Zitto anakataje Rufaa wakati aliomba kujiuzulu?

Z
Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM.

Huyu mtoto yuko timamu kweli? Yeye anapoleta hoja za CCM za ukabila na udini ndani ya CDM anajiona anafanya tofauti na CCM? Kauli za Zitto na kauli za Nape/Mwigulu zinafanana, tofauti yake na maCCM ni nini?
 
habar jamiiforums.
Bila shaka kila mmoja wetu anajua sakata lililoko chadema kwa wakati huu, sakata hili huenda lisiishe leo,kutokana na kamati kuu ya chama kuendelea kusubiria utetezi wa watuhumiwa, lakini kinachoshangaza katika hili, ni kwanini mmoja wa watuhumiwa ambaye ni zitto, alikata rufaa kwa baraza kuu, ili hali yeye mwenyewe alishawasilisha maombi ya kuachia nafasi zote ndani ya chama? Kwa mujibu wa chadema kupitia kwa mwanasheria wake na gwiji wa sheria
mh.antipas tundu lisu.

hebu twambie zitto alijiuzulu?au alinyang'anywa vyeo na kusingiziwa makosa kibao?

Zitto ana kata rufaa kupinga kile kilicho fanywa na kamati kuu cha kumvua vyeo na kumpakazia makosa chungu nzima.

Zitto alitaka kujiuzulu lakini wenye chama wakasema asijiuzulu bali wamfukuze kwa aibu kwa kumhusisha na makosa kibao.

Zitto alitaka kujiuzulu akiwa clean lakini si kuchafuliwa na kufukuzwa na hii ndio imemfanya kukata rufaa kupinga uamuzi wa kijuha wa kamati kuu ya chadema.
 
Nadhani aliomba kujiuzulu kwa hamaki (alifumwa kwenye kona "unprepared"). Ila aliporudi kwa "waajiri" na "washirika" wake wakamwambia zege halilali ni lazima "agangamale potelea mbali".

Zitto hana nia njema na CHADEMA. Zitto hawezi kutufundisha demokrasia au namna ya kumpima/kumhukumu mwanasiasa yeyote yule nchini na duniani. Zitto hawezi kuaminika tena kwani alipoaminiwa kwanza yeye aligeuka na kuwa msaliti, mharibifu na ndumilakuwili.

CHADEMA naomba CC yenu, ikiwezekana Januari 2014, ikutane kujadili utetezi wa Zitto na kutoa hukumu haraka sana. Kuchelewa kwenu mnalea ugonjwa na kusababisha magonjwa nyemelezi pia kuchipuka.

Sina shaka hukumu itapasa kumvua uanachama Zitto, yaani avuliwe na afukuzwe CHADEMA.....hiyo ni pretext ya FACTS on the ground.

Ana jasho lake? My foot. Well hizo stereo-type claims zake hazina mashiko. Kama vipi atupe kiasi (quantity) na bei ya "jasho lake" tumlipe. Mpuu.zi SANA. Kila siku anajifanya ana mchango mkubwa CHADEMA, ni upi huo autaje na tuujue. Ukiondoa umaarufu aliojengewa na chama "reciprocally" mchango wake ni chini ya wastani wa mwanachadema yoyote wa kawaida.
 
...

Maoni yangu.
Angekuwa mtu wa heshima na mnyenyekevu na mtii kwa viongozi wake sidhani kama angeweza kiandika ujumbe kama huo. Huyu dogo wangempiga chini tu hata chama.kikifa bora kuliko kukaa na kirusi mbaya kama huyu!

Mkuu hii umei'quote' kutoka wapi....!? Nahitaji 'source' kwa ajiri ya kuboresha kumbukumbu zangu.
 
Hivi ni kwa nini Zitto anatumiaga sana fesibuku, kwanini hapendagi kuleta maoni yake kupitia jf??

ndg yangu zitto akikanyaga huku atapewa hata majina ya panyabuku, jf hawampendi sababu alitishga uhai wa panya wao majumbani
 
Last edited by a moderator:
Nadhani aliomba kujiuzulu kwa hamaki (alifumwa kwenye kona "unprepared"). Ila aliporudi kwa "waajiri" na "washirika" wake wakamwambia zege halilali ni lazima "agangamale potelea mbali".

Zitto hana nia njema na CHADEMA. Zitto hawezi kutufundisha demokrasia au namna ya kumpima/kumhukumu mwanasiasa yeyote yule nchini na duniani. Zitto hawezi kuaminika tena kwani alipoaminiwa kwanza yeye aligeuka na kuwa msaliti, mharibifu na ndumilakuwili.

CHADEMA naomba CC yenu, ikiwezekana Januari 2014, ikutane kujadili utetezi wa Zitto na kutoa hukumu haraka sana. Kuchelewa kwenu mnalea ugonjwa na kusababisha magonjwa nyemelezi pia kuchipuka.

Sina shaka hukumu itapasa kumvua uanachama Zitto, yaani avuliwe na afukuzwe CHADEMA.....hiyo ni pretext ya FACTS on the ground.

Ana jasho lake? My foot. Well hizo stereo-type claims zake hazina mashiko. Kama vipi atupe kiasi (quantity) na bei ya "jasho lake" tumlipe. Mpuu.zi SANA. Kila siku anajifanya ana mchango mkubwa CHADEMA, ni upi huo autaje na tuujue. Ukiondoa umaarufu aliojengewa na chama "reciprocally" mchango wake ni chini ya wastani wa mwanachadema yoyote wa kawaida.

we ni m .ke wa kamanda wa anga!!!!
 
Zitto wewe ni mzandiki na mzushi .Wapambe wako wamekuwa wakisema Udini kule Chadema kumbe hata kiatu chako cha kwanza ----------- na Mgalatia .Mtoto wako umezaa na Mgalatia na unaishi naye .Leo unakosa heshima kabisa hata zile za kiafrika kwamba Slaa ni kama mzazi wako .Upumbavu wako utakugharimu ila najua unafanya haya kuwaonyesha wenzako kwamba unaweza ivuruga Chadema .Haya sasa they have gone public Slaa kasema wapambe wana kuhatarishia maridhiano endele na mikutano Kasulu utajua maamuzi yakoke soon .
 
Yu wapi zito yuleee wa kabla ya 2008 mkimwona mwambieni tunaye mzito mwingine anadanhanya umma kuwa anakipenda chama chake cdm lakini anaharibu tawira ya chama na viongozi wake sasa sijui anataka kuwa na chama kisicho aminiwa na wananchi?!
 
ZZK has to go,he lacks respect to the party! If he thinks is more than a party why shouldn't he leave and form his party? So that all his followers should join him!
 
....I can assure you, it was a wrong chosen target for neutralizing Chadema. They have to go back to the draft board.
uzoefu unaonyesha watu muhimu wanapotoka kwenye chama wanauwezo wa kukichachafya chama kwa kipindi fulani, kama alivyowahi kufanya sharifu hamad (zanzibar), dr.slaa na lyatonga mrema walipohama ccm katika vipindi vyao tofauti, lakini ukweli utabaki palepale kuwa mwisho wa siku MM(kama anayo hatia) ataondoka na yake na kukiacha chama kinaendelea. uamuzi mbaya ni kumwacha kiongozi anayekigawa chama kimakundi. 2015 sio mbali sana na wasipochukua hatua za kinidhamu mapema watakuja kujikuta hawana mwelekeo uchaguzi ujao.

hofu ya watu wachache ni kutaka kuaminishwa kuwa chadema ni kigoma na bila MM wana-kigoma hawataikubali CDM tena, na huu ni udhaifu wa kupuuza nguvu za mikoa mingine mingi nchini. hata kafu inaendelea lakini ina nguvu sehemu fulani katika nchi, ccm wenyewe kuna mikoa hawana sauti nchini lakini hili jambo halijawafanya wayumbe kama chama. CDM wanatakiwa wajue wanaweza kuipoteza kigoma inayomfuata MM lakini ikachukua mikoa mingi zaidi tanzania inayofuata CDM na pengine hata visiwani na kuendelea kuwa na nguvu nchini.

MM anaamini anapendwa sana na wanakigoma wenzake na wasanii wamuziki wa bongofleva hususan kigoma all stars ambao wamekuwa wakitumika kumpigia debe kwenye ishu nyingi ukizingatia wasanii wanakuwa na uwezo wa kuwashawishi wananchi kuliko makundi mengine ya wasomi. na ndipo wanaoamini ana nguvu sana wanapojitokeza. MM aliwahi kuwahakikishia wana-kigoma kuwa akirudi atagombea urais, pia alisema 2015 ataacha siasa na kuwa lekcha, na pia amekuwa na mienendo inayopelekea watu kumshuku na kupoteza imani naye ndani ya chama na yeye akidai CDM inamwonea wivu urafiki wake na JK, ni ngumu kuamini kuwa nakala ya mkakati wawa ushindi inamtaja yeye kama kiongozi wanaomtaka, ukizingatia kashfa zilizowekwa kwenye maelezo ya mkakati wa ushindi kwa viongozi wao ambazo hazijawahi kuwasilishwa katika mikutano ya chama zenye kila dalili ya kutengeneza makundi na kukigawa chama. zaidi ya yote jamaa is so cunning and very unpredictable all the time, meanwhile to keep him is too risky like to dump him. yeye binafsi hataki kutoka.

nachoamini MM hafanyi yale anayoyafanya kimakosa bali anayo-target fulani, japo ukimfuatilia unaweza kudhani hana target. ninachoamini hata kama unatetea demokrasia kama mtu makini lazima uwe na target, tofauti na hapo utajikuta unawavuruga na unabomoa kile unachotaka ukifikie, ndio maana naammini MM anayo-target, na sio hiyo anayoiweka hadharani, kubwa niionayo ni ile ya yeye kuwa rais ifikapo 2015 na pengine vikwazo vilivyojitokeza vya kunyimwa nafasi hii muhimu, katika safari yake ndivyo vilivyomfanya aandae mkakati utakaohakikisha anafikia lengo kama ambavyo aliwaambia wanakigoma kuwa 2015 atakuja kama mgomba urais na sio mbunge tena.na urafiki wake na JK ni kujifunza mbinu ili mpango wa kuhakikisha anafikia pale kwani JK naye alifanikiwa kwa mtandao, na wote wamefanikiwa kuwateka wasanii wa muziki nchini, wanaodhani MM anaonewa hawaliangalii hili kwa kina. CDM wanayohaja kufanya maamuzi magumu ikibidi hata kama wataipoteza Kigoma ya MM na wasanii wake.
 
hii haiwaachi salama chaga saccos.

Kaka watetezi wa Zitto ni wa aina yako basi hana future .Unawatukana wachaga ? Zitto mtoto wake anaitwa Chachae kazaa na Jaqueline ni mchaga .Zitto kalelewa na Mbowe hadi kufikia hapo Mbowe akina hana shuke sawa na Zitto lakini ndiye kamfikisha hapo.Matusi yenu na udini sasa kamuulize Ndugai yameanza ya ukabilsa kule kwake na CCM ndiyo waasisi .Endeleni mtakuja kuona
 
Mmezoea mno kudanganywa katika siasa zetu hizi za bongo. Mkiambiwe ukweli mnadhani ni uwongo na wanaopigia uwongo ndio mnaowaamini. Sie tulio ndani na tunakula mshahara wa ruzuku ya CDM tunajua kinachoendelea. Hawa viongozi wetu hawapo serious na wanajua hivyo. ZZK alichotakiwa kufanya ni kwenda Moshi apande mlimani Kilimanjaro na kwa sauti kubwa atangaze kuwa "Mimi Zitto Zuberi Kabwe kamwe sitogombea uenyekiti wa CHADEMA hadi pale Mheshimiwa Mbowe atakaponiruhusu na wala sitothubutu kuchukua fomu ya kugombea urais". Angefanya hivi angetangazwa kwamba ni kijana jasiri asiyetaka makuu, ni mchapa kazi ndio tegemeo la chama chetu.
 
habar jamiiforums.
Bila shaka kila mmoja wetu anajua sakata lililoko chadema kwa wakati huu, sakata hili huenda lisiishe leo,kutokana na kamati kuu ya chama kuendelea kusubiria utetezi wa watuhumiwa, lakini kinachoshangaza katika hili, ni kwanini mmoja wa watuhumiwa ambaye ni zitto, alikata rufaa kwa baraza kuu, ili hali yeye mwenyewe alishawasilisha maombi ya kuachia nafasi zote ndani ya chama? Kwa mujibu wa chadema kupitia kwa mwanasheria wake na gwiji wa sheria
mh.antipas tundu lisu.
kwa sababu alikataliwa kujiuzulu, hivyo ameadhibiwa na ndio sababu ya rufaa kupinga adhabu
 
Back
Top Bottom