Zitto apewa mpini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto apewa mpini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Dec 14, 2010.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupima mwenyewe kama aendelee na wadhifa wake wa naibu kiongozi wa upinzani bungeni baada ya wabunge wa chama hicho kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.Pia, mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda ameundiwa tume ambayo itamchunguza mwenendo wake ikiwa ni baadhi ya mikakati ya chama hicho kujiweka sawa dhidi ya mtikisiko uliotokea baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

  Zitto, ambaye alijijengea umaarufu mkubwa katika Bunge la Tisa, aliingia matatizoni baada ya kupinga hadharani msimamo wa wabunge wa Chadema kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kutoa hotuba ya uzinduzi wa Bunge la Kumi.

  Zitto, ambaye hakuingia kwenye ukumbi wa Bunge kutekeleza uamuzi wa wenzake wa kumsusia Rais Kikwete, aliitisha mkutano na waandishi wa habari baada ya kitendo hicho cha kihistoria na kusema kuwa hawakupaswa kutoka kwenye ukumbi huo na kuweka hadharani jinsi uamuzi huo ulivyofikiwa ndani ya vikao vya wabunge wa Chadema.
  Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama chake hakiwezi kuwaachia viongozi wake kufanya mambo yaliyo kinyume na misimamo ya chama na hivyo kimempa fursa Zitto apime mwenyewe kama anaweza kuendelea kuogoza watu wasiokuwa na imani naye.
  Alikuwa akizungumzia mambo yaliyojiri katika kikao cha wabunge kilichofanyika kwa muda wa siku mbili mjini Bagamoyo wiki iliyopita na kufikia uamuzi huo wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani mbunge huyo katika nafasi yake ya unaibu kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Dk Slaa alisema maamuzi ya wabunge ya kutokuwa na imani naye kwa nafasi ya unaibu kiongozi bungeni yalifikishwa kwenye kamati kuu ya Chadema iliyoketi Desemba 11 mwaka huu.
  “Kamati kuu haikukutana kujadili suala za Zitto sababu chama hakina mamlaka ya kuingilia kazi ya kamati ya wabunge, bali kilipokea taarifa ya uamuzi wa wabunge hao,” alisema Dk Slaa.
  Alisema kutokana na chama kutokuwa na uwezo wa kutoa uamuzi dhidi ya msimamo huo wa kamati ya wabunge, ni jukumu la Zitto mwenyewe kupima suala hilo na kuchukua uamuzi wa kujiuzulu au kuendelea na wadhifa wake.

  Akizunguzia suala lililozua mjadala la uchaguzi mkuu, Dk Slaa alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais kujadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete yalichezewa.
  Alisema kutokana na sababu hizo, Chadema imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

  “Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa,” alisema Dk Slaa.
  “Kisheria Tanzania ina rais na sisi Chadema tunasema nchi hii ina rais, lakini njia iliyutumika kumpata rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa Chadema kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge,” alisema Dk Slaa.
  "Unajua hapa suala la kutambua au kutokumtambua rais siyo issue. Rais yupo na katiba inaelekeza kwamba rais akishachaguliwa huwezi kuhoji mahali popote na kwa maana hiyo rais yupo. Tatizo ni jinsi alivyopatikana."
  Naye mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo alisema kamati kuu iliunda tume inayoongozwa na Profesa Mwesiga Baregu na kutaja kazi zake mojawapo ikiwa ni kumpa ushauri Zitto na pili kumchunguza mbunge wa Jimbo la Maswa, John Shibuda.

  Shibuda, ambaye alitokea CCM baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni, aliripotiwa na vyombo vya habari kuwa alikorofishana na mbunge mwenzake wa chama hicho, Ezekiel Wenje wa Jimbo la Nyamagana kiasi cha kufikia kutupiana maneno makali.
  Vyombo hivyo vilidai kuwa Shibuda aliahidi kumshtaki Wenje kwa wazee wa chama hicho kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  “Kamati kuu ya imeunda tume itakayaofanya kazi mbili; ya kwanza itakuwa kukutana na Zitto na kumshauri na kazi ya pili ni kumchunguzi mbunge wa Maswa John Shibuda,” alisema Tumbo.

  Kamati kuu, iliyokutana kwa siku moja jijini Dar es Salaam na pia kujadili suala la uchaguzi mkuu na mwenendo wa wanachama wake, imeeleza kuwa uamuzi wa kumchunguza Shibuda unatokana na mbunge huyo kuonekana kutokuwa na madili ndani ya chama.

  “Kamati itamchunguza Shibuda na kutoa taarifa kwa chama na hii imetokana na mwenendo wake kubadilika na amekuwa akikiuka maadili ya chama,” alisema Tumbo.
  Alisema Chadema ina maadili yake ambayo kila mwanachama na kiongozi anastahili kuyafuata na kwamba kitendo cha mbunge huyo kukiuka maadili hayo ikiwa ni pamoja na kuzungumza mambo ya chama kwenye vyombo vya habari bila utaratibu.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Chadema watafanya kila njia wa Isla wang'oke. Ikiwa watazidi kuwepo, dhana yao ya "wapiganaji" haitotimia, wapiganaji wa nini? kuna vita Tanzania? kwa nini hamsemi kweli tu? wapiganaji wa kusimika misalaba, Crusaders.
   
 3. Double X

  Double X Senior Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona huyu Zito anacheleweshwa, we want to move foward.hiki ni kirusi na nilazima tukiondoe tu, hata kama akionywa huyu ni mr misifa na kimbelembele, anyang'anywe na ukatibu mkuu msaidizi awe mwanachama wa kawaida tu kama mr sugu,akileta za kuleta achomolewe kabisa na uanachama aende akawe dereva wa RA.
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  heeee we wa wapi?una washwa nini?????
   
 5. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hao CHADEMA inaelekea wamesahau jinsi vyama vinavyokufa. Marando wako nae humo ndani, wakumbushane tu kuwa NCCR ilikuwaje 1995 na ikoje sasa? Buriani CHADEMA.
   
 6. P

  Patchu New Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na kumsamehe mh. zito bado wamuwekee muda wa kumchunguza huyu dogo ni hatari sana kwa chama ni ndumila kuwili sana huyu .
   
 7. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kelele za nini? Zito keshasema hakugombea nafasi ya unaibu kiongozi kambi ya upinzani. Wala haoni sababu ya kuiachia nafasi hiyo. Amwachie nani? Amwachie nyani shamba la mihogo?. Halafu hao wabunge waliopiga kura kutokuwa na imani naye ndio waliompa hicho cheo? Je, wanayo jeuri ya kumvua nafasi hiyo?
  Nafasi ya unaibu ipo kulingana na sheria na taratibu za bunge na sio matakwa ya chama au kikundi fulani. Hivyo hakuna ulazima wa kujiuzulu. Zito ni mwelewa na hawezi kuchukua uamuzi wa kijinga. Yupo kwa maslahi ya wananchi zaidi. Ana dhima kwa watanzania zaidi kuliko chama. Hana cha kupoteza katika siasa. Anafaa kuongoza.
   
 8. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Dar es salaam INRI kama hujaelewa omba uelimishwe maana mara nyingi unakuja na mambo ya dini humu hatu batizi wala hatusilimishi tuna elimishana tu udini tuacha naomba kuwasilisha
   
 9. P

  Pamba Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema unajua ndio mwisho wenu,
  Zitto yuko juu kuliko mnavyofikili sisi huku tunamuunga mkono ni bora aende NSSR kuliko chama cha wachagga wabaguzi sana,au mnataka kumfanaya kama chacha wangwe?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma!
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma! Kama post yangu umeisoma vizuri utaelewa nilichoandika. Kinaelimisha kwa mwenye kutaka kuelimika.

  Unaweza kunambia maana ya "wapiganaji" na nchi yetu shwari haina vita?
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  si umeuliza swali hapo juu mbona hujibu au unawashwa kweli?
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Vipi, inauma?
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  we haikuumizagi???
   
 15. M

  Major JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiyo unataka kufa na wala siyo CHADEMA, kumbuka ili mahindi yajae sawasawa ktk ndoo au debe ni lazima yatingishwe, other way itakuwa kanyaboya, kwa hiyo chama makini ni lazima wajitingishe
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  NSSR ni chama cha wapi?
  sio lazima kuchangia mada kama hujui unachokiandika.
  Na kama huna cha kuandika basi kachukue kopo ukachambe.
   
 17. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe kuna watu hawajui tanzania tuna na tuko vitani?ndg zangu tuna vita kubwa kuliko ile ya sadam,kwa uchache,UMASKINI,UFISADI,MARADHI,mengne ongeza mwenyewe,hivi vita vinahitaji makamanda wa kweli tuwape moyo
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Zitto atajitoa mwenyewe chadema haitaki kutumia nguvu kwa ajili ya hili
   
 19. D

  DENYO JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dar es slaam hawezi kuelewa kwamba tanzania si shwari na kwakuwa katumwa ndio maana utamsikia mara nyingi hoja zake ni za ubaguzi. Hawa ndio wakisemwa kwa maovu yao wanakimbilia huruma ya udini na ukabila. Hawafai watu hawa. Chadema ipo na inawakilisha umma. Tutaijadili chadema siku zote katika jukwaa hili kwa kuwa ndio chama cha upinzani kilichobaki wengine wasindikizaji. Tunamtakia safari njema zitto zuberi kabwe home boy aende atakako kwenda hatutaki mapopo chadema hatutaki mandumila kuwili. Period!
   
 20. minda

  minda JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  cdm si bure; kuna mkono wa mtu.
   
Loading...