Zitto aomba Bunge la dharura kumjadili Pinda

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Leo wakati Zitto anawasilisha hoja yake ya kutaka kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu pamoja na kuiwasilisha misingi ya maombi yake ametumia kanuni ya 27(4) ambayo inataka kuitishwa kwa Bunge la dharura na mwenye mamlaka hiyo ni Spika wa Bunge .

Kanuni hiyo inasema kama ifuatavyo; "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata,bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi,basi Spika anaweza ,baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi ,kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele au nyuma zaidi"

Kifungu hicho kimetumiwa na hivyo kwa kuwa Waziri Mkuu katangaza Bunge kukutana tarehe 12/06/2012 basi kuna uwezekano mkubwa likakutana mapema zaidi ili kujadili hoja hiyo.

Msingi mwingine wa hilo ni kutokana na ukweli kuwa kitendo cha waziri mkuu kuendelea kuwa ofisini huku akijua kuwa bunge linaweza kumjadili wakati wowote kinamfanya akose ujasiri wa kufanya maamuzi ama kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kudidimiza uchumi wa taifa , au hata kufanya maamuzi akijua kuwa wakati wowote anaweza kuondolewa.

naomba kuwasilisha.
 
zitto unatafuta nn Ww?, mbona nakuhurumia kabla? Kuwa mwangalifu.

Peleka ujinga huko mwizi wewe anataka nini kwani wewe unataka nini?!! mipesa yote hiyo mnaiba tu mna laana nyie mnatishia watu sasa hivi mtaona moto hamtaiba tena
 
Mkuu asante ka kuwakilisha,
Ila kasome sheria vyema, spika ndie baada ya kujiridhisha kutokana na kanuni na hoja ya mbunge baada ya kuipokea ndio anayeruhusu hoja hiyo ijadiliwe.

Pia ili PM atolewe ni lazima majority waunge mkono, sasa kwa wasomao alama za nyakati kitendo cha wana CCM 5 tu kuanguka signature zao ni ushahidi kuwa hata kama hiyo hoja italetwa itaangukia pua.

Mwisho uwe unafikilia kwa makini kabla ya kuleta hoja, Pinda pamoja na kuwa ananiboa kwa kutokuwa strong, ni mzoefu sana na hawezi kuathirika kutimiza majukumu yake kwa hizo signature 73, ushahidi wa hili angalia hotuba yake ya kuhitimisha.
 
MAsikini zitooooooooooooooooooooooooooooo

siasa sio kutumia nguvu misuri mpaka inatoka by ANa makinda

Zitto-K13.jpg
 
Mungu atawalaani tu wataondoka mmoja mmoja, maisha ya watanzania yanayopotea kwa ulafi wao .. utawarudi tu .. ngoja tuone kati ya MUNGU na huyo KIKWETE wenu nani zaidi...
 
Serikali yetu ni makini na sikivu, imepokea na itayafanyia kazi kulingana na taratibu husika
 
waziri mkuu kaahirisha bunge hadi Juni 12 na kapotezea changamoto za kujiuzulu! Naomba kujua, je leo uliwasilisha kwa Spika taarifa ya maandishi yenye sahihi 73? Kama uliwasilisha tutegemee nini tunaofatilia kadhia hii kwa hisia za uzalendo? Kama hukuwasilisha ni kwa nini?
 
Serikali yetu ni makini na sikivu, imepokea na itayafanyia kazi kulingana na taratibu husika
Nakuunga mkono kaka, haiwezekani uwe amiri jeshi mkuu halafu watu wakuburuze. Hata mimi najua kuwa kuna watu watawajibishwa kwa kufuata kanuni na sheria.
 
Nchi hii si ya Zitto peke yake, hivyo basi ni mbaya sana kufikiri jukumu hili ni lake peke yeye au G75. Wao wametimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni za bunge, na hoja ipo mezani kwa speaker. HOJA hii ipo pape pale hata kama wao wataamua kupindisha kanuni kwa manufaa yao
Ni vizuri tukielewa kuwa OPERESHENI UWAJIBIKAJI ni jukumu letu sote
 
Peleka ujinga huko mwizi wewe anataka nini kwani wewe unataka nini?!! mipesa yote hiyo mnaiba tu mna laana nyie mnatishia watu sasa hivi mtaona moto hamtaiba tena
Na alivyodharauliwa zitto hata kwenye hitimisho hoja yake haijaguswa. Mpe pole
 
Back
Top Bottom