Zitto, Arfi, Shibuda kujadiliwa Kamati Kuu...

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,691
10,114
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamemweka kikaangoni Mbunge wa Kigoma Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho, Zitto Kabwe, katika kikao chao kilichokaa jana mjini Bagamoyo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha ndani cha wabunge hao kilichokaa juzi na jana mjini humo mara baada ya semina ya wabunge wa chama hicho, wabunge hao walipiga kura ya kutokuwa na imani na uongozi wa Zitto na pia wamemtaka ajieleze kwanini asichukuliwe hatua kwa kutataa kuunga mkono uamuzi wa pamoja wa kususia hotuba ya Rais wakati yeye naye alishiriki katika kuufikia uamuzi huo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ndani ya kikao hicho, wakati uamuzi huo ukipitishwa, Zitto hakuwa katika kikao hicho ingawa alihudhuria kikao cha juzi.

"Tumeamua kuwa hatuna imani na uongozi (Zitto)," kimesema chanzo hicho. "Tumepitisha uamuzi wa pamoja. Ujumbe utamfikia, autafakari, kisha aamue mwenyewe."

Habari zaidi zinasema ingawa Zitto alikuwa Bagamoyo wakati kikao hicho kinafanyika, hakuhudhuria kwa sababu inadaiwa kuwa kutwa nzima ya jana alikuwa amepumzika akidai kuwa anaumwa.

Chanzo kingine ndani ya kikao hicho kimeliambia gazeti hili kuwa Zitto amekuwa mwiba kwa chama hicho.

"Apokee uamuzi wa kikao halali cha chama. Apime mwenyewe na achukue uamuzi," amesema mbunge mmoja katika chama hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Gazeti hili lilipowasiliana Zitto, simu yake ya kiganjani haikupatikana.

Miongoni mwa nyadhifa ambazo Zitto ameshikila lakini akapigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ni ile ya Umakamu wa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Kiongozi wa kambi hiyo ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Novemba 17, mwaka huu, wabunge wa CHADEMA, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, walitoka ndani ya ukumbi wa bunge mara tu Rais Jakaya Kikwete alipoanza hotuba yake ya kulizindua Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano.

Ingawa wabunge hao walitoka wakati Rais akianza kuhutubia, Zitto hakuwa Bungeni siku hiyo. Wengine ambao hawakuwa bungeni ni pamoja na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambao wanadaiwa kuwa walikuwa wanaumwa siku ya tukio, na mwingine ni Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ambaye alikuwa safarini Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vya siasa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, Chadema ilitangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais kwa madai kuwa taratibu na sheria nyingi zilikiukwa, ikiwa ni pamoja na ujumlishaji wa kura na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuingilia zoezi hilo kwa lengo la kumbeba mgombea wa chama tawala.
 
Kama hatua zinazo/zitakazochukuliwa dhidi yake zitafuata utaratibu/kanuni/katiba ya CDM, I dont see anything wrong. Isipokuwa tu wasimnyang'anye kadi -- maana Spika wa CCM anaweza akagoma, kama alivyogoma Msekwa kuhusu Wabunge fulani wa CUF waliofukuzwa chamani a few years back.
 
Asingeweza kutoka bungeni kususia hotuba ya rais kwani kuna taarifa kuwa ni Baba mkwe mtarajiwa. Hivyo angeweza kukosa mengi
 
Jamani ndugu tungeelekeza nguvu zetu kwenye more constructive things (katiba, tume mpya, ufisadi, bajeti iliyochakachuliwa) tujadili tunafanya nini.... hizi speculations will do no one any good ile thread ya bajeti iliyopelekwa kwa wahisani still needs watu kuichangia sio hizi issue
 
Kama hatua zinazo/zitakazochukuliwa dhidi yake zitafuata utaratibu/kanuni/katiba ya CDM, I dont see anything wrong. Isipokuwa tu wasimnyang'anye kadi -- maana Spika wa CCM anaweza akagoma, kama alivyogoma Msekwa kuhusu Wabunge fulani wa CUF waliofukuzwa chamani a few years back.

Nakuunga kwa hoja zako hapo juu.
 
hatimaye zitto kabwe amevuliwa unaibu kiongozi kambi ya upinzani bungeni, tukio hili pengine la kihistoria limetokea huko bagamoyo, katika semina ya wabunge wa chadema inayofanyika huko. mnamo majira ya mchana jana, yeye mwenyewe aliwasilisha paper na katika paper hiyo alijitetea kwa mengi yanayosemwa juu yake.

baadaye wabunge wa chadema walikutana kwa dharura na katika kikao hicho wabunge 28 walipiga kura ya kutokuwa na imani naye, wakati wabunge 8 wakibakia bila kuwa na msimamao, na mmoja akiwa amepiga kura ya kuwa na imani na zitto

nafasi yake bado iko wazi

chanzo, semina ya wabunge wa chadema inayoendelea huko bagamoyo
 
I liked Kalikawes Raggae which goes ''Panapofuka Moshi kuna moto chini'' RIP in peace my rasta farae!!
 
hatimaye zitto kabwe amevuliwa unaibu kiongozi kambi ya upinzani bungeni, tukio hili pengine la kihistoria limetokea huko bagamoyo, katika semina ya wabunge wa chadema inayofanyika huko. mnamo majira ya mchana jana, yeye mwenyewe aliwasilisha paper na katika paper hiyo alijitetea kwa mengi yanayosemwa juu yake.

baadaye wabunge wa chadema walikutana kwa dharura na katika kikao hicho wabunge 28 walipiga kura ya kutokuwa na imani naye, wakati wabunge 8 wakibakia bila kuwa na msimamao, na mmoja akiwa amepiga kura ya kuwa na imani na zitto

nafasi yake bado iko wazi

chanzo, semina ya wabunge wa chadema inayoendelea huko bagamoyo
Ni gharama za siasa hizo............. kama ambavyo ameshawahi kutamka
 
haya sasa. kwahiyo unamaanisha tuna wiki nzima ya kumjadiri zitto? inaboa sana.
 
nafiriki haitoshi na ule wa ndani ya chama pia wamvue, hafai huyo.abaki mwanachama wa kawaida, then aamue vizuri aende CCM au abaki CHADEMA, Hatutaki vibaraka sisi, atauza siri za chama kwa MAFISADI wa CCM na kutuvurugia mambo ndani ya chama.
 
baadaye wabunge wa chadema walikutana kwa dharura na katika kikao hicho wabunge 28 walipiga kura ya kutokuwa na imani naye, wakati wabunge 8 wakibakia bila kuwa na msimamao, na mmoja akiwa amepiga kura ya kuwa na imani na zitto

Kitendo cha kukaidi maamuzi ya vikao kwa kutoshiriki kumtoroka JK Bungeni ule ulikwa ni usaliti wa hali yta juu...halafu bado ana akili ya kitoto mno......................kauli zake ni kichekesho sana...........Hongera Chadema kwa maamuzi ya busara.....................
 
Back
Top Bottom