Zitto anataka magazeti yamshinikize Waziri Mkulo kujiuzulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto anataka magazeti yamshinikize Waziri Mkulo kujiuzulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamura, Oct 14, 2011.

 1. K

  Kamura JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vyombo vya habari vimeripoti kwamba Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zubei Zitto anataka Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mukulo ajiuzulu ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusu tuhuma za kusitisha utendaji wa Bodi ya Shirika la Hodhi ya Mashirika ya Umma.

  Ninasema Zitto anataka magazeti yamshinikize Mkulo kustaafu kwa sababu anafahamu utaratibu wa kisheria kama Mbunge ambao anatakiwa kufuata ili Mkulo ajiuzulu. Utaratibu si kuchonga domo kwenye magazeti.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Aisee bado tuna kazi sana kama mawazo yetu ndio haya tena kwenye jukwaa linalojipambanua kuwa the home of great thinkers sijui...kinachoniumiza ni kwamba hakuna mabadiliko kwa watanzania,unaweza ukadhani kuwa labda as time goes on people altitude might change,but nothing new.Mkuu jaribu kuleta hoja kama great thinker kidogo,hizo hoja ni mipasho tu,sioni la maana hapo.Kabwe alikuwa anaongea na vyombo vya habari kuwapa taarifa,sasa ulitaka akatoe msimamo wake wapi? kwenye kamati ya chama,au bungeni? Tuache kukurupuka na kuleta hoja za kizembe ni aibu kwako pia japo yawezekana kwasababu hatufaamiani ndio maana kuna hoja nyingi uharo hapa JF....
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  How old are you Kamura?
   
 4. K

  Kamura JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo tumekuwa mabingwa wa kulalama bila kuchukua hatua. Sasa kama Mbunge ambaye ni miongoni mwa watunga sheria analalama kwenye magazeti bila kuchukua hatua stahiki, Mkulo atafanywa nini? Usitegemee ajiuzulu kama utaratibu wa kumsababisha ajiuzulu haujafuatwa.
   
 5. K

  Kamura JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,825
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuwa makini kwenye kusoma habari na kuielewa. Zitto amemuomba Mkullo apishe uchunguzi akiwa na maana Mkulo asiweke cumbersum kwenye uchunguzi unaofanyika na sio kujiuzulu. Think critically Mr.Green Guard.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  1. Kwa mawazo yako unadhani Zitto alipaswa kuchukua hatua gani?
  2. Kwa nini unaona hatua ya Zitto kqwenda kwenye vyombo vya habarui na kuliwe hili wazi kwa watanzania wote kuwa si kuchua hatua?
   
 8. K

  Kamura JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Source Mwananchi: Huko alikokwenda kulalamika ndiko wamemnukuu kwamba anataka Mkulo ajiuzulu sasa wewe unasema anataka apishe uchunguzi maana yake ni nini?
   
 9. K

  Kamura JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo suala linatakiwa litafutiwe ufumbuzi bungeni na hatua stahiki zichukuliwe kama ilivyokuwa kwa Jairo.
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Zitto alichofanya ni kuutarifu umma uozo wa Mkullo wala si vinginevyo.
   
 11. K

  Kamura JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli lakini kwa mtu makini hutakiwi kutoa tuhuma ukaishia hapo unatakiwa kuonyesha way-foward, huo ndio Ugreat Thinker.
   
 12. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Mkulo naye ni kati ya mawaziri ambao hawako active kabisa ,yupo tuu anchekacheka tu mweee tz mungu atusaidie
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kamura hebu toa utoto wako hapa..nenda kavae nepi huko huna unachokijua unasumbua watu tu hapa....
   
 14. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Una maana kuwa una uhakika Zitto kaishia hapo?
   
 15. K

  Kamura JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jibu hoja si kutoa lugha ya kifedhuli. Tatizo watu hamtaki kuliangalia hili suala kwa upana wake na manaishia kutukana tu, Zitto aligusia hili suala kwenye Bunge la Bajeti na ninachofahamu CAG inachunguza suala hilo sasa unaposema silijui unamanisha nini?
   
 16. K

  Kamura JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe unafikiri kaishia wapi kama si hapo? Tusiwe Jamhuri ya Walalamikaji.
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Nimegundua tatizo lako,una shida ya kutofautisha malalamiko na kutoa taarifa kwa umma,unapaswa kujua kuwa Zitto anapaswa kuripoti kwa waandishi ili umma upate habari,sasa kama ulitaka Zitto akaongee na mke wake nyumbani basi sema hapa.Tofautisha kutoa habari na kulalamika,na kwa nafasi yake kama M/kiti wa kamati ya kudumu ya mashirika ya umma alipaswa kuonyesha msimamo wake baada ya kutofautiana na mawazo ya waziri.....kusema kuwa ang'atuke sio kulalamika ila ni mawazo ya kujenga na kumaliza tatizo......acha kuleta hoja bila kufikiri mkuu!!!
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Kuna msemo mmoja unasema"Kama mtu hajui na anajiona hajui msaidie,kama kuna mtu hajui na anajifanya anajua achana nae".....tafakari chukua hatua....
   
 19. K

  Kamura JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anachofanya Zitto ni kutafuta cheap popularity tu.
   
 20. F

  Fahari MJ JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa manufa ya wale tusiojua tartibu au kama wewe ndio Ungekuwa zitto
  • Tuelezee na tufafnulie nini ungefanya ?
   
Loading...