Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.

"Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani," alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.


Source: UHURU

Sosi ni gazeti la Uhuru - sina la kuongeza
 
Kwa mtazamo wangu kuna mambo matatu hapa

1.Zitto ni mwanasiasa aliyekomaa tunaamini anafamu anachokifanya.

2.Uhuru ni jarida la chama tawala na linaolongozwa kwa sera za chama tawala na ni moja ya majarida yenye wahariri makini na wasomi (wanaotumika kwa maslahi ya chama tawala) tulikubali hilo.

3. binafsi ninaamini maslahi ya watanzania yataletwa na viongozi bora, wakiongoza wananchi wenye ari na nia ya dhati ya kupata maendeleo, sio lazima mabadiliko yaletwe na Zitto na sina mkataba na Zitto kuwa fanyanje nini na aseme nini. mpaka kufika hapa ninaheshimu juhudi zake na chama chake za kuleta mabadiliko, ningependa aendeleze juhudi zake za kuwatetea watanzania.
 
hawa ndio waandishi wa habari wa kitanzania, 3 months course kisha mtu nae ni mwandishi!!! what a joke!!! yaani hawana analytical skills kabisa! sasa hii habari ni kwa manufaa ya nani?inaonekana biased, twisted na unbalanced!!!

nawaheshimu waandishi makini waliopo bongo lakini aina ya waandishi uchwara kama hawa ndio wanaochangia media houses za tanzania zidharaulike!!

mfumo wetu wa elimu ubadilike ili waandishoi wa habari wanaopatikana wawe na skills za kutosha
 
Siamini hayo maneno yanatoka kwa Zito kwanza chanzo cha habari chenyewe ni CCM!!
 
Zitto ameshanunuliwa huyu, ukifuatilia kauli zake toka kipindi kile ambacho mama yake mzazi pia alihusika katika kale ka "mgogoro" Chadema na kuwa anabwabwaja hovyo utaanza kupata picha Zitto amekuwa ni mtu wa namna gani. Nafahamu kwamba ana mashabiki wake wengi tu humu ndani na mimi nilikuwa mmoja wao ila kijana wameshamharibu huyu kwa sasa. Mfano mwingine halisia ni siku ile alivyozindua kampeni zake jimboni kwake na moja kwa moja kuanza kuongelea habari ya yeye kugombea urais 2015 bila hata ya kuulizwa.
 
Zitto Kabwe atangaza kung'atuka

na Samuel Mwanga, Maswa


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametangaza kung'atuka katika wadhifa wake mwaka 2010.

Kabwe alitangaza adhima yake hiyo jana, wakati akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Greenbeach mjini Maswa mkoani Shinyanga.

Alisema amefikia uamuzi huo bila kushinikizwa na mtu yeyote na ameamua kutangaza mapema ili kutoa nafasi kwa wanaotaka kugombea nafasi hiyo, ili wajiandae.

Kabwe alisema anatamani kufanya kazi za kitaalamu, hasa zinazohusu taaluma yake baada ya kuwa mwakilishi wa wananchi kwa kipindi cha miaka mitano.

"Tangu nimalize masomo yangu chuo kikuu, ni kipindi cha mwaka mmoja tu niliofanya kazi kisha nikachaguliwa kuwa mbunge, hivyo nina hamu ya kufanya kazi nyingine mbali na hii ya uwakilishi," alisema Kabwe.

Alisema uamuzi wake wa kuachana na ubunge hauhusuni na masuala ya siasa ambayo iko katika damu yake.

Kabwe alisema kamwe hataachana na siasa bali baada ya kuachana na ubunge, ataendelea kufanya kazi za kuiimarisha CHADEMA ambayo imemfikisha katika mafanikio aliyonayo sasa.

Aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uaminifu na kushirikiana nao kuondoa kero mbalimbali zinazowakabiri pamoja na kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba kura.

Kabwe alionya kuwa kazi ya ubunge si lelemama kama baadhi ya watu wanavyofikiria, bali ni ngumu na inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu.

"Nimeifanya kazi hii ya ubunge kwa muda wa mwaka mmoja sasa, si kazi ya lelemama, ni lazima ujitolee kweli kuwatumikia watu, kwani kila tatizo linapotokea jimboni wananchi wanakutazama wewe mbunge," alisema Kabwe.

Kabwe ni miongoni mwa wabunge vijana wa CHADEMA ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wa mwaka 2005 alifanikiwa kuwashinda wagombea wa vyama vingine vya siasa.

SOURCE : TANZANIA DAIMA 1/03/2007
 
Thursday, 31 December 2009

Zitto Kabwe: Kumbikumbi huruka na kuliwa na kunguru

z.jpeg


ZITTO Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini, amekiri kumpa magari matatu ofisa habari za zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Kafulila.

Magari hayo anayatoa kama msaada kwa Kafulila ili aweze kushinda kampeni za ubunge katika jimbo la Kigoma Kusini. Hizi ni habari zinazozua maswali mengi, ikiwamo utajiri na uwezo wa Zitto kiuchumi.


Je, inakuwaje Zitto aweze kumiliki magari matatu wakati kipato chake kinajulikana? Lakini la pili, Kafulila na Zitto wanawezaje kuanza kampeni za ubunge wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijatangaza?


Tayari Zitto amekaririwa akisema, “Ni jambo la msingi kupunguza idadi ya wabunge wa CCM…ndiyo maana nimeamua kumsaidia Kafulila katika chama alichopo (NCCR-Mageuzi). Nipo tayari kujitolea kwa kijana mwingine anayegombea, hata kwa chama kingine, isipokuwa CCM.”


Kwa maneno ya Zitto ni kwamba anamuunga mkono Kafulila, ingawa bado anadai yuko CHADEMA. Ni ajabu kidogo. Je, kama CHADEMA wataamua kusimamisha mgombea Kigoma Kusini wakati Zitto ana mtu wake, atamuunga mkono nani kati ya mgombea wa chama anachodai kimemlea na kumkuza na kumfikisha hapo alipo na rafiki yake kipenzi?


Si vizuri kumsemea Zitto wala Kafulila. Kuna haja ya CHADEMA kuuliza swali hili kabla mambo hayajafika huko. Kwa sasa, Zitto ama kwa kujua au vinginevo, anaanza kujiona maarufu kuliko chama, kama Jakaya Kikwete-kwa mujibu wa maneno ya katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba.


Ifahamike. Kumbikumbi akaribiapo mauti huotesha mbawa na kuruka na kuishia kuliwa na kunguru.


Inapofikia mtu akafikia kujiona bora kuliko chama, huyu bila shaka hakifai chama wala chama hakimfai. Na lazima kuna tatizo, tena kubwa tu. Hivyo, uwezekano wa kukitosa chama wakati mbaya, hasa ule wa uchaguzi, ni mkubwa. CHADEMA wasingoje kufika huko.


Siasa za Tanzania zina bahati mbaya. Chama kinamlea mtu hadi kufikia umaarufu kama alivyo Zitto Kabwe sasa. Halafu mtu huyu aliyefinyangwa na kulelewa na chama, analewa sifa kiasi cha kujiona bora kuliko chama.


Mwisho wake huwa mbaya kwa mhusika na chama. Daniel arap Moi wa Kenya alifikia hatua ya kulewa sifa hizi pale alipoitwa profesa wa siasa. Alifanya ubabe hadi akakikosesha dola chama chake cha KANU.


Kuna haya ya wanasiasa kuchagua kati ya chama na urafiki. Tumekuwa tukimshutumu Kikwete na CCM kwa kuendekeza urafiki na kujuana. Hata wapinzani wanamlaumu kwa hili, hasa kwa kusema anaendesha nchi “kishikaji.” Hili sina mjadala nao wala sitaki kuingia undani wake. Lakini CHADEMA waangalie wasitoe kibanzi kwenye jicho la mwenzao wakaacha boriti kwao.


Zitto kwa watu wa nje ya chama chake anaonekana kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje. Ushahidi ni shaka juu ya msimamo wake. Kwenye mkutano wa Opesheni Sangara kule Tanga watu wanataka kujua kama Zitto bado yumo chamani au la.


Ni rahisi mtu kukanusha, lakini ushahidi wa mazingira unaweza kupaaza sauti kuliko mwenye kukanusha. Ingawa Zitto anasisitiza kuwa yuko CHADEMA, matendo husema zaidi ya maneno matupu.


Inakuwaje Kafulila awe mali kuliko chama? Zitto anapaswa kubanwa ajibu swali hili kwa usahihi na majibu yanayoingia akilini siyo kupiga siasa. Je, kwa kumuunga mkono Kafulila, hata dhidi ya uamuzi wa CHADEMA, Zitto hadhihirishi asivyokubaliana na hukumu aliyopewa Kafulila?


Kama chama kilimuona Kafulila ana makosa na kikafuata taratibu zote za kumtimua, naye akaamua kujitoa na kutoa kashfa nyingi, maana yake ni kwamba kuna mgongano hata kama wahusika hawataki kulikubali hili.


Litakuwa jambo la ajabu kwa mtu wa cheo na elimu ya Zitto kutoliona hili. Wenzake wamekaa chini wakamtimua Kafulila na kutaja makosa yake-kuvujisha siri za CHADEMA.


Yeye bado anamtetea. Je, huku si kutetea madhambi yake au kuonyesha kuwa kipenzi chake kimeonewa? Kwanini asimtetee kwa namna inayoeleweka badala ya kuendelea kukidhoofisha chama?


Ifahamike. Tunaelekea kwenye uchaguzi mwakani. Kwa uzoefu wangu, wanasiasa nyemelezi watavitelekeza vyama vyao, hasa baada ya kuahidiwa vinono na CCM. Nani mara hii amesahau akina Masumbuko Lamwai, Tambwe Hiza, Walid Aman Kabourou, Shaib Akwilombe, Salum Msabaha na wengine wengi? Kwanini uone ubaya wa chama baada ya kutimuliwa?


Ingawa kuhama vyama ni haki ya wahusika, wengi wa wanasiasa, hasa waliojirejesha CCM baada ya kukosa ukuu kwenye vyama vyao, wameonyesha kuwa nyemelezi na “changudoa.”


Ukiwaondoa watu kama Wifred Rwakatare na wengine wachache, wengi wamedhihirisha wanavyosaka madaraka badala ya kutumikia umma. Wamejivua nguo hata kama baadhi yao wanapewa madaraka ya kufinyangwa kama ilivyo sasa ofisi ya propaganda ya CCM, ambayo imegeuka dampo la wanasiasa nyemelezi.


Hivyo basi, CHADEMA wangembana Zitto wajue msimamo wake kwamba ni nani hasa atamuunga mkono kati ya mgombea wa chama chake na rafiki yake Kafulila.


Ni heri CHADEMA wakamkosa Zitto mapema kuliko kuwachenga saa za mwisho. Huu si wakati wa kucheza pata potea.


Bado Zitto ni mdogo kisiasa na kiumri. Ubunge wa kipindi kimoja hauwezi kumfanya awe yote katika yote hadi kuwa maarufu kuliko chama. Na chama kinapozidiwa umaarufu na mtu mmoja, kama CCM, kijue kinaelekea kuzimu. Nisingetaka CHADEMA wafike huko ingawa dalili zinaonyesha ukomavu wa hali ya juu katika kuyakata mawimbi haya na majaribu makubwa.


Zitto kaamua kumuunga mkono Kafulila wazi wazi, hata kabla ya chama chake kuamua kumsimamisha mgombea Kigoma Kusini. Anajiona si mchezaji bali mwamuzi. Je, alitaka kujenga mtandao ndani ya chama ili baadaye apate madaraka?


Na ikumbukwe. Hii si mara ya kwanza kwa Kabwe kupimana misuli na chama. Nani amesahau mvutano uliotokea hivi karibuni kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa chama? Je, Kabwe anatingisha kiberiti kwa ajili ya kuchukua uamuzi katika chaguzi ujao?


Chanzo: MwanaHALISI Desemba 23, 2009.
 
JEYKEYWAUKWELI
user-online.png
Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date
Fri Sep 2010
Posts 10
Thanks 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power 0

AHSANTE SANA MARALIA SUGU KWA TAARIFA NZURI
AHSANTE SANA KWA KUJIUNGA LEO LEO PIA
 
Anayegombea urais ni Dkt Wilbroad Slaa
.Umuhimu wa Zitto kwa sie wapenda mabadilijo hauna tofauti na Salma Kikwete.They could say whatever they want but we are not voting for them (except zitto huko jimboni kwake).
 
Source : UHURU

Mmmmmm, I doubt if this Newspaper can report anything impartial, he might have said that Mkapa tried his best but then came calamity JK which they did not report.

Kazi kweli kweli
 
Kumbe imeandikwa na Uhuru basi mie naenda kumeza dawa . Kazi yao ni ku twist lakini habari hii ndiyo yote nzima?
 
Kwa kifupi huyo ndiyo Zitto Kabwe ambaye sasa wafadhili wake (CCM) wanamshinikiza agombee uenyekiti wa chadema taifa ili akisambaratishe chama hicho ambacho kwa sasa ndiyo tegemeo kuu la watanzania na kisiweze tena kuinyima usingizi CCM katika suala zima la UFISADI ambao ndiyo MOYO na SERA mama ya CCM kwa hivi sasa. Wasiomjua Zitto wanaweza kupumua baada ya kusikia kuwa amejitoa katika kinyang?anyiro hicho lakini ukweli ni kwamba Zitto ataibuka na jambo lolote jingine hivi karibuni wakati chama hicho kikielekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika adhma nzima ya kuibomoa CHADEMA ili mradi tuu akaunti yake izidi kunona hata kama pesa hizo ni chafu. Ushahidi wa malipo mengi haramu kwa Zitto kutoka CCM nitauwekwa hadharani. ZITTO anaipenda CHADEMA na TANZANIA lakini PESA anaipenda zaidi!


SOurce:Nimjuavyo mhe. Zitto zuberi kabwe [Archive] - MwanaKijiji.COM
 
Kwa kifupi huyo ndiyo Zitto Kabwe ambaye sasa wafadhili wake (CCM) wanamshinikiza agombee uenyekiti wa chadema taifa ili akisambaratishe chama hicho ambacho kwa sasa ndiyo tegemeo kuu la watanzania na kisiweze tena kuinyima usingizi CCM katika suala zima la UFISADI ambao ndiyo MOYO na SERA mama ya CCM kwa hivi sasa. Wasiomjua Zitto wanaweza kupumua baada ya kusikia kuwa amejitoa katika kinyang?anyiro hicho lakini ukweli ni kwamba Zitto ataibuka na jambo lolote jingine hivi karibuni wakati chama hicho kikielekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika adhma nzima ya kuibomoa CHADEMA ili mradi tuu akaunti yake izidi kunona hata kama pesa hizo ni chafu. Ushahidi wa malipo mengi haramu kwa Zitto kutoka CCM nitauwekwa hadharani. ZITTO anaipenda CHADEMA na TANZANIA lakini PESA anaipenda zaidi!

SOurce:Nimjuavyo mhe. Zitto zuberi kabwe [Archive] - MwanaKijiji.COM



Kama katiba inaruhusu tatizo liko wapi akigombea nafasi ya mwenyekiti ?...si ndio demokrasia?? Wewe source kwamba anashinikizwa na CCM umezitoa wapi? wacha stori za udaku
 
23 September 2010
Na waandishi wetu


kabwee_fr.jpg


WAKATI kampeni zikipamba moto, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, amekiri serikali ya CCM imejenga uchumi imara. Amepongeza utendaji kazi wa serikali za CCM na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi.

Zitto anayewania ubunge Kigoma Kaskazini, alisema hayo juzi jioni katika Uwanja wa Mashujaa, alipomnadi mgombea ubunge wa Mtwara Mjini, kwa tiketi ya chama hicho, Jetha Othuman. Akizungumzia mafanikio ya serikali ya CCM, Zitto alimmwagia sifa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akisema amefanya mambo makubwa katika uongozi wake na kama kuna makosa ni ya kibinadamu.

“Hakuna anayeweza kila kitu kama yapo yaliyomshinda huo ni ubinadamu,” alisema Zitto na kuongeza kuwa, uchumi imara uliwezesha kushuka kwa mfumko wa bei. Aliwaponda watu wanadai serikali ya CCM inabagua wapinzani, akisema imekuwa ikitekeleza Ilani kwa kufikisha maendeleo hata kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani.

“Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani,” alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.


Source: UHURU

Unategemea nini pale source inapokuwa uhuru au mzalendo?
 
Hata biblia ina tafsiri tofauti kulingana na ufinyu wa mawazo ya anaetafsiri ndo maana wemgi wamewehuka kwa tafsiri potofu hivyo sikushangaa kusikia hivyo baada ya kugundua kuwa source ni gazeti la uhuru. Afu ukumbuke kuwa upinzani c kupinga kila kitu lakini kwa serikali ya kikwete hakuna cha kuunga mkono, sioni tatizo kama kabwe alimsifia mkapa kwa sababu hata nyerere ambae ni roll model wetu alikuwa ccm na tunapomsifu, tunamsifu yeye kama yeye na siyo ccm.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom