Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,743
Kama nionavyo chaguo la Mh.Zitto katika kamati ya kuchunguza iliyoundwa na Mh.Jakaya Kikwete hivi karibuni ni jambo la hatari ikiwa tu Zito ataweza kuitumia nafasi hiyo na kumwezesha kupata umaarufu maradufu ya aliokwisha jipatia.
Zito anaweza kucheza kama Kocha na wanakamati wote akawaburuza vile anavyotaka yeye,anaweza akafanya maamuzi ya mwisho kuwa ni yake na hakuna wa kuyapinga.
Hii ni karata au turufu ya Upinzani ambayo kama itatumika vizuri inaweza kuiangusha serikali ya Kikwete au kuiporomosha hapo ilipo,kwa maoni yangu Zitto asikae mpaka muda ukaisha ajitoe pengine baada ya mwezi mmoja tu ,sasa kitu ambacho kinahitajiwe akifanye ili aibuke na ushindi mwengine kwanza ni kuwachambua washiriki wa kamati hiyo ambao wote wanaonekana wapo katika kundi la mafisadi na wengine inasemekana wamehusika hadi kwenye utiaji saini kwa mantiki hiyo hawataweza kuhakikisha uchunguzi ni wa wazi na hautopendelea au kuwalinda wengine ikiwemo serikali,baada ya mwezi Zitto atakuwa ameshakusanya data za kutosha kuweza kubuni mbinu ya kuzitumia data hizo na kuziuza kwa wananchi kirahisi kabisa data ambazo zitampa nguvu ya kijuiengua katika kamati hiyo,natumai nimeeleweka nini afanye Zitto ili kuibuka mshindi.Kama kuna wengine wana uwezo wa kuelezea zaidi kwa kina nafasi ipo wazi ili kuwasaidia upinzani kuitumia nafasi hii aliyopata wenzao.
Na huku ndiko kufanya siasa,tunasikia huko ulaya chama kidogo kilichoshirikishwa kinaweza kujitoa na kuhatarisha uongozi mzima uliokuwepo,ila hapa kidogo naona upo ufanano.