Zitto apewa majukumu ya Kimataifa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mwanachama mwenzetu na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ameombwa kushiriki katika panel ya wabunge wa Kimataifa duniani. Tafadhali soma barua ya uteuzi wake na nyaraka ya majukumu yake hayo. Kuteuliwa kwake kujiunga na panel hiyo ni heshima kubwa kwake kama Mbunge kijana lakini pia ni ishara ya jinsi nyota yake njema inavyozidi kuangaza. Hongera na kazi njema.
 
Attachments

  • PN_Event_Invite_23JUL08_(ZITTO).pdf
    161.7 KB · Views: 207
  • TF_PN_Proposal_(13June2008).pdf
    124.1 KB · Views: 99
Hongera Zitto...hii inaonyesha kuwa kuwatumia Wananchi kunalipa, tena malipo haya ni yale yanayoacha LEGACY hata kwa vizazi vijavyo. Nakutakia mafanikio zaidi na zaidi kwenye majukumu yako mapya, unastahili kabisa na nina imani utapeperusha bendera yetu vema.
 
Hongrea Zitto.

Ila suala la Address,hiyo siyo address ya Bunge

Hon. Kabwe Zitto​
[FONT=Garamond,Garamond], [/FONT]MP
Parliament of Tanzania
P.O. Box 325
Kigoma
[FONT=Garamond,Garamond],
[/FONT]
Tanzania
 
Mwanachama mwenzetu na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ameombwa kushiriki katika panel ya wabunge wa Kimataifa duniani. Tafadhali soma barua ya uteuzi wake na nyaraka ya majukumu yake hayo. Kuteuliwa kwake kujiunga na panel hiyo ni heshima kubwa kwake kama Mbunge kijana lakini pia ni ishara ya jinsi nyota yake njema inavyozidi kuangaza. Hongera na kazi njema.

Big Up Zitto
Ukaturepresent vizuri
 
Date::7/28/2008
Zitto ateuliwa Mtandao wa Wabunge Duniani
Na Tausi Mbowe
Mwananchi

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, ameteuliwa kuungana na Mtandao wa Wabunge Duniani, wanaoshiriki kuzuia na kulinda usalama wa wananchi.

Zitto anaingia katika mtandao huo wa wabunge wa kimataifa utakaokuwa hauko katika mfumo wa kichama na utakuwa ukijengwa na wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani ambao unafanya kazi kwa pamoja kitaifa na kimataifa.

Mtandao huo unaundwa chini ya Taasisi ya Mashariki na Magharibi ya Mtandao wa Wabunge (EWI), yenye makao yake makuu Brussels, Ubelgiji.

Wabunge hao watatarajia kuwa na mkutano Oktoba 8 mwaka huu, kwenye Bunge la Ulaya jijini Brussels, Ubelgiji.

Zitto ambaye ni mbunge kijana zaidi Tanzania anayewakilisha jimbo, alipata mwaliko kuhudhuria mikutano ya wabunge hao, ikiwa ni hatua ya kumkaribisha kufanya kazi katika mtandao huo.

Moja ya majukumu ya mtandao huo ni kujihusisha na utafutaji wa ufumbuzi wa migogoro na kusaidia katika vita dhidi ya usalama wa kibinadamu ili kuhakisha malengo ya millenia (MGDs) yanafikiwa.

Kwa miaka 28 sasa EWI imekuwa ikitumia njia ya utandawazi katika kufikiri na kutenda ili kusukuma na kuhakikisha dunia inakuwa sehemu salama.

Taasisi hiyo pia ina jukumu la kuhakikisha inaweka utetezi madhubuti kwa nia ya kuchechea mabadiliko; tayari imeanzisha programu yake ya mpango kazi wa kimataifa ili kutetea demokrasia kama kielelezo katika mapambano dhidi ya migogoro.
 
Hongrea Zitto.

Ila suala la Address,hiyo siyo address ya Bunge

Hon. Kabwe Zitto​
[FONT=Garamond,Garamond], [/FONT]MP
Parliament of Tanzania
P.O. Box 325
Kigoma
[FONT=Garamond,Garamond],
[/FONT]
Tanzania

Mkuu kila mbunge ndani ya Bunge anatambuliwa Rasmi na anuani yake ya Jimbo ama kama ni wa viti maalum anatambulika kwa address yake ya Halimashauri ambayo anaiwasilisha.

hIVYO NAAMINI KUWA WAMETUMIA ADDRESS SAHIHI MKUU ,Kwani ya Bunge itakuwa kama inaenda kwa katibu wa Bunge as a taaisisi mkuu.

Hongera Zitto ,naamini wapo wengi watakaokuwa tayari kukusaidia kwenye majukumu yako.
 
Mkuu umepoetea sana Mjini...mpaka 29th utakuwa huko?
 
Mheshimiwa Zitto,

kwanza hongera sana kwa kuteuliwa kwako. Hii ni dalili kwamba kazi zako kama mbunge zinathaminiwa na watu wengi hata nje ya nchi yetu.

Ila tu mimi pia nina ushauri, pamoja na kushiriki kwenye tume mbalimbali, weka juhudi zako kubwa kwenye kuendeleza jimbo lako la Kigoma. Mafanikio yako kama mbunge yatakuwa judged na juhudi zako za kuwakomboa wana jimbo lako kuliko kitu kingine chochote.

Ukianza kushiriki hizi tume na kamati mbalimbali ni rahisi mno kujisahau na kukuta jimbo linabaki pale pale.

Mafanikio mema katika shughuli zako.
 
Mtanzania ungemuuliza anafanya jitihada gani za kuendeleza Jimbo lake na hadi hivi sasa amefanya nini JImboni kwake ili angalau ushauri wako uwe na uzito wake. Kwa sababu ulivyoandika ni kana kwamba hafanyi mambo ya kuendeleza jimbo lake.
 
Wapi? Tatizo wengine mnaandika kama mnanijua vile, hilo ndio tatizo.....Mpaka kieleweke is YOU.
Ndugu,

if it is you so what is the matter with you if i know you from who you are?Ans i will let you know this when the times comes..nitakapochukua Kadi ya CHADEMA?
 
Mtanzania ungemuuliza anafanya jitihada gani za kuendeleza Jimbo lake na hadi hivi sasa amefanya nini JImboni kwake ili angalau ushauri wako uwe na uzito wake. Kwa sababu ulivyoandika ni kana kwamba hafanyi mambo ya kuendeleza jimbo lake.

Mzee Mwanakijiji,

Nafikiri hayo maelezo yangu yanajitosheleza, hakuna niliposema hafanyi mambo ya kuendeleza jimbo lake. Nimetoa ushauri tu wa jumla ingawaje pia sio lazima mtu aufuate.

Kwa uzoefu wangu majukumu mengi yanaongozana na kushindwa kushughulikia mambo mengine. Kama hilo sio tatizo kwa mheshimiwa Zitto, well ni jambo jema na mungu amsaidie zaidi.
 
Nimekupata, nilidhani ulikuwa unaimply kwamba Jimbo lake linazidi kuachwa nyuma kwa sababu Zitto anajishughulisha na mijumuiko kama hii. Lakini ushauri wako ni mzuri sana kwa kadiri ya kwamba Zitto asije akajisahau.
 
Hongera sana Zitto...naamini utatuwakilisha vizuri sana ....kabla hujaachana na siasa na kwenda kufundisha...
 
Hongera mheshimiwa Zitto.

Fahamu kuwa hapa JF na nje ya JF una "support" kubwa kwa hio usisahau hilo.
 
Back
Top Bottom