Iwensanto
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 1,173
- 1,092
Hiyo ni kweli jamaa aliiharibu nchi
Mimi ni mtu naependa consistency, mtu akishakua unpredictable siwezi kumuelewa.
Leo Zitto anashinda mitandaoni anamsema Marehemu Magufuli kwamba aliharibu uchumi, hakuna kitu alichofanya na kumbebesha lawama zote za udhaifu ama inefficiency ya serikali ya awamu ya sita kwamba ilisababishwa na Magufuli.
Msikilize hapa Zitto akimwagia sifa lukuki na sifa kede kede Magufuli enzi za uhai wake alipotembelea Kigoma. Zitto anakiri kua Magufuli amewapelekea watu wa kigoma maendeleo na anasema ushahidi ni idadi ama nyomi ya watu waliopanga msululu ama msafara barabarani kumlaki Magufuli.
Zitto anakiri kabla ya Magufuli watu wa kigoma hawakua na maji ila serikali ya Magufuli imewapelekea maji.
Leo hii Zitto anashinda mitandaoni kumtukana Marehemu Magufuli wakati enzi za uhai wake amemsifia mbele yake.
Zitto tunajua hupendi ama hutaki mama aonekane hana uwezo, sasa unashirikiana na wabaya wa Magufuli kuhamishia udhaifu wa serikali ya awamu ya sita na matatizo yake kwa Magufuli ila watu wenyewe wanaona kwamba hii serikali imeshindwa kabla haijaanza, failed from the start.
Miezi 6 tu hakuna umeme, hakuna maji, mafuta bei ghali, vifaa bei ghali na sio muda nchi itakosa chakula.