Zitto anatuchanganya kuhusu posho! Wabunge CCM ndio...

Pius J. Kiwarya Lema

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
1,097
566
Nimemsikia mara nyingi akidaiwabunge wa upinzani waonyeshe
kwamba wanachukia posho!Wakati akijua posho za wabunge pale Bungeni ziko kisheria, wenye uwezo wa kuondoa ile Sitting allowance ni wabunge wa CCM ndio walio wengi CCM.

Juzi tena anadai Magufuli iondoe hizo posho wakati, tayari imeshaondioa zile zilizo chini ya mamlaka yake walizokuwa wanazipata wabunge kwenye mashirika ya umma!Anapopiga kelele kwa mtu asiyehusika ni kutuchanganya. Atoke apeleke hoja bungeni isipopitishwa awaambie watanzania wanaokwamisha ni Chama cha Mapinduzi kupitia wabunge wao kwa kuwa wako wengi!Kwanini anawaogopa kuwaeleza?

Ni kama anataka ionekane kama vile UKAWA ndio kizuizi badala ya CCM ambao ndo wengi?Zitto anajua kabisa Magufuli ni yule yule na CCM ni ileile asitarajie Miujiza!Kinachofanyika ni sasa kujitekenya mwenyewe na kucheka wenyewe!Yako wapi mabadiliko ya kisera kisheria na kifikra tuliyoyahitaji?

Kwa maoni yangu hii ni miaka mingine mitano ya kupoteza.
 
Kwani wabunge wa UKAWA hawajui kuwa posho za makalio ni dhulma kwa nini hawatoki mbele kumpa sapoti katika kulisemea na kuchukua hatua?

Utetezi wa kuwa eti ziko kisheria ni muflisi, sheria zipo hata zile kandamizi, na hiyo ni mojawapo!
 
Hivi ni kazi ya upinzani pekee kutetea maslahi ya watanzania?
 
Hivi wabunge wote wa upinzani wakipiga kura za kupinga posho na wale wa CCM wakapiga kura za kutopinga kwa style ile ya kumchagua spika suala hilo itakuwaje? Wengi wape demokrasia yetu. Nashauri bunge letu litunge sheria ya majority of the minority katika bunge hii itaondoa udikteta wa wingi na itawavuta wabunge kutetea maslahi ya kitaifa kwa pamoja kuliko ilivyo sasa. Na majority of the minority ifahamike kama watakaokuwa wachache au opposition au tawala maana kuna siku raisi atajashinda kwa kishindo lakini hana wabunge wengi na hapo itakuwa majority of the minority hata akiwa ni mtawala
 
Kwenye suala la posho wabunge wote ni wakali kama mbogo tu haijalishi chama hapo. Km utakumbuka vizuri mwaka jana majibu aliyojibu Lissu alipoulizwa kuhusu kupewa penshen kubwa hutopata shida kuongea yote hayo. Pia refer kwa dr slaa ambaye naye alishawah suggest kuhusu suala hilo na akakwama
 
Hakuna anayemlaumu tatizo anazunguka mno kwa jambo ambalo.anamjua mhusika ,,
Ukawa kama kweli wana uchungu na nchi waache tu kuchukua,posho ipo kisheria lakini onesheni kuigomea kwa kuikataa.Mbona mkigoma kwa mambo yalio katika sheria mnatoka bungeni kwa madai mnaburuzwa,suseni posho kwa madai mnaburuzwa kuiibia serikali.
Acha porojo,suala la posho ccm na ukawa ndipo wanakua kitu kimoja na wanaweza hata kukujeruhi
 
Hii michezo ya kucheza na akili za watu imeshafikia ukingoni !
Ni nani adiyekumbuka bunge la kumi Upinzani ulivyokomalia hili jambo mpaka likashindikana ??
Spika Makinda alisema hawezi kujibizana na wabunge wa upinzani wanaosema hawachukui posho kwa sababu posho inaingizwa kwenye akaunti moja kwa moja !!
Waziri Mkuu Pinda alisema "

"Kwani hiyo posho ni shilingi ngapi ?? ikitoka tu hapo nje zinaishia" !

Wakalumbana weee mwisho tukaachwa
solemba !

Kwa hiyo unataka mjadala mwingine ambao hutaki kulenga mlango wa kuingia ambao ndio kizuizi?? ( wabunge wz ccm)

Eti unaandika Namchukia zitto kwani ana nini alichonizidi ?
 
Nassari alienda China kutuletea vitanda vya hospital hajarudii???au wamemzuia tena Holili!!
 
Back
Top Bottom