Zitto, Arfi, Shibuda kujadiliwa Kamati Kuu...

Mbona watu humu ndani mmetokea kumchukia Zitto? Hamkumbuki yeye ndiye aliyefanya chadema ipendwe na vijana??

Mkuu CHADEMA inapendwa na vijana si kwaajl ya Zitto bali ni sera na dira ya chama chao na watu watu wenye upeo wa kuongea ushuhuda wenye nuru na mstakabari wa Nchi hii kv huduma ya elimu bure, afya, malazi n.k ndicho kinatuvutia tuipende CDM kuwa inamwelekeo wa kile sisi Taifa la Leo nakesho tuhitaji.
Hata zitto alijiunga CDM kwa kuvutiwa na Manifesto ya CDM.
 
bora katoka..

YOU CAN START REVOLUTION BUT YOU CAN'T STOP REVOLUTION
 
VIVA Chadema, tunawaunga mkono, huyu jamaa(Zitto) ni mwiba ndani ya chama makini, avuliwe na unaibu katibu mkuu,Kama Chadema tuliweza kujitoa bungeni kwa nn tushindwe kumuadhibu huyu MSALITI, asanteni wabunge kwa kutokuwa na imani naye.wananchi tulishaanza kuichoka mienendo ya Zitto Kabwela
 
Kinachofurahisha chadema ni kuwa maamuzi mengi yafananayo na haya huwa yanafanyika wakati muhusika HAYUPO!
 
Mie siielewi kabisa sasa!

Kwani si kura zilipigwa? Maana ya kupiga kura si demokrasia? Sasa mtu akikataa hoja ni kosa?

Jamani mbona nachangannyikiwa hapa? Mhhh, maybe bado mchanga wa haya mambo ya kisiasa wacha nisikilize great thinkers mnasemaje..

Mana ndo mana kura ilipigwa from first place vinginevo wangetoa amri kwmba wasiingie then angekiuka ingekuwa kosa, sasa kura jamani?!he
 
Wacheni unafiki nyie mnajenga ama mnabomoa? Siwezi furahishwa na migawanyiko ndani ya chadema hata kidogo, kama Zitto kakosea wangemwonya kwa upole na sio kumkomoa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, mbona mnawapa ccm raha?

Namuomba muheshimiwa Zitto na wabunge wote wa CHADEMA waache malumbano washugulikie kero zinazowakabili wananchi, kwakweli mnatukatisha tamaa wafuasi wenu, hatuwaelewi huku mnataka katiba mpya mara mnapinga ufisadi mara malumbano baina yenu je? Mtafaulu kweli au mnasubiri mwaka 2015 tuwatoeni bungeni mkafie mbali.
 
Kwa kweli, inaumiza na kukatisha tamaa.

Tulimwamini Zitto naye akaaminika, Kama kweli amesaliti wenzake katika mapambano haya Mungu amsamehe. Kama bado nguvu ipo apewe onyo moja tuu la kuvuliwa madaraka awe mjumbe tuu wa kawaida na aendelee na Ubunge wake mpaka hapo itakapo onekana amekomaa kiuongozi.

Pia ushauli wangu aendelee na PHD yake bado tunaupungufu wa walimu huku vyuoni.

Mungu Ibariki Chadema, Mungu Ibariki Tanzania.
 
VIVA Chadema, tunawaunga mkono, huyu jamaa(Zitto) ni mwiba ndani ya chama makini, avuliwe na unaibu katibu mkuu...

Kwani tayari?? wao si wamekaa kikao na ''kupiga kura ya kutokuwa na imani nae...'' na tena wanasema eti watamfikishia ujumbe ili yeye ndo aamue. Wanamuogopa?

Akiamua kukataa kutoka?? hizi politics sijui zimekaaje.
 
Mbona watu humu ndani mmetokea kumchukia Zitto? Hamkumbuki yeye ndiye aliyefanya chadema ipendwe na vijana??

Mkuu umesahau msemo wa vijana EASY COME EASY GO. Kama alivyoweza kuvuta wapenzi kwa haraka kwa matendo yake ndivyo hivyo alivyo wapoteza wapenzi hao kwa matendo yake!

Lakini kumbuka hayo ni maoni yangu mkuu.
 
Kuna wengine apa mmoja wao mie nimeijua chadema cz of zitto,yani huniambii kitu!haya majungu yote wtvr yanaingilia uku yanatokea kule!yani am zittomaniac!

I value him loads cz kani inspire sana ktk huu ulimwengu wa kisiasa!naona wanamsakama sana!
We behind u Zitto,just keep it real!some of us are beliaving in you!
 
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamemweka kikaangoni Mbunge wa Kigoma Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho, Zitto Kabwe, katika kikao chao kilichokaa jana mjini Bagamoyo.

''Tumeamua kuwa hatuna imani na uongozi (Zitto),kimesema chanzo hicho. "Tumepitisha uamuzi wa pamoja. Ujumbe utamfikia, autafakari, kisha aamue mwenyewe...''

Huu ni ubabaishaji as usual......kama habari hii ni ya kweli.

Kama hawa watu wana uhakika na wanachokisema, walipaswa wa-analyse makosa ya Zitto kisha waamue kumfukuza/kumtoa kwenye hizo nafasi wanazosema hawana imani nae.
 
Napenda kujua hivi yule dada mbunge wa Chadema viti maalum kutoka Kigoma, Muhonga ni mke wa Zitto? Naona kila mahari na kila kona wako pamoja. Hivi Zitto yeye siyo Mkabila? Ninavyojua mimi yule dada kaingia siasa kwa sababu ya Zitto. Tukianza kuchambuana tutaona vingi vya ajabu.

Zitto tulia chapa kazi, Siasa ni kazi na kazi moja wapo ni kuwa smart kwa kila jambo. Usithubutu kunywa maji machafu kwa kupenda, lazima utahara na hutampata wa kumtwisha mzigo wako
 
Jamani naomba mnisaidie nyie mnaomfahamu fika zitto. Ni taasisi gani ambayo amewahi kuwa kwa kwa zaidi ya miezi sita ikabaki salama? Year round wanakuwa wanamanage crisis moja hadi nyingine na mitafaruku inayotokana na utovu wa nidhamu
 
Back
Top Bottom