Zitto ang'ang'aniwa viwanja vya Temeke Mwisho, asisitizwa asiondoke CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Jamani Taswira amekuwaje ??ninafatilia mwenendo wako.. Unataka kugain trust ya wanachadema hapa JF ili badae uanze mauzauza.. Huyu taswira tumtizame vizuri threads zake ambazo sio biased zinanifanya nijiulize maswali mengi.
 
Last edited by a moderator:
We ndo mnafiki usiyependa na kukubali ukweli. Zitto ni image ya vjana makini katika taifa hili na Chadema. Kumchukia akutaondoa ukweli huo.
unakurupuka sana shabiki
we ni walewale wanaosifia rangi ya kinyonga wakati yuko katika bustani wa mawaridi, ..akiwa kwenye rami unaijua rangi yake itakuaje..(ukishindwa kunielewa omba msaada)
 
[HUYU NDIYE ZITTO TUNAEMUITAJI NDANI YA CHADEMA VIVA ZITTO SIMAMA NA VIONGOZI WENZAKO IMARISHA CHAMA SIKU IPO TENA YAJA KWA UAMINIFU NA NIDHAMU NDANI YA CHAMA UTAKUWA ZAIDI YA ULIVYO.]Majuzi kwenye Mkutano wa CHADEMA,Mh zitto kabwe alikutana na kundi kubwa la vijana wakitaka kumgusa, namba zake, wengine wakitaka kuzungumza naye mambo yao.

Zitto bila ajizi alifanya hivyo baada ya kuona upepo wa kundi kubwa la watu wakimkimbilia kwa nyuma wakitaka kumbeba na wengine wakitaka kumsalimia.Usalama wa chadema ulikuwa makini sana kuhakikisha kiongozi huyu haguswi, lakini bado hali ilikuwa ni ngumu kutokana na mamia ya wanachadema kulizunguka gari lake huku wakipiga kelele mbalimbali.

Kubwa nililopata kulisikia kutoka kwao walikuwa wakimsihi Mh:Zitto atulie chadema, asihame. Walikuwa wakipaza sauti wakiomba namba za simu ili Mh:Zitto aweze kufika kwneye matawi na mikutano yao huko wanakoishi wanachama hao. Zitto alisikika akisema peoples Power, chadema tupo makini hatuyumbishwi na lolote.

Picha hizi ni namna wanachama walivyomkomalia Mh;Zitto atoe namba za simu na asikie kilio chao kwake.

Photo-0082.jpg

Wafuasi wa chadema wakipigana vikumbo kuhakikisha wanapata namba ya Zitto kabwe kwenye gari yake. Zitto aliwapatia namba hiyo kwa kuwatajia na kuwaandikia kwenye mikono na karatasi zao.

Photo-0085.jpg


ZITTO KABWE kama anavyoonekana kwenye Gari ndani akiandika namba za simu zake na kuwapatia wanachama wa chadema ambao walipiga kambi kwenye gari yake wakitaka namba zake za simu.

Photo-0093.jpg


Moja ya vijana waliokuwa waking'ang'ania Mh;Zitto awasikilize huku msafara ukiwa umesharuhusiwa kuondoka maeneo ya Temeke mwisho.
Photo-0091.jpg


Kijana anayeonekana amevaa miwani alilazimika kuondolewa kwa nguvu na maafisa usalama wa chadema,Kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alikuwa akipiga kelele za kumtaka Mh. Zitto asihame chadema.

Moja ya maneno niliyopata kuyasikia "Bro, Bro shusha kiooo unisikie Brooo, Nakuomba zitto, Nakuomba kaka usiondoke chadema, Usihame chadema kwenda CCM, ...Broo unansikia kweliii, nakuaminia sana Zitto"

Baada ya kuondolewa kwa nguvu kwenye gari la Mh Huyo kupisha msafara uondoke,Kijana huyo alijikusanya na wenzake pembeni wakijadili mambo mbalimbali kuhusu Mh;Zitto na Tundu lissu kwamba ni majembe ya chadema,Wamefurahi sana Zitto kuja kwenye mkutano ule.

Kitendo cha Mh. Zitto kushiriki mkutano wa temeke kilionekana kama ni ishara ya kujibu maswali ya watu wengi waliokuwa wakihoji kwanini zitto haonekani kwenye kazi za chama?Zitto aliamsha kelele za watu alipokuwa akimkaribisha katibu mkuu wa chama kwa kusema "naomba nimkaribishe rais ambaye hakutangazwa".Baada ya kutamka maneno hayo Zitto alishangiliwa sana kwenye viwanja hivyo.

Mkutano wa temeke ulionesha sura ya tofauti kabisa ya chadema(Umoja).watu wengi amabo walidhani viongozi au wabunge wa chadema hawaelewani walipata majibu yao kwamba hawa watu wapo pamoja.

Mbowe katika hotuba yake asilimia kubwa alisimamia kusafisha hali ya ukabila na udini unaotamkwa kuwa kikwazo ndani ya chama
[/QUOTE]
 
Kweli akili za wana chadema sawa sawa na za kuku zinasahau upesi majuzi tu mlimtusi kila tusi huyu kiumbe kiongozi na mfadhili wa masalia leo amegeuka lulu ama kweli wajinga ndio waliwao
 
Amefanya vyema kuonyesha bado yupo kundini! Mimi sielewi aliyewaambia watu kwamba alikuwa na mpango wa kuhama CDM ni nani!?
 
  • Thanks
Reactions: Hhm
Ni kazi ya CCM kuhakikisha CDM inaparaganyika ili wapate nafasi 2015...niliwahi kuandika last time kuwa Zitto is a great guy inteligent and matured!! hayo yanayosemwa SI KWELIIII...You seee !!! CCM tuwasikilize wanachokiongea But Tusiwaamini lets make sure our CDM is always front its M4C...Big Up Zitto Big up CDM leaders Big up wanachama na wafuasi wa CDM.....
 
Nadra sana Taswira kuja na uzi kama huu...anyway pamoja na kumpongeza Zitto kwa dhaati kabisa. Mimi nazidi kumpongeza sana M/Kiti Freeman na Katibu Mkuu kwa kuonyesha Ukomavu wa kisiasa...Zaidi ya pongezi hizo kwa moyo mkunjufu na mshukuru na kumuombea Kijana mwenzangu msomi jasiri, mwenye ueledi mtambuka, Jemedari alie katika mstari wa mbele kuwango'a magamba, Mhe sanaaaa BEN SAANANE! ...Nakuombea kwa Allah S.W.T akulinde na hasidi wenye kuhusudi my brother...
 
Kweli akili za wana chadema sawa sawa na za kuku zinasahau upesi majuzi tu mlimtusi kila tusi huyu kiumbe kiongozi na mfadhili wa masalia leo amegeuka lulu ama kweli wajinga ndio waliwao

kila jambo na wakatiwe ,kikumacho nini!
 
Hata kama taswira ni zitto haijalishi kikubwa ni kwamba zito amejitambua na kurudi kwenye mstari. Tunakutakia mafanikio mema na crew nzima ya cdm kwani nyie ndio watetezi wetu muliobaki. Pamoja.
 
Umiza akili bwana mdogo,usitake kuletewa kila kitu kama mama wa nyumbani,Taswira ndiyo Zitto Kabwe kama hautaki hacha

we unatumia kweli akili zako au za mkeo,hizo chuki binafsi zitakuua,mi nilikuwepo miongoni mwatu tuliokuwa tumelizunguka gari la zito,kiukweli jamaa anakubalika.
 
kweli zitto karudi kazini kama hata taswira sasa hivi anaisifu chadema kama taasisi na wala si mtu mmoja hapo safi. Jamani sisi wanachadema tunampenda sana zitto akiwa kama sehemu ya taasisi. Ukosoaji huwa unaanza pale anapotafuta mamabo yake . Zitto bado tunakuthamini sana

kitu ambacho wanajamvi wengine mnashindwa kutofautisha, siasa. Swali hapa ni jee mhe zzk aliondoka cdm, jee alitangaza kujitoa na kuamua ataenda ccm? Hapana hata siku moja hakusema hivyo wala hakutoa ishara hiyo. This is a true politician who deserves to lead cdm, n become the next president. He is here taking advantage of the situation to consolidate his popularity within chadema. Hiyo action ya kukimbiliwa na watu is one of it. Na mtamuona sasa katika kila mkutano wa hadhara wa cdm, na mtaona vituko wana cdm wote wakimshangilia yeye tu, itakuwa zito zito zito, na wala sio slaa au mbowe. He is charismatic and always a winner. Ataiteka cdm vizuri sana. Go zito go. Kwa hivyo hold your horses and start listening to the interiews he is going to start giving as of tmrw onwards.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom