Zitto anatapatapa, sasa naelewa kwanini alifukuzwa CHADEMA

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
987
Nimemsikiliza Zitto Kabwe wakati akichangia bungeni asubuhi kuhusu matukio ya watu kutekwa na kupigwa. Moja ya matukio aliyozungumzia ni kuvamiwa kwa mwandishi Absalom Kibanda.

Zitto amelitaka bunge kuunda Kamati maalum kuchunguza mambo hayo ambayo kwa mchango wake anaonekana kuyahusisha moja kwa moja na serikali.

Nimkumbushe Zitto kwamba, tukio la kuvamiwa Kibanda lilitokea baada ya yeye kuandika makala kuwatadharisha wapinzani hasa Chadema, kuhusu ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana.

Makala hiyo ilikuwa na kichwa cha habari; "Namuogopa Abrahman Kinana". Ndani ya makala hiyo alielezea sifa za Kinana kisiasa na kuweka wazi kwamba, haziwezi kufananishwa na viongozi wa upinzani akiwemo Slaa ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema.

Makala hiyo Kibanda aliandika akiwa Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wakati huo Chadema walikuwa kwenye mashambulizi dhidi ya Kinana baada ya kukabidhiwa 'mikoba' ya ukatibu mkuu wa CCM.

Baada ya makala hiyo, Kibanda akaondoka Tanzania Daima, inadaiwa ni baada ya kutokea kutoelewana na wakubwa wake.

Haikuchukua muda mrefu Kibanda akahamia gazeti la Mtanzania, hakukaa muda mrefu akavamiwa na kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana.

Nakumbuka moja ya maandiko yake baada ya kupata nafuu, nanukuu sehemu mojawapo; "Hakuna vita ngumu kama ile ya kutomjua adui yako au ile ambayo mtu au watu uliowaona kuwa ndugu na marafiki wanapogeuka kwa njia ya siri kuwa maadui wanaoamini katika kisasi chenye adhabu ya kifo kwa kosa la kuwakosoa tu".

Zitto Kabwe na kila anayesoma hapa aitafakari kauli hii ya Kibanda. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
 
Umeandika nini sasa ma ccm lumumba sasa zamu yenu kuokota makopo


Swissme
 
Anatafuta kiki mpya baada ya kupoteza dira na mwelekeo. Huwezi kukurupuka leo na kuibua mambo ambayo mlifanyiana huko chumbani mkashindwana halafu ukaanza kusingizia majirani. Hiyo huruma hutaipata
 
Siioni hoja yako. Kama kamati ya uchunguzi ikiundwa itatoa majibu ya kweli juu ya hisia zote zikiwemo na hizi za kwako.

Katika hili Zito yupo sahihi sana. Tunataka tuujue ukweli. Na kama kweli TISS inafanya haya basi ina maana imeacha kuwa Idara ya usalama wa Taifa na kuwa kikundi cha kigaidi. Ugaidi unatakiwa upigwe vita na wananchi wote, ikiwezekana hata kwa kushirikisha jumuia ya kimataifa. Hatuna urafiki na ugaidi.
 
Vipi na yale aliyoongea mh Juma Nkamia,na vipi kuhusu mh Bashe nae anaisingizia serikali ?hebu tia neno hapo mkuu!
 
Umeandika nini sasa ma ccm lumumba sasa zamu yenu kuokota makopo


Swissme

Ni matumaini yangu Bunge litaridhia kuunda tume ya kuchunguza kile kinachodaiwa "kuongezeka kwa utekwaji wa watu" wakihusisha moja kwa moja na Serikali.

'swissme': usijifiche ukweli utakapojulikana.
 
Anatafuta kiki mpya baada ya kupoteza dira na mwelekeo. Huwezi kukurupuka leo na kuibua mambo ambayo mlifanyiana huko chumbani mkashindwana halafu ukaanza kusingizia majirani. Hiyo huruma hutaipata
Very low argument! Kama kuna uhalifu kwenye chombo chochote, vyombo vya usalama vinazuiwa kuwachukulia hatua?
 
M naamini magufuli ndio anatafuta kiki maana amefunikwa mpka na halima bulembo duuh
 
Zitto anataka kujipendekeza kwa Mbowe ili tusijue kuwa Mbowe alikerwa na Makala ya Kibanda kumsifia Kinana kwny Gazeti la Mbowe la Tanzania Daima.

Baada tu ya Makala ile tuhuma zikaanza kuwa Kibanda kanunuliwa nae alipokerwa na kuamua kuhama na kuhamia Habari cooperation ndio Akavamiwa na kutolewa Jicho

Labda Kama Zitto anataka Kamati teule ili Mbowe aumbuke maana Wanasiasa ni Wanafiki anaweza akajifanya anakutetea kumbe anakupeleka kwny Kamba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom