BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Zitto: Kuna njama
na Mwandishi Wetu
Tanzania daima
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema chama hicho kimegundua kuwapo kwa njama mahususi zinazoendeshwa na baadhi ya watu wenye lengo mahususi la kuwasambaratisha.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili jana, Zitto alisema njama hizo zinafanywa na watu hao ambao hakuwa tayari kuwataja ambao wamekuwa wakitumia baadhi ya vyombo vya habari.
"Tumegundua kuwapo kwa juhudi za makusudi za kutaka kutugombanisha CHADEMA. Hiki ni chama makini, kimezibaini njama hizo na kwa hakika hakiwezi kusambaratishwa na njama hizo," alisema Zitto.
Akifafanua, Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa wapo wanaotumia jina lake, wakilihusisha na matukio fulani, kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa yeye ni maarufu zaidi, au muhimu zaidi kuliko chama hicho.
"CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake," alisema Zitto.
Akitoa mfano katika hili, alisema wakati alipoamua kugombea ubunge alikuwa ndiyo kwanza amemaliza masomo yake ya chuo kikuu na kimsingi kulikuwa hakuna watu waliokuwa wakimfahamu.
"…eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta grassroots network ya chama, hakikujengwa na mimi.
"CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo, nilikuta uongozi intact (imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote. Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofikia 10,800 katika jimbo zima. Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.
"Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?" alibainisha Zitto akinukuu habari na taarifa za vyombo kadhaa vya habari.
Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni kuwakatisha tamaa watu aliosema wana nia mbaya na chama hicho, Zitto alisema kuwa ni vigumu kuisambaratisha CHADEMA kwa propaganda kama hizo kwani tayari imeshajijenga katika misingi ya kitaasisi.
Alisema kuwa CHADEMA ni moja kati ya vyama vichache vya upinzaani nchini ambavyo kimeendelea kuwa na viongozi wastaafu ambao wanaenziwa ndani ya chama.
"CHADEMA ni chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya chama… institutional memory ipo kuliko katika vyama vingine vya upinzani," alisisitiza akiwazungumzia Edwin Mtei na Bob Makani.
Alisema kuwa wanaodhani kuwa watu binafsi ndio wanaoipa CHADEMA umaarufu wanakosea, kwa sababu wapo watu wengi maarufu ambao awali ilikuwa ikiaminika kuwa wakihama katika chama hicho kitasambaratika, lakini hilo halijatokea.
"Alipohama (Dk. Aman Walid) Kabourou wengi walidhani ndio mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali," alisema Zitto.
Zitto alikuwa akijibu hoja zinazolenga kuonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kusambaratika iwapo yeye ataondoka kwenye chama hicho.
Hoja hizo zinajengwa katika misingi kuwa Zitto ni mtu ambaye anakijengea umaarufu chama hicho, kwa hiyo kumfanya yeye kuwa msingi wa uhai wa CHADEMA.
Kikubwa kinachotajwa sasa katika vyombo mbalimbali vya habari hivi sasa ni uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa mjumbe katika kamati ya kuchunguza mikataba ya madini, hatua ambayo iliibua msigano wa maoni ndani ya chama hicho cha upinzani.