Zitto: Anatetea Maslahi ya Taifa zaidi kuliko ya waliompa Ubunge?

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
Kuna madai kwa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini hawana imani na Mbunge wao, Kabwe Zitto hivyo huenda atalazimika kufanya kazi ya ziada ili abaki kwenye nafasi hiyo.

Inadaiwa kuwa, wapiga kura jimboni humo hawana imani na Zitto kwa kuwa tangu achaguliwe mwaka 2005 hajawasaidia.

Wapiga kura hao wametoa maelezo hayo walipozungumza waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa Habari mkoa Kigoma waliokuwa wakifanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo wakati wa mafunzo yao ya uandishi wa Habari za vijijini yaliyofadhiliwa na baraza la Habari Tanzania (MCT).

Wamesema,tangu Zitto achaguliwe mwaka 2005 kuwawakilisha bungeni,hawajawahi kumuona hata mara moja wakimaanisha kwamba, hajawahi kuwatembelea kusikiliza shida zinazowakabili, na pia hakwenda kutoa shukurani kwa kumchagua kuwa Mbunge wao.

Mkazi wa kijiji cha Bitale, Muyera Yahya amewaeleza waandishi wa habari kijijini hapo kuwa Zitto anapaswa kwenda na hoja nzito kuwashawishi wananchi wa kijiji hicho kumchagua tena kuwa Mbunge.

Yahya amesema, Zitto badala ya kwenda kufahamu matatizo yanayowakabili na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, amekuwa akizungumzia hoja za Buzwagi ambazo hazina umuhimu wowote kwao.

Mkazi wa kijiji cha Chankabwimba, Kayla Mussa, amedai kuwa,hata katika ziara za viongozi wa kitaifa wa serikali Mbunge huyo hashiriki, viongozi hao wamekuwa wakiambatana na wabunge wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Peter Serukamba.

Hivi Karibuni Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kigoma maalum kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa barabara za Mwandiga – Manyovu na Kigoma – Kidahwe kiwango cha lami, na katika ziara hiyo takribani wabunge wote mkoani Kigoma walihudhuria isipokuwa Zitto na Manju Msambya.

Sehemu kubwa ya Barabara hizo zinapita katika jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa muda mrefu mbunge huyo alikuwa akisema kuwa yeye ndiye aliyepigia debe hadi serikali kutafuta fedha kwa ajili ya miradi hiyo.

Wakati akiwa katika ziara hiyo,Waziri Mkuu alishangaa kutomuona mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini ,Zitto kwa kuwa miradi hiyo ipo jimboni kwake, wabunge wengine wa mkoani humo walihudhuria.

Waziri Mkuu alisema, kama ni bungeni hata yeye alikuwa huko na wabunge wengine alioambatana nao walitoka bungeni Dodoma hivyo alishangaa kwa nini Zitto hakuwapo na akahoji kama suala hilo halimuhusu.

Hivi karibuni, Pinda alimweleza Zitto bungeni kuwa, kama anataka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini itabidi afanye kazi ya ziada.
 
Chanzo cha habari hiyo juu ni gazeti la:Habari leo
toleo la tarehe 25/7/2009
 
Ugonile malafyale, habari hii umeinukuu wapi?
 
Malafyale,
Si ni wewe umekuja hapa juzi na habari za uzushi kuhusu Mwakalinga? Sasa tutakuaminiaje katika hili?
PS. Nani mmiliki wa Habari Leo?
 
Kwani akilitetea Taifa na sote tumeona hao wapiga kura wake si sehemu ya Taifa ? Sasa umeleta habari hii unataka tusemeje ? Anyimwe ama aache kutete Taifa akakae Kigoma kuwasaidia ? Kwanza awasaidie kwa njia ipi ? Una maana atope pesa mfukoni awape wao ama ?Hivi hajatetea lolote na Serikali ikafanya kweli huko ? Majibizano na Pinda hayakuwa juu ya moja ya wananchi hao kujengewa barabara kama sijakosea ?
 
Juu hapo wana JF wanaomba mtu yeyote mwenye kuona jambo amablo anahisi linajenga kwenye jamii zetu anatakiwa alete hapa lichangiwe,na mimi nimetimiza jambo hilo na sijui kama nimefanya kosa!(kama kuleta habari hii hapa ni kosa naomba sana msamaha kwenu wakuu)

Kuhusu maneno yako hapo juu mkuu Lunyungu,ni vyema maswali hayo ukawauliza watu wa Kigoma,ambao ndiyo waliolalamika(kama kweli)mimi nimeleta tu ili watu wasome na si zaidi ya hapo
 
Kwa kawaida si hulka yangu kushiriki kwenye mijadala ya kashfa kama washika dau wengine walivyofanya kwenye post inayohusu mdau Mwakalinga,lkn huwa nafanya uhakiki kabla sijaleta kitu hapa na nilichosema kuhusu harakati za mwenzetu na kugombea ubunge Kyela ni kweli tupu!

Labda ambacho sikueleweka ni kutumia tamathali za semi niliposema "Mwakalinga aingia Kyela" ukweli ilikuwa hajafika Kyela phyisical lkn "kiroho" tayari huyu jamaa alikuwa Kyela muda mrefu!

Jasusi,kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi August mwaka 2009,uwepo hapa ambako nitakuletea habari moja kwa moja toka ama kiwanja cha Mwakangale-Kyela mjini,au kutoka kule kijijini Katumba ambako labda rasmi mbio za kuwania ubunge Kyela zitakapotangazwa kuwa ndiyo zinaanza!
 
Labda ambacho sikueleweka ni kutumia tamathali za semi niliposema "Mwakalinga aingia Kyela" ukweli ilikuwa hajafika Kyela phyisical lkn "kiroho" tayari huyu jamaa alikuwa Kyela muda mrefu!!

Mmmhhhhhh!
 
Kwani akilitetea Taifa na sote tumeona hao wapiga kura wake si sehemu ya Taifa ? Sasa umeleta habari hii unataka tusemeje ? Anyimwe ama aache kutete Taifa akakae Kigoma kuwasaidia ? Kwanza awasaidie kwa njia ipi ? Una maana atope pesa mfukoni awape wao ama ?Hivi hajatetea lolote na Serikali ikafanya kweli huko ? Majibizano na Pinda hayakuwa juu ya moja ya wananchi hao kujengewa barabara kama sijakosea ?
Lunyungu.
acha kumdanganya Zitto.bado hajachelewa muda huu akienda jimboni mambo yatakuwa sawa.watu wa Mwandiga wanamuhitaji sana Zitto.
kuna CHADEMA wanamdanganya ZITTO agombee Kinondoni.asijidanganye mambo yote MWANDIGA.
 
Ujinga mtupu, wakati mwingine muwe mnakuja na hoja za maana. Kama ndio mmetumwa na mafisadi kuleta distraction mtachemsha tu. Kwani kuna ubaya gani Zito akitetea maslahi ya Taifa? Waliompigia kura ndio taifa wenyewe, na Zito anajua kama mabilioni yakiibiwa basi hata watu wake hawawezi kupata ule mgao wanaostahili. Uzuri ni kwamba hajajifungia kwenye chungu kama ilivyo kwa baadhi ya wabunge, ambao wanaona kuwa maslahi ya chama au maslahi yao ndio kila kitu. Bravo Zitto, bila shaka wana kigoma wametoa zawadi kubwa kwa watanzania kwa kukuchagua wewe kuwa mbunge.
 
Juu hapo wana JF wanaomba mtu yeyote mwenye kuona jambo amablo anahisi linajenga kwenye jamii zetu anatakiwa alete hapa lichangiwe,na mimi nimetimiza jambo hilo na sijui kama nimefanya kosa!(kama kuleta habari hii hapa ni kosa naomba sana msamaha kwenu wakuu)

Kuhusu maneno yako hapo juu mkuu Lunyungu,ni vyema maswali hayo ukawauliza watu wa Kigoma,ambao ndiyo waliolalamika(kama kweli)mimi nimeleta tu ili watu wasome na si zaidi ya hapo

kuna source kupata taarifa zisizo egemea kwa CCM lakini siyo gazeti la habari leo. Usitupotezee muda na mi-habari yako ya habari leo(CCM)
 
Lunyungu said:
Kwani akilitetea Taifa na sote tumeona hao wapiga kura wake si sehemu ya Taifa ? Sasa umeleta habari hii unataka tusemeje ? Anyimwe ama aache kutete Taifa akakae Kigoma kuwasaidia ? Kwanza awasaidie kwa njia ipi ? Una maana atope pesa mfukoni awape wao ama ?Hivi hajatetea lolote na Serikali ikafanya kweli huko ? Majibizano na Pinda hayakuwa juu ya moja ya wananchi hao kujengewa barabara kama sijakosea ?

Lunyungu,

..Buzwagi, na Richmond ni masuala ya kitaifa na Kigoma kaskazini ni sehemu ya taifa. lakini kuna mambo kama ujenzi wa shule, zahanati, uchimbaji visima vya maji, uhifadhi wa mazingira etc ambayo yanawa-affect wananchi wa Kigoma Kaskazini moja kwa moja na Zitto anapaswa kuyashughulikia.

..wananchi wa Kigoma Kaskazini wanahitaji mbunge aliyekaribu nao na anayetetea na kufuatilia masuala yao kuliko majimbo mengine mengi ya Tanzania. vilevile lazima tuelewe kwamba wananchi wa Kigoma kaskazini ndiyo waliompa Zitto platform ya kushughulika na masuala ya kitaifa kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni.

..binafsi sina matatizo ikiwa Zitto ataamua kutoa pesa mfukoni mwake kusaidia wananchi wenzake wa Kigoma Kaskazini. Watanzania tunapaswa kujenga moyo wa kujitolea. kuna mambo makubwa sana duniani yamefanikishwa kwa kutumia pesa za mfukoni za wananchi mbalimbali.
 
Wewe ni mwenyeji wa Kigoma kaskazini kweli au umetumwa hapa kuwasemea waliokutuma?
 
Kama mnaamini kuwa Zitto atakuwa na kazi kutetea jimbo lake basi wale wenye tamaa ya ubunge waende huko wakalipate hilo jimbo kwa urahisi
 
Mpita Njia said:
Wewe ni mwenyeji wa Kigoma kaskazini kweli au umetumwa hapa kuwasemea waliokutuma?

Mpita Njia,

..mimi siyo mwananchi wa Kigoma Kaskazini. pia hakuna aliyenituma niwasemee.

..ninachojaribu kusema ni kwamba Zitto can and should juggle btn kutetea masuala ya kitaifa na vilevile awe karibu na wananchi wake.

..Kigoma Kaskazini siyo sawa na jimbo la Ubungo au Temeke. Kigoma in general iko nyuma sana kimaendeleo wanahitaji wabunge waliokaribu nao na wakereketwa wa kweli wa maendeleo yao.

NB:

..habari kwamba Zitto amelitekeza jimbo lake zilianza kutolewa na waziri mkuu Pinda bungeni.

..vilevile kuna mchangiaji wa jamii forums namheshimu sana naye alidai mambo jimboni kwa Zitto siyo mazuri.
 
Mpita Njia,

...ninachojaribu kusema ni kwamba Zitto can and should juggle btn kutetea masuala ya kitaifa na vilevile awe karibu na wananchi wake.

..
lakini kumbuka Mkuu JK kuwa Zitto anajua anachokifanya, ni mwasiasa na kama ana nia ya kugombea tena lazima atakuwa amehakikisha kuwa ananiwekea mazingira ya ushidni.
Hilo moja, lakini jingine ni kuwa afadhali wewe umesema kwua hujafika hujo jimboni kwa Zitto lakini unajua kunahitaji maendeleo (naamini umesema hivyo kutokana na assumption kuwa sehemu nyingi za tz ziko nyuma kimaendeleo), lakini wapo wengine ambao wanazungumza with authority kuhusu jimbo hilo wakati hata ukiwauliza ili ufike huko unapita barabara gani hawajui.
 
Nafikiri ndugu yangu huyu hadi kuwa jasiri wa kuleta hoja mbele yetu inabidi tumsaidie. Hana elimu ya uraia na uzalendo katika kichwa chake. Hivi Kigoma au jimboni kwa Zitto Kabwe ni wapi, siyo sehemu ya Tanzania? Sijui lengo lake na sina hakika na habari hizi za wananchi kulalamika juu ya Kabwe kutowajali na kama wanafanya hivyo nao pia ni miongoni mwa wengi Wantanzania wasio na uzalendo na elimu ya uraia iliyomuhimu kututoa hapa tulipo na kuwa Taifa lenye maisha yenye NEEMA.

Tuna kila rasilimali muhimu zinazohitajika kwa ajili ya uzalishaji na maendeleo ya nchi. Lakini kwa sababu tunao watu kama hawa wa kuleta hoja kipofu kama hii, ndiyo maana hadi leo maisha yetu bado ni duni kwa walio wengi. Tanzania yetu iko chini ya mfumo wa Serikali Kuu ambapo rasilimali zote au mapato yote mengi lazima kwanza yaifikie Serikali hii ambayo kwa bahati mbaya haijafanikiwa kuzitumia rasilimali hizi kwa ajili ya maisha ya wananchi (watanzania) hata wale wa Kigoma.

Tunafahamu kazi anayoifanya zito. Kubwa ni kupigana vita ya kulinda matumizi mabaya ya rasilimali za watanzania. Tukifanikiwa katika hili ndipo litafuata la kugawa namna ya kutumia rasilimali hizo kwa wananchi ndani ya Tanzania (yaani "allocation"). Kama zoezi hili lingekuwa linafanywa katika usahihi na usawa hata Kigoma leo lingekuwa JIJI.

Hapa tatizo kubwa tulilo nalo Watanzania wengi ni umaskini wa ufahamu "yaani Illiterate Poverty". Watu hatujui haki ya kuwa mwanadamu, hivyo ni vigumu kutafuta au ku-support wachache wanaotia bidii ili haki zetu kama wanadamu tuzipate kutoka wa wale waliozishikilia mikononi mwao. Labda nifupishe kwa kusema kwamba, yawezekana ndugu yangu amekuja na hoja yake hiyo kwa sababu amejawa na "Itikadi za Chama cha Siasa fulani", lakini kama siyo hivyo; hakika hatupaswi kwa wakati huu kuwa tunajadili agenda dhaifu kiasi hiki.

Namaliza kwa kumuomba mtoa hoja awe makini kabla hajaamua ni hoja gani itawafaa wana JamiiForums.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom