Zitto anakataje Rufaa wakati aliomba kujiuzulu?

Mungai Msele

Senior Member
Dec 19, 2013
105
0
Habar Jamiiforums.
Bila shaka kila mmoja wetu anajua sakata lililoko Chadema kwa wakati huu, Sakata hili huenda lisiishe leo,Kutokana na Kamati kuu ya Chama kuendelea kusubiria utetezi wa watuhumiwa, Lakini kinachoshangaza Katika hili, Ni kwanini Mmoja wa watuhumiwa ambaye ni Zitto, Alikata Rufaa kwa baraza kuu, Ili hali yeye mwenyewe alishawasilisha maombi ya kuachia nafasi zote ndani ya Chama? kwa mujibu wa Chadema kupitia kwa Mwanasheria wake na gwiji wa Sheria
Mh.Antipas Tundu Lisu.
 
Hebie

JF-Expert Member
Jul 29, 2012
1,347
2,000
Washauri pamoja na mwanasheri wa zitto hawajagundua kuwa zitto anahitaji msaada wa kisaikolojia (pyschology cauncelling) wakigundua hili hataendelea kuvurunda.
 
Mungai Msele

Senior Member
Dec 19, 2013
105
0
yule hatoki mpaka aakikishe anakiua chama

Ni sawa lakini mwanasheria wake analijua hili? maana barua ya zitto ilipokelewa CC ya chama ambayo alikua akiomba kujiuzulu. lakini cc ilijua maasi yake haikumruhusu.
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,280
2,000
Zitto hata hotuba zake ni wendawazimu, huw anajikweza,na kujishusha bila hata kujua anajipinga.Huyu chalii atakuwa kala dawa mbaya akili ikahama km si issue za giza.Zinazomsukuma kufanya mambo kinyume wakati yakipanda na wakati yakishuka.

cc:HAMY-D
 
2013

JF-Expert Member
Jan 1, 2013
11,330
2,000
Ni sawa lakini mwanasheria wake analijua hili? maana barua ya zitto ilipokelewa CC ya chama ambayo alikua akiomba kujiuzulu. lakini cc ilijua maasi yake haikumruhusu.
mwanasheria ni mtu anayefanya kazi kwa maslahi ya mteja wake,
hawakutaka ajiuzuru kwani ingekuwa kama maamuzi huru, badala yake walitaka waonyeshe kuwa ztto amewajibishwa kwa makosa yake.
 
Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
935
1,000
Zitto Kabwe
Nitapambana kutetea uanachama wangu.
Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM. Tuhuma za matumizi
mabaya ya fedha za umma kwa upinzani ni mbaya zaidi kuliko. Hivyo
uwajibikaji kwa wote bila kujali vyama. Uwajibikaji sio msamiati kwa
watawala tu bali kwa viongozi wote. Namna tunavyotaka nchi iendeshwe
ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa
Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna
ile ile wanayohukumiwa watawala.
Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina
jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya
uanachama wangu.
Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio
wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine
wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa
upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha
operesheni tokomeza!

Maoni yangu.
Angekuwa mtu wa heshima na mnyenyekevu na mtii kwa viongozi wake sidhani kama angeweza kiandika ujumbe kama huo. Huyu dogo wangempiga chini tu hata chama.kikifa bora kuliko kukaa na kirusi mbaya kama huyu!
 
TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
0
Sasa hapo kinachokushtua ni nini?Mbona anasema kweli tupu?Mara nyingi tu baadhi ya Makada wahamiaji wamekuwa wakimshambulia Zitto kupitia mitandao ya kijamii wakimtuhumu hana uzalendo na Chama na hilo nalo hulijui?
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Na nyie mnaendaga kutafuta nini huko kwenye mafesibuku yao? ona sasa mlilengwa nyinyi umetuletea na sisi. aaah!!!
 
nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,898
2,000
Zitto ni sawa na gari moshi iliyokatika breki

lazima lipinduke, na kwakua hajielewi soon tunachukua na uanachama wake kuthibitisha anguko lake
 
Queen Kyusa

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
663
250
Dah yani hata huwezi kuelewa zitto kabwe analengo gani!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
2,090
2,000
Zitto Kabwe
Nitapambana kutetea uanachama wangu.
Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM. Tuhuma za matumizi
mabaya ya fedha za umma kwa upinzani ni mbaya zaidi kuliko. Hivyo
uwajibikaji kwa wote bila kujali vyama. Uwajibikaji sio msamiati kwa
watawala tu bali kwa viongozi wote. Namna tunavyotaka nchi iendeshwe
ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa
Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna
ile ile wanayohukumiwa watawala.
Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina
jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya
uanachama wangu.
Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio
wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine
wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa
upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha
operesheni tokomeza!

Maoni yangu.
Angekuwa mtu wa heshima na mnyenyekevu na mtii kwa viongozi wake sidhani kama angeweza kiandika ujumbe kama huo. Huyu dogo wangempiga chini tu hata chama.kikifa bora kuliko kukaa na kirusi mbaya kama huyu!
tulia tu ndugu yangu nakwambia hata juliana shonza mpaka dakika ya mwisho wanampiga chini alikuwa anasema kuwa yeye ni makamu mwenyekiti BAVICHA ...wewe ukitaka kujua jamaa anapenda ligi na ujuaji usiona maana cheki huu mstari...
Uwajibikaji sio msamiati kwa
watawala tu bali kwa viongozi wote. Namna tunavyotaka nchi iendeshwe
ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa
Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna
ile ile wanayohukumiwa watawala.
yawezekana hizi ni tuhuma za kweli lakini unaweza ona anavyozituma ..
maoni yangu muda unatuambia tu...
shida yangu mimi na zitto ni EGO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom