Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Habari nilizopata hivi punde, Waziri wa nishati na madini Wiliam Geleja amesema serikali haitataifisha mitambo ya DOWANS, AMEDAI SERIKALI INA MIPANGO THABITI YAKUTATUA TATIZO LA UMEME NCHINI.


Kama ni kweli, Mbona anaongelea UVUNGUNI?
 
Hiyo ndiyo akili ya waziri wetu...zezeta au ziro...anasubiri nini "Kujiuzulu" mikakati mpaka lini??? waziri wizara imekushinda just go go.....
 
Keli demokrasia imekuwa doh, sikutegemea kama Zitto anaweza kuja kupingwa namna hii kutokana na umahiri wake wa kutetea taifa na kutokana na uaminifu aliojijengea miongoni mwa wananchi, haya Zitto Kabwe naamini unaingia humu ndani kazi kwako kupima maoni ya wanajamvi.
 
Hiyo ndiyo akili ya waziri wetu...zezeta au ziro...anasubiri nini "Kujiuzulu" mikakati mpaka lini??? waziri wizara imekushinda just go go.....
Tanzania siku hizi hakuna cha kujiuzulu. Mwulize waziri wetu wa ulinzi!
 
Mhe, Zitto Kabwe (MB) atakuwa na Press Conference kesho Oktoba 15, mida ya saa 6 adhuhuri Cortyard Hotel - Dar es Salaam.

Press Conference hii itahusiana na Mgawo wa Umeme unaoendelea. Kwa waandishi mlio Dar tunatarajia mtatufahamisha kinachoendelea. Kama kawaida, JF itatuma mwakilishi wake kutufahamisha kilichojiri.

Stay tuned


Update 1: Hiki ndicho alichoongea:


TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA, NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KUHUSU MGAWO WA UMEME NCHINI.

COURTYARD HOTEL, DAR ES SALAAM
OKTOBA 15, 2009.


UTANGULIZI




Kwanza niwashukuru ndugu zangu wana habari kwa kukubali kuja kunisikiliza, hatua ambayo kwangu ni fursa ya kuzungumza na umma wa Watanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa letu lipo kwenye matatizo mengi, na kwakweli linapita kwenye kipindi kigumu sana kisiasa, kiuchumi na hivyo kijamii. Najua tunakabiliwa na matatizo mengi sana kama Taifa, kiasi kwamba ni vigumu kama kiongozi kuchangia mawazo kuhusu ufumbuzi wa matatizo yote yanayotukabili.

Ni kwa msingi huo, leo nimeona nizungumze nanyi kuhusu hali tete ya mgawo wa umeme unaolikabili Taifa kwa sasa. Mwanzoni mwa mgawo huu sikupenda kusema chochote pamoja na kuulizwa sana na waandishi wa habari na wadau mbalimbali. Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhu. Pia kumekuwa na shutma mbalimbali, mojawapo ikidai kuwa baadhi ya watendaji wa TANESCO wanajaribu kuthibitisha madai yao ya kitaalumu ya kununua mitambo ya DOWANS. Shutma kama hizi, ni dhahiri zinauelewa finyu juu ya vyanzo vya mgao wa umeme uliopo sasa, ambao unasababishwa na uhaba wa mashine na upungufu wa maji. Uelewa huu finyu si tu hauna manufaa, bali hautoi ufumbuzi juu ya tatizo lililopo sasa ili kuepuka madhara ya kiuchumi kwa taifa na wananchi wake.

Kwa maendeleo yote duniani, nishati ya umeme ni msingi mmojawapo wa kujenga uchumi. Kwa utambuzi huu nchi mbalimbali duniani, hata zile zinazoweza kutoa huduma ya umeme kwa asilimia 90 kukidhi mahitaji yake, zinajaribu kuimarisha sekta zao za nishati kama msingi wa ujenzi wa maendeleo kwenye viwanda na wananchi wake. Nchi yetu ya Tanzania, huduma ya umeme inauwezo wa kuhudumia asilimia 12 tu na bado kunamgao.

Ni kweli changamoto za kuendeleze sekta ya umeme ni kubwa sana, na mipango ya muda mrefu ipo ingawaji haitekelezwi kwa sababu mbalimbali, lakini si lengo la mazungumzo yangu ya leo. Kwa mazingira tuliyonayo sasa, hasa katika kufuatia kuporomoka kwa uchumi duniani, hatua za haraka hazinabudi kuchukuliwa kuliepusha taifa katika uporomokaji wa uchumi wa kitaifa unauweza kuzuilika. Huu ni wakati ambapo serikali inapaswa kufanya tathimini ya haraka ili kufikia muafaka wa taratibu zipi zichukuliwe kuepuka hasara zitakazoletwa na mgao wa umeme, na hivyo maongezi yeyote yajikite kutafuta suluhu ya kuondoa mgao wa umeme kwa haraka zaidi. Badala ya hali ya sasa ambayo mijadala na hatua mbalimbali zimejikita kutafuta chanzo cha tatizo bila kutoa suluhisho, huku madhara ya mgao yakiendelea kuwaumiza watanzania.

Tumeambiwa na TANESCO kuwa Mgawo wa umeme wa masaa 14 kila siku msingi wake ni upungufu wa 90MW za umeme. Kwa mgawo huu TANESCO wanapoteza mapato ya takribani shilingi 200 milioni kwa siku! Lakini hii ni kwa upande wa TANESCO tu, bado kunamadhara mengi kwa upande wa wananchi na taifa kwa ujumla.

MADHARA YA MGAWO WA UMEME KWA UCHUMI WA TAIFA.

Ndugu zangu, mgawo huu una madhara makubwa sana, kuanzia kwenye uchumi mkubwa wa taifa (macro economy) hadi uchumi mdogo wa makampuni na mtu mmoja mmoja. Madhara ya mgawo wa umeme yana athiri mpaka wasio na umeme;

  • Katika sekta ya Ujenzi, mfano wa viwanda vya Simenti gharama za uzalishaji zimeongezeka sana. Kwa mfano Kampuni ya Twiga Cement hutumia dola za Marekani 10 kama gharama ya kuzalisha umeme iwapo wanatumia umeme wa TANESCO. Gharama hizi huongezeka mara 4 na kufikia dola 40 kwa Tani wakati wa mgawo. Hii maana yake ni kwamba bei ya Saruji itapanda kwa shilingi 1000 zaidi kwa kila mfuko wa Saruji. Watakaoumia hapa ni raia wa kawaida wanaojiwekea akiba ili kujenga nyumba zao.
  • Nimeambiwa sekta ya Mabenki inaathirika sana na mgawo wa umeme kwani gharama za kuwasha umeme katika matawi yao imeongezeka sana. Mfano, Benki ya CRDB sasa itatumia shilingi 400 kwa mwezi kwa gharama za umeme na Benki ya Barclays itatumia zaidi ya shilingi 210 milioni kwa mwezi. Zote hizi zinaongeza gharama za biashara na hivyo kupunguza kodi ya serikali.
  • Katika sekta ya Mawasiliano gharama za kuendesha minara ya simu zimeongezeka kutokana na kampuni za kugharamia mafuta ya kuwasha minara. Takwimu zinaonesha kuwa Kampuni ya Simu ya Zain sasa inatumia shilingi 700 milioni zaidi kwa mwezi kwa sababu ya mgawo. Kampuni ya Vodacom inatumia zaidi ya shilingi 800 milioni zaidi kwa ajili ya kuwasha minara yao. Hii maana yake ni kwamba gharama hizi zitapunguza kodi za makampuni ambazo kampuni zitalipa serikalini. Zaidi ya hapo mgawo husababisha matatizo ya mawasiliano kwa watu kushindwa kutumia simu zao kutokanana ukosefu wa umeme.
  • Madhara ya mgawo wa umeme yanamuathiri kila Mtanzania, Mkulima kwa mfanyakazi, wafanyabiashara wakubwa kwa wafanyabiashara wadogo. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu, Kamati yangu ya Mashirika ya Umma tulifanya utafiti mdogo kuangalia madhara ya mgawo wa umeme kwa watu wa kawaida, tulikuta salooni moja wakatwambia wanatumia 8000/= pakiwa hakuna mgawo lakini pakiwa na mgawo wa umeme wanatumia hadi 68000 kwa ajili ya umeme wa jenereta, sawa na gharama ya ziada ya shilingi 60,000/= kwa siku. Hivyo mgawo unawaumiza sana wajasiriamali wadogo wadogo na kuharibu mitaji yao na hivyo kuongeza umasikini.
  • Hivi juzi nilikuwa nazungumza na watu wenye mashine za kusaga nafaka huko Nzega naambiwa , pakiwa hakuna umeme wanatumia mafuta ya diesel na gharama za uendeshaji ni mara tatu ya gharama wanazotumia umeme ukiwepo. Hii maana yake ni kuwa madhara ya mgawo yanamgusa mwananchi wa kawaida kabisa vijijini kwa kuongeza bei za vyakula na hivyo kuongeza mfumuko wa Bei.
  • Nimekwenda Internet café moja hapa Dar es salaam, wanasema bei ya huduma ya internet kwa saa siku za mgawo wa umeme ni shilingi 2000 wakati siku umeme ukiwepo ni sh1000. Hii ni mifano ya maeneo machache tu kuhusu mgawo, ambayo kwa ujumla inaonesha wazi kuwa mgawo wa umeme unapandisha gharama za maisha (cost of living) wakati mapato ya mtanzania yakiwa duni.
Serikali na Taifa linapoteza mabilioni ya fedha kutokana na mgawo huu wa umeme. Naamini baadae Benki kuu itakuja kufafanua hili. Lakini Taifa linapokuwa kwenye mgawo uchumi wa unayumba. Nimewaambia kwamba mgawo wa 2006 peke yakeuliporosha uchumi kwa nukta moja ambayo ni sawa na shilingi billion 250. Na sasa ninawaambia, tukiacha mgawo huu uendelee hata kwa miezi miwili, taifa litatetereka vibaya sana.

  • Mfumuko wa bei utazidi kupanda(cost push inflation),
  • Uwiano wa malipo ya nje utaathirika kwasababu ya kutumia pesa nyingi za kigeni kununua mafuta nje(import),
  • Gharama za uzalishaji viwandani zitapanda sana na kusababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha ambayo ingekusanya kama kodi.
Inaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.

3. HATUA NINAZOPENDEKEZA
Nimesema mwanzo kwamba, kuendelea kwa mgawo huu wa umeme ni udhaifu wetu wa uongozi kushindwa kufanya maamuzi magumu lakini ya msingi, na badala yake kujikita katika kutafuta nani mchawi kila tunapokabiliwa na tatizo. Ni bahati mbaya sana hata vyombo vya habari vimejikuta vikiendelea kutoa taarifa za mchawi anatafutwaje badala ya kueleza madhara ya mgawo kama njia ya kushinikiza ufumbuzi wa tatizo.

Wakati Taifa linakabiliwa na upungufu wa 90MW za umeme, na uchumi wa kila mtanzania unaathirika, hapa nchini tuna mitambo ya IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW, ambayo imezimwa kwa sababu ‘eti’ ina kesi dhidi ya serikali. Majadiliano kuhusu mgogoro huu bado yanaendelea bila kwisha. Hapa nchini tuna mitambo ya Dowans yenye uwezo wa kuzalisha 125MW, ambayo ni ya kuwasha tu. Lakini kwasababu tu serikali imeshindwa kufikia maamuzi, inaendelea kuwepo nchini huku Taifa linayumba kwa giza.

Kama nilivyoeleza hapo awali, nishati ya umeme ni kichocheo kikubwa sana cha ukuaji wa uchumi na hatimae maendeleo ya kiuchumi. Kwahiyo kama kiongozi sikubaliani kabisa kuona nchi inaendelea kuwa gizani na kugharimu uchumi wa Taifa, kuongeza gharama za maisha ya mwananchi wa kawaida na hata kupunguza mapato ya serikali.

Ninapendekeza;

  • Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
  • Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.
4. HITIMISHO

Mgawo huu wa takribani mwezi sasa umeshaligharimu Taifa kwa kiasi kikubwa sana. Mgawo huu ukiendelea kwa wiki tatu zijazo, madhara yake ni makubwa kiasi cha hata maamuzi ya serikali kuhami uchumi (stimulus Package) yaliyotajwa na Rais Kikwete mjini Dodoma mwezi Juni yatakuwa hayana maana kabisa kwani mfumuko wa bei na kudorora kwa shughuli za uchumi kutaporomosha ukuaji wa uchumi uliotarajiwa na mkakati huo.

Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.

Asante sana.

KABWE ZUBERI ZITTO,MB
Dar es Salaam.

Huyu mbunge ana data za kushangaza katika makampuni makubwa aliyoonyesha yatapata hasara kubwa ni Twiga cement.Twiga cement mitambo yake inatrgemea zaidi gesi si umeme wa Tanesco katika uzalishaji wake hizo data za kusema hasara inakuja kwao kubwa mchumi koko wa Dowans? Ambaye hajui kuwa kiwanda kile kinategemea gesi zaidi ambayo ni bei rahisi kuliko umeme wa Tanesco.Hizo projections zake za kupanda bei NI ndoto za Alinacha DOWANS

Mkampuni mengine aliyopata data alizomwaga NA KUONGEA KWA UCHUNGU KOKO ni CRDB ambako mamilioni ya KIBAKA RICHMOND YALIPITIA,ametaja pia Baclays Bank ambako Mkopo wa KULIPIA mitambo umeme KIBAKA fisadi ulitoka,pia Kataja VODACOM ambako kuna ,anayetuhumiwa kuhusika DOWANS na Richmond.Zitto anawapigia debe kuwa hao wanapata hasara kubwa mno....inaumiza sana blablablabla.

Yaani anaita press confrence ili aongelee data za hao jamaa bado wako moyoni mwake wamempa nini na ana agenda gani nao?

UKISOMA TU UNAJUA ANAWALILIA DOWANS,IPTL,BACLAYS,CRDB na VODACOM ambao sababu ya kuwalilia anaijua vizuri sana yeye hao wengine aliowachomekea ni tu ili uwongo unoge zaidi akidhani watu wataungana naye na kuendelea kulia naye kuwalilia.Hasira za wananchi hazijapoa juu ya hao anaowalilia kweli Zito ni mzito kuelewa na kusoma nyakati na wananchi wanataka nini na kipi hawataki.
 
Watanzania na Wana JF,nafikiri sio jambo jema kabisa kumkashifu Zito Kabwe,kama kiongozi amejaribu kutoa mtazamo wa nini kifanyike,kitu ambacho si cha hekima mpaka sasa ni kuona viongozi wahusika wa suala zima la umeme kutofanya kazi yao kikamilifu,wamekaa kimya bila kusema chochote,na wanaojaribu kusema wanatuletea majibu ya siasa,ni aibu kwa kweli.Hongera Zito kwa kuonyesha njia.Kiongozi mzuri siku zote anatetea anachokiamini hata kama atapingwa na Ulimwengu mzima.
 
Jamani Zitto kakamatwa kwa uwongo eti Twiga cement inakula hasara na mifuko ya cement itapanda kwa ajiri ya umeme,lakini ukweli ni kwamba Twiga cement wanategemea Gas ya Songos kuzalisha na sio umeme wa Tanesco....Zitto kumbuka hapa huongei na peasants walioishia darasa la tatu!
 
Muda wote alikuwa kimya leo baada ya Zitto ameamua kuongea, hawa ndiyo viongozi wetu hawa.

Halafu anaongea pumba. Zaidi ya wiki yeye na boss wake Kikwete wako kimya wakati Watanzania wanateseka na mgao wa umeme!
 
Kama ni kweli, Mbona anaongelea UVUNGUNI?

Mkuu hii kitu ni ya kweli haikuwa press column ilikuwa inasomwa kwenye tv, na jamaa akanichapa na message, ni mtu makini sana...ilikuwa ni Channel 10 leo majira ya saa moja afrika mashariki, labda ujaribu kuuliza walio angalia lakini kwa kifupi ndiyo hivyo...vipi nadhani sasa niko juu ya kiti mkuu.

MJ
 
Jamani Zitto kakamatwa kwa uwongo eti Twiga cement inakula hasara na mifuko ya cement itapanda kwa ajiri ya umeme,lakini ukweli ni kwamba Twiga cement wanategemea Gas ya Songos kuzalisha na sio umeme wa Tanesco....Zitto kumbuka hapa huongei na peasants walioishia darasa la tatu!

Hapo zamani nilishawahi kusema kwamba aidha Zitto anaongea bila utafiti au wanaomfanyia utafiti wanampa mautumbotumbo yalioyojaa mavinyesinyesi ya uharoharo.

Angekuwa makini hasingeleta habari za kutaifisha DOWANs wala habari za kushauri IPTL intengeneze umeme wakati serikali ina matatizo nayo. Naona Zitto anawapa cha kusema wale wazee waliobaka democracy. Zitto, kuwa makini na lugha zako katika mashirika ambayo yanakesi na serikali, pia hizi lugha zako za kutaifisha makampuni yanapeleka dhana mbaya kwa wawekezaji, at best itakifanya chadema kuwa chama kinacholenga kuturudisha, at a full speed, kwenye azimio la Arusha na siasa za ujamaa na kujitegemea.
 
Sijui kama ni ushabiki au ni kitu gani,ni kwanini tuseme kwamba Zito ameshikwa kwa uongo,ninavyofahamu katika hali ya kawaida huwezi kuongelea madhara ya Uchumi wa jumla(Macroeconomy) bila kugusia sekta za Mawasiliano kama ilivyo kwa Vodacom,sekta za kibenki kama ilivyo kwa CRDB na Backlays na sekta ya viwanda kama Twiga cement.Kwamba tunamashaka ya mahusiano kati ya Richmond na Makampuni yaliyotolewa mfano wa kuathirika kiuchumi haina maintiki yeyote kwa kuwa hiyo ilikuwa ni mifano tu.

Jambo jingine ni kwamba,ukisoma vizuri taarifa ya Zito kuhusu kuathirika kwa kampuni ya Twiga cement kutokana na ukososefu wa umeme,anasema kwamba;namnukuu,..." Kwa mfano Kampuni ya Twiga Cement hutumia dola za Marekani 10 kama gharama ya kuzalisha umeme iwapo wanatumia umeme wa TANESCO."...kwangu mimi neno iwapo ni kama altenative,maana yake zipo njia zingine Twiga cement wanatumia badala ya umeme wa tanesco kama gesi ya Songos.Kwa ufupi naomba tumtendee haki kijana mwenzetu Zito badala ya kumkatisha tamaa.
 
Anachotaka Zitto:

1. kutaifisha Dowans .....(my foot)
2. Dowans wafungue kesi huku mabepari wakitoa macho
3. Serikali ya Kikwete inafyata mkia na kuanza mazungumzo (ya amani?)
4. Baadaye inaamuliwa kuwa Dowans walipwe mabilioni ya fidia
5. Mpango wa kuilipa Dowans AKA Richmond AKA Loliondo unarudi ulikoanzia

Janja ya nyani kisagundulika wakati huo Zitto yuko Ujerumani anakula mrija kwa kuku
 
Jambo jingine ni kwamba,ukisoma vizuri taarifa ya Zito kuhusu kuathirika kwa kampuni ya Twiga cement kutokana na ukososefu wa umeme,anasema kwamba;namnukuu,..." Kwa mfano Kampuni ya Twiga Cement hutumia dola za Marekani 10 kama gharama ya kuzalisha umeme iwapo wanatumia umeme wa TANESCO."...kwangu mimi neno iwapo ni kama altenative,maana yake zipo njia zingine Twiga cement wanatumia badala ya umeme wa tanesco kama gesi ya Songos.


Donrich, tafadhali tetea pale panapoteteka. Kama mimi na wewe tunajuwa kwamba Twiga cement haitumii umeme wa TANESCO, mgao wa umeme unaathiri vipi Twiga cement?
 
Wenye Akili tulimcrash Zitto na idea ya kuitaifisha hiyo mitambo, wenzetu wakabaki kupongeza ujinga....! Tusubirie serikali kuinunua

Hivyo mwenye akili hukaa na kujilabu? Pengine ni njia ya kujitowa pahala panapostahiki.
 
Habari nilizopata hivi punde, Waziri wa nishati na madini Wiliam Geleja amesema serikali haitataifisha mitambo ya DOWANS, AMEDAI SERIKALI INA MIPANGO THABITI YAKUTATUA TATIZO LA UMEME NCHINI.
Hiyo mipango thabiti ilikuwepo tangu lini, au mheshimiwa waziri alikuwa anasubiri mpaka bwana Zito / wananchi waseme ndipo naye aseme? mimi nafikiri hii kazi imemshinda ni vizuri akawapisha wengine pengine watakuwa na mipango endelevu ya kuinusuru nchi.
 
Wakuu, naona hapa tunachanganya mambo. Kutaifisha/nationalization ni kuhamisha ulimiki kutoka kwa mtu au shirika binafsi kwenda kwa umma.

Lengo langu lilikuwa kumsahihisha Mkandara kwamba fidia sio lazima wala si haki ya mtu anayenyang'anywa umiliki wa rasilimali. Wala fidia hai-justify utaifishaji kwani kinacho justify utaifishaji ni dhana kwamba rasilimali husika ni muhimu kwa maendeleo ya umma as whole na kwamba umiliki binafsi unahatarisha au kukwamisha maendeleo au usalama wa umma. Kwa mantiki hii utaifishaji katika nchi yeyote duniani ni ubabe husiopingika.

Sasa tusipotoshe JF kwa kuchanganya utaifishaji na bail out. Bail out kamwe sio Utaifishaji, bailout ni nyongeza ya mtaji kwa kampuni inayokufa kutokana na ukosefu wa mtaji. Wala tusipotoshe JF kwa kuchanganya utaifishaji na ubia wa serikali katika makampuni mama katika uchumi wa nchi husika.

Very simple, utaifishaji ni unyang'anyi. Na mnyang'anyaji (serikali) anaweza kuwa na huruma na kumpa mnyang'anywaji kifutia jasho.
Mkuu hata sikuachi...
Mimi nimesema AIG imetaifishwa na serikali (nationalize) lakini wao wanatumia neno Bail Out..Hakuna mahala nimesema Bail out ni Kutaifisha, nimekupa mfano huo kwa sababu wewe umeuliza ni shirika gani ambalo limetaifishwa hivi karibuni nchi za magharibi..Nikasema AIG na baadhi ya bank...
Maadam AIG ni mali ya Umma, hivyo haijalishi kimetokea nini kufikia kuwa mali ya taifa. Na ndio maana nikasema hata kuchukua mali za criminal ni utaifishaji maadam serikali imezichukua mali hizo na kuwa za taifa, haijalishi kilichotokea maadam inatoika mkononi mwa mtu binafsi kwenda serikalini (Taifa).
Nikakupa tena mfano wa Privatization ambapo pia haijalishi yaliyotokea maadam shirika limetoka mkononi mwa Taifa na kuwa la mtu/watu binafsi.
Mkapa alichukua Kiwira ni Privatization, ATC na mashirika mengine tuliyouza ni Privatization, Mwinyi na Karume wamepora Majumba ya serikali (Msajili) ni Privatization, ingawaje kuna taratibu zinazotakiwa kufuata ili ikubalike kisheria. Hivi vipengele vya kuseize, confiscate, kulipa fidia (compasation) na kadhalika ni mbinu tu zilizotumika lakini mwisho wa yote maadam mali hiyo inachukuliwa na serikali na kuwa mali ya taifa neno Nationalization lina fit.
Hata hivyo tuendelee na mjadala kizungu lugha ya watu mimi simo tena!
 
Ungejuwa kwamba wapiga kura wengi hawajaona hata waya wa umeme husingeandika ulichoandika. Tatizo Dar na sehemu chache vikikosa umeme basi inaonekana NCHI imekosa umeme!! Tanasahau kwamba umeme ni kitu cha kufikirika miongoni mwa mamilioni ya watanzania!!

Kuwa na umeme bongo ni a privileged sio haki...
 
Ngeleja alichozungumza ndicho nilichotegemea kutoka serikalini.. haiwezekani hata aje yesu kesho mitambop ya Dowans kutaifishwa. Sio katika utawala huu kwa sababu huyo huyo Ngeleja muulize mitambo ni ya nani hatakujibu lakini mwepesi kusema serikali haiwezi kutaifisha kwa sababu anajua fika kwamba Rostam atawamaliza..
Nilimuunga mkono Zitto nikijua fika huu ni mtihani mkubwa kwa JK na utawala wake..Na hakika Ngeleja kajaa kama pishi la mchele.., hawa wote waliwekwa na Rostam, wote walienda omba kazi kwa Rostam/Lowassa na sii JK leo waje na hoja ya kutaifisha mali ya boss wao... thubutu!
 
Back
Top Bottom