelewa utatu unavyonichanganya mpaka leo.
Rais anatambuliwa, matokeo hayatambuliwi! Hii ni ajabu na kweli!

Si uwe jasiri na ukubali makosa tu kama mwenzio Mzeemwanakijiji! Kafanya ujasiri na kakubali.

"Asiyekubali kushindwa si mshindani"

Nadhani kuna watu wana matatizo ya kusoma. Nimekubali makosa gani na wapi?
 
MKJJ;

CHADEMA hawapaswi kuomba radhi hata chembe kwani madai yao ni ya msingi kabisa;haiwezekani uteua TUME YAKO then isimamie uchaguzi ambao wewe BOSI WAO unashiriki;isitoshe hamna sehemu ambayo CHADEMA ILIPINGANA na katiba inayosema kuwa TUME ikitangaza matokeo hauwezi yapinga popote pale isipokuwa ilitaka KUIONYESHA DUNIA kuwa njia inayotumika kumuingiza madarakani Rais JK ni haramu!

Chadema wamenegate hoja zao zote za kuwa uchaguzi haukuwa free and fair na kuwa tume iliboronga. Period. Utalalamikia vipi uchaguzi wakati umetambua matokeo yake unqualified? Ndio maana nimesema waombe radhi kwa sababu they are acting as they are the ones who ruined this election. Instead of acting at they should be - victims of a corrupt political system; Chadema by they are very acts ndio wanaonekana kama wameikosea serikali na CCM! this is pathetic stand of the first order.
 
Ukiangalia hapo kwenye taarifa ya hali halisi. Utaona watu wanamjadili Zitto kama mtu mwenye makosa. Mbona hamsemi kwamba Zitto ni MSHINDI? Hamuoni kwamba kamati kuu imeiagiza CHADEMA imtambue Rais? Kwahiyo hata hao waliopiga kura na kutoka Bungeni ndio wanamakosa na wao ndio wanastahili wahojiwe. Hivi huo uamuzi wa kutoka Bungeni ni nani mwenye final say? Au ni kujiamulia tu? Kiufupi kamati kuu inakubali kuwa Zitto alikuwa sahihi na kwahiyo hataadhibiwa. Tulisema na tutaendelea kusema, CHADEMA hawakujipanga na hawakujua kuwa kuna ishu zitajitokeza baada ya uchaguzi na hatimaye ndio mvurugano huu. Tunaendelea kusema, CHADEMA watazame saana muundo wa viongozi wao na nani hasa mwenye mamlaka katika CHAMA wakati huo wakizingatia maslahi ya CHAMA na wananchi kwa ujumla.
Labda wenye macho wanaweza kuyaona hayo! Ila ni wachache sana. Nilipata kusema pia na kwa sasa narudia tena kwa sauti kuu Mh. ZK anawazidi mbali sana kiupeo na kiuono viongozi wengi wa CHM, ukweli ni kwamba viongozi wengi wa CDM pamoja na wapenzi wao achilia mbali wanachama HAWAJUI NINI MAANA YA SIASA na HAWAJUI PIA NINI MAANA YA DEMOKRASIA! mimi hufikia hatua kuwaona kwamba wako kinyume na sera zao yaani.... sera tofauti na misimamo tofauti (WAWEZAJE KUWA MWANADEMOKRASIA HALI DEMOKRASI UMEIKANYAGA?) Inawezekana vipi utake kupigania kitu ambacho ndani kwako hujakikamilisha? Tubadilike na tuendane na tunayoyasema la si hivyo wakati utatuhukumu.

Ahsanteni kwa kunisoma!
 
Nadhani kuna watu wana matatizo ya kusoma. Nimekubali makosa gani na wapi?
Hilo ndilo tatizo letu kubwa! Si kusoma na kuandika bali kusoma na kuelewa pia!! Wewe utaandika kitu kingine mtu anakihariri kichwani mwake na kukileta kwa namna nyingine... hao ndio taifa linalokuja!!
 
Msimamo wa Chadema haujabadilika by Dr. Slaa


Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.


Source: Dr. Slaa wall post on facebook
 
Back
Top Bottom