Zitto arejea Nchini

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu

Heri ya Xmass na Hongereni kwa mapumziko kwa wale mlioko mapumzikoni,naamini tumepata muda mzuri wa kutafakari kwa kina mafanikio tuliyoyapata mwaka huu yawe ya binafsi ama ya taifa.

Muda mfupi uliopita nimeona kijana Zitto mitaa ya kati lakini sikupata bahati hata ya kumsalimia tu ingawa nilitamani kufanya hivyo.Nimefurahi sana kumuona Zitto kwakuwa nadhani na pia nashauri afanye mkutano na media ili aweze kujibu tuhuma zote tulizozisikia na kuzisoma kipindi ambacho hakuwa nchini.Ni vema tukamsikia nakumuona live kwenye luninga akijibu tuhuma hizo.
 
Kibunango.

Kwakuwa wewe ni kilaza ndo maana unajifanya hujui kama anatuhuma za kujibu.Ofcoz anazo.Mengi yalisemwa kipindi hayupo hivyo ni lazima ajibu ili mambo yanende hivyo.

Kibs sio kilaza bana ... katika hili nitamtetea .... ila zito itabidi ajibu tuhuma zote dhidi yake.
 
Only in Tanzania, kuwa mtu kama ana tuhuma then solution ni media!!!hiki kichekesho sana hiki.RA, EL, Chenge, Mkapa wakifika kwenye media hence justice done!

Kama Zito ana tuhuma lazima kuna watu amewakosea then hao watu inabidi wamchukulie hatua kali(kama tuhuma zipo) asipochukuliwa hatua then inabidi ujiulize inawezekana ulizosema tuhuma hazikuwa tuhuma bali facts!

Nitashangaa Zito naye akienda kwenye media eti anajibu tuhuma zipi? kamfanyia nani? akikaa kimya je?

Nchi hii itafika muda kila mtaa au kijiji una gazeti lake, achilia mbali matajiri!!
 
Atakuwa amecopy na ku paste tu !

Lol... wewe na Kibs hampikiki kabisa :)

Kibs mtaalam wa mambo mengi ya mazingira. Alishaelezea mengi sana katika hii nyanja, haswa ya waste management. Amediriki hata kuelezea jambo moja ambalo linahusiana na FLYING TOILETS kule Zenji!!

Btw, heading ya thread ilinifanya nije kusema: Mh. Zitto karejea nchini: SO?!!
 
Hakuna cha kujibu hapo. Unless kama watu wanataka kuuza magazeti. Kuna hoja zipi zaidi ya majungu? Hapo strategy ya BWM ndio sahihi.
 
Heshima mbele!!

Kama ni Kibunango ninaemjua mimi, ukweli ni kilaza kupita vilaza wote. Kwanza angalia eti "Mapinduzi daima". Walimpindua nani? Historia ya uhuru wetu haionyeshi tumepindua utawala wowote. Hivyo hayo mapinduzi yanatoka wapi?

Agenda kubwa hapa ni Mh. Zitto si kujibu tuhuma, ila kusafisha hali ya hewa kutokana na taarifa mbalimbali zilizotolewa juu yake na chama chake. Ni muhimu yeye angalau kutujuza maoni yake, hasa ukuzingatia kwamba ni "public Figure", hasa kwa vile anawakilisha watanzania kwenye taasisi yenye maslahi kwa watanzania.

Mh. Zitto kwa vile ni member humu ndani, tunajua atasoma maoni yetu na kwa busara zake tunaamini ata- "Set Climate".
 
Nd. Kibunango,
Tuhuma hana, isipokuwa wengine tungelipenda kujua tu kama ile barua bado anatembea tembea nayo mfukoni au kaiacha huko huko Ujerumani!
Mbona hakuna cha maana hapo? Kwani mtu anatumia muda gani kuandika barua hadi atembee nayo. It is a matter of second. Akiongelea haya basi na yeye kwishneii. Nashauri angekwenda kwa wapiga kura wake akawaeleze anavyotekeleza aliyowaahidi.
 
Mbona hakuna cha maana hapo? Kwani mtu anatumia muda gani kuandika barua hadi atembee nayo. It is a matter of second. Akiongelea haya basi na yeye kwishneii. Nashauri angekwenda kwa wapiga kura wake akawaeleze anavyotekeleza aliyowaahidi.

Mtu kama Zitto atatumia miezi miwili kuandika hii barua.
 
Kibunango.

Kwakuwa wewe ni kilaza ndo maana unajifanya hujui kama anatuhuma za kujibu.Ofcoz anazo.Mengi yalisemwa kipindi hayupo hivyo ni lazima ajibu ili mambo yanende hivyo.

Zijaona kama Zitto ana tuhuma za kujibu....anajibu nini sasa na kwa manufaa ya nani??anataka kutupotezea timing to ya mambo yetu ya hepi nyu iya huku LAMU
 
Kama Zitto karudi na kama kweli ni mwanaJF mimi kama mimi nampa ushauri ufuatao, asije akaitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia tuhuma kama zipo ama yaliyokuwa yakisemwa na watu wakati yeye hayupo, atazua maswali mengi kuliko majibu. Ajue kwamba wabaya wake na wabaya wa Chadema wanatumia mbinu mbalimbali ikiwa pamoja na kuzusha kitu ili alazimike kujibu na atakapojibu tu hatajua ni wapi na lini aliingia mtegoni. Akumbuke alivyoingia mtego wa Dowans.
Kwamfano, ukiambiwa mahakamani " unatuhumiwa kuwa ulihusika kumuua marehemu" ukijibu "mimi sikumuua" utaulizwa sasa basi tuambie aliyemuua kama sio wewe, hapo utalazimika kuongea kiswahili kireefuu mwisho utajikuta umejichanganya. Yeye Zitto aendelee tu na mikutano ya kawaida, kwenye mikutano hiyo watu wataanza kuulizana kama kweli aliandika barua ya kujiuzuru mbona anamwaga sera tu na operation sangara mwendo mdundo?,watakuwa wamejijibu wenyewe. Ni logic ndogo sana.
 
wakuu

heri ya xmass na hongereni kwa mapumziko kwa wale mlioko mapumzikoni,naamini tumepata muda mzuri wa kutafakari kwa kina mafanikio tuliyoyapata mwaka huu yawe ya binafsi ama ya taifa.

Muda mfupi uliopita nimeona kijana zitto mitaa ya kati lakini sikupata bahati hata ya kumsalimia tu ingawa nilitamani kufanya hivyo.nimefurahi sana kumuona zitto kwakuwa nadhani na pia nashauri afanye mkutano na media ili aweze kujibu tuhuma zote tulizozisikia na kuzisoma kipindi ambacho hakuwa nchini.ni vema tukamsikia nakumuona live kwenye luninga akijibu tuhuma hizo.

sooooo what?????

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom