Zitto ana hofu KUBWA: A fear of being ruled by a lesser.

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
Nimefuatilia sarakasi ambazo zinaendelea Chadema na kwa kiasi kikubwa nazidi kupata mawazo na mitazamo mipya kwa kadri siku zinavyokwenda kutokana na watu mbalimbali ambao ni viongozi na hata wanachama wa kawaida wa chama cha demokrasia na maendeleo wanavyozidi kufunguka juu ya maono yao na mtazamo wao halisi (si ule wa kufuta mkumbo) kuhusu uongozi wao wa juu na maamuzi yao na athari za maamuzi hayo ndani na nje ya Chama hiko.

Ndipo baada ya kutuliza akili yangu na kujikumbusha miongoni mwa yale ninayoyafahamu kuhusu migogoro, mgawanyiko na hofu za kiutawala, nikakumbuka andiko moja la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Upande wa Bara na Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Ndugu yangu Zitto Kabwe kuhusu hofu, hofu ambayo aliionesha waziwazi, hofu ya kuongozwa na watu dhaifu ,watu ambao hawana busara ya kutosha katika kufanya maamuzi na kuyasimamia.

Ndio kusema kwamba katika andiko lake hilo alitumia fasihi barabara katika kuwaambia watanzania kuwa yeye binafsi anahofu juu ya Viongozi wake ndani ya Chama hicho juu ya uwezo wao na busara zao za kufanya maamuzi. nitanukuu kipande cha andiko hilo hapa ili tupate mjadala makini.

THE FEAR.

Over the years, I have developed a habit of going to quiet places and reflect in solitary. This has become very important to me as I critically think and evaluate my ideas. Over and over, I find myself reflecting about my country and her future direction. I reflect on development, leadership, and politics of my country. This is mostly influenced and informed by my experience as a political leader, exposure to different places in the world, and readings. I have come to value readings and its impact on my personal development is invaluable. Previously, I used to read books that relate to politics, economics, or history. This has now changed. I have started reading novels, fictions, and philosophical books. This mixture of reading has further developed my thinking and the scope of my regular reflection.
Last week, while I was in Malaysia, I had more time to reflect. It was not easy. My reflection was haunted by fear. This fear was irresistable. Most likely, the fear was set-off by a passage I read in Tom Blake’s book titled ‘Doctor M: Operation Malaysia-Conversations with Mahathir Mohamad’. The passage, is quoted from Plato’s Republic, and it goes like this:
‘….but accepts the responsibility of ruling because he or she cares deeply about the Republic and the people in the Republic and only takes the job for fear of being ruled by a lesser’.
This was almost a turning point for me. It triggered an urge in me. The urge of fear. It made vivid many fears that, I believe, were overlooked and disappeared back into the subconscious mind of mine. This pumping fear on my chest overcame and deleted all the optimism I have had about my country. Previously I used to see only a rosy picture of Tanzania’s future. The fear helped me to see the reality and realised that the rosy picture was only an imagination and a wish at best.
I kept on reflecting and now the focus was on the fear. I asked myself, why fear? What is this fear about? I came up with two answers – the two fears. These fears are not mutually exclusive. They relate to each other.
Fear # 1: I fear about the leadership in my country. Plato’s Republic rightly noted the ‘fear of being ruled by a lesser’. Looking into the pool of people who position themselves to lead us in the near future was heartbreaking and scary. Not because many people are less smart or underprepared to run our country, but enormous challenges facing the country now subjects us to a thourough critical thinking about the country and developmental leadership. I fear about getting a leader who will be ‘lesser’. Lesser with regards to enormous tasks and need for wisdom to lead this big beautiful Tanzania into a prosperous future. We are faced by many challenges that can easily reduce someone to a ‘lesser’ if not wise enough. King Solomon asked for ‘wisdom to lead the great nation’. He was wise to know that the ‘big nation’ can easily make him ‘lesser’. He was not stupid but he realised that being ‘lesser’ is easy amidst challenges. We will need leaders who are ready to sit down, analyse the reality, and work hard. Leaders who would put selfish motives away and think of the nation. Who will not be influenced by party politics but people’s interests. A leader with a developmental mindset. Are Tanzanians wise enough to not choose a lesser?

Na swali hilo ambalo liko katika maandishi ya kijani ndilo swali la msingi ambalo watanzania hasa wanachama na wafuasi wa Chadema leo wanapaswa kujiuliza, kuwa busara zao zinawaongoza kupata kiongozi asiye dhaifu..???
 
CCM WAMEAMUA kutumia magazeti ya Chama na serikali kumkuza Zitto, lakini haogopwi mtu hapa!
Katika shughuli za kawaida zilizokipandisha chati chama, Zitto kashirikije, wakati unaambiwa hajakanyaga ofisini miezi kadha!
 
Kama alianza siasa akiwa na miaka 16 ajue kuna watu ndio waliomfikisha hapo. Kuwaona watu hao hawafai ni utoto na ujinga wa hali ya juu.
Mnafiki ni mnafiki tu, dhambi ya usaliti itamtafuna huyo kijana
 
Nimefuatilia sarakasi ambazo zinaendelea Chadema na kwa kiasi kikubwa nazidi kupata mawazo na mitazamo mipya kwa kadri siku zinavyokwenda kutokana na watu mbalimbali ambao ni viongozi na hata wanachama wa kawaida wa chama cha demokrasia na maendeleo wanavyozidi kufunguka juu ya maono yao na mtazamo wao halisi (si ule wa kufuta mkumbo) kuhusu uongozi wao wa juu na maamuzi yao na athari za maamuzi hayo ndani na nje ya Chama hiko.

Ndipo baada ya kutuliza akili yangu na kujikumbusha miongoni mwa yale ninayoyafahamu kuhusu migogoro, mgawanyiko na hofu za kiutawala, nikakumbuka andiko moja la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa Upande wa Bara na Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Ndugu yangu Zitto Kabwe kuhusu hofu, hofu ambayo aliionesha waziwazi, hofu ya kuongozwa na watu dhaifu ,watu ambao hawana busara ya kutosha katika kufanya maamuzi na kuyasimamia.

Ndio kusema kwamba katika andiko lake hilo alitumia fasihi barabara katika kuwaambia watanzania kuwa yeye binafsi anahofu juu ya Viongozi wake ndani ya Chama hicho juu ya uwezo wao na busara zao za kufanya maamuzi. nitanukuu kipande cha andiko hilo hapa ili tupate mjadala makini.

Na swali hilo ambalo liko katika maandishi ya kijani ndilo swali la msingi ambalo watanzania hasa wanachama na wafuasi wa Chadema leo wanapaswa kujiuliza, kuwa busara zao zinawaongoza kupata kiongozi asiye dhaifu..???

Kwanza ingependeza saana ungefahamu ,ZZK alianza kuonywa lini juu ya mienendo yake nje ya Chama..
Pili,yakupasa ujiridhishe kua ZZK amekua na mambo ambayo ni ya Kujikweza saana yeye kama yeye.. Mfano,alitangaza kua angegombea ubunge tofauti na Jimboni kwakwe (2010) kitu ambacho sijawahi kusikia Akaavha kutetea Jimbo akaenda kutafuta Jimbo jipya..
Tatu,Akiwa kama Naibu Katibu mkuu na anaijua vyema Katiba ya Chama chake,Alikiri Kuandaa Mswada huo mbele ya CC,na akijua vyema kua hilo ni kosa kikatiba,Wewe kwa mtazamo wako Ulitaka Chadema itoe Maamuzi yapi?
 
CCM WAMEAMUA kutumia magazeti ya Chama na serikali kumkuza Zitto, lakini haogopwi mtu hapa!
Katika shughuli za kawaida zilizokipandisha chati chama, Zitto kashirikije, wakati unaambiwa hajakanyaga ofisini miezi kadha!
Hapo kwenye red..
Kulivesha suala hili la mgogoro ndani ya CDM kuwa lina mkono wa CCM ni kulidogoisha na mwishowe kulitolea uamuzi ambapo hautakidhi haja na utaendelea kutunza ugonjwa mkubwa uliosababisha jambo hili kufikia hapa lilipofika.
Kuhusu ushiriki wa Zitto katika kuijenga Chadema nadhani wale graduate wa Mlimani na Duce katika miaka ya 2005 mpaka 2009 watakupa majibu kwa maana hakuna siku ambayo iliisha kabla ya Zitto kuwasiliana nao kimkakati, lakini to leave that aside ili nisionekane nambeba sana Zitto ni kweli kuna matukio ambayo yanatajwa kwa Zitto kutoshiriki likiwemo lile la kumpinga Mheshimiwa Rais na Kutoka nje ya Bunge, lakini kama ni mtu makini ukijiuliza impact ya matukio hayo kwa chama chenyewe na kwa jamii nadhani unaweza kukubaliana na Zitto kuwa yalikuwa matukio yanayoambatana na vitendo vya hovyo ambavyo havitoi taswira njema kwa watanzania.

Nadhani suala la mgogoro wa Chadema si magazeti ama wahariri ni viongozi wa Chadema kuja na matamko kila kukicha, nadhani kuwapakazia wanahabari sio sahihi nadhani njia sahihi ni viongozi wenu kucompromise na kuacha kushutumiana kwenye vyombo vya habari. Au mnataka wanahabari wasiandike habari zenu.??
 
Kama alianza siasa akiwa na miaka 16 ajue kuna watu ndio waliomfikisha hapo. Kuwaona watu hao hawafai ni utoto na ujinga wa hali ya juu.
Mnafiki ni mnafiki tu, dhambi ya usaliti itamtafuna huyo kijana
Yawezekana viongozi wa Chadema wapo katika makundi mawili ya watendao dhambi.,kuna wale watendao dhambi ya usaliti nao tunawaona kwa macho yetu kuwa dhambi hiyo inawatafuna ipasavyo.,lakini kubaliana na mimi kuwa kuna dhambi nyingine ya ubaguzi ambayo pia hufanywa na viongozi wa Chadema, na kwa faida yako na wasomaji wengine wa Comment hii ni kuwa dhambi zote mbili zinauzito mkubwa na athari mbaya katika taasisi yeyote ile. Lakini dhambi ambayo hata baba wa Taifa aliwahi kuitolea angalizo ni dhambi ya ubaguzi akasema nitamquote
mkianza dhambi ya kubaguana hamuachi..,itakuwa mfano wa mtu aliyeonja kula nyama za watu. HAACHI..!!!
Sijui chadema imejipangaje kukabiliana na Dhambi hiyo ambayo HAIACHIKI..,maana ya usaliti inaonyeka na huachwa pia.?
 
kwa vyovyote vile uamuzi wa kumtimua ZITTO chadema utakiumiza CCM, kuliko CHADEMA.

Kama cdm inania ya kweli kupeleka njaa na msiba wa kweli ccm basi hii ndo nafasi ya dhahabu iliyotokea kabla ya 2015, cdm isipofanya hivyo sasa itajiweka pagumu sana.

ZITTO amejengwa na kuwezeshwa kwa muda mrefu sana hata kufikia hapo, sasa huu ndo ulikuwa wakati wake wa kulipa fadhila kwa ccm.

tunachotaka ni chama imara na chenye mshikamano kitakacho itoa ccm madarakani, na kuonyesha +ve difference sio chama kilicho na lengo tu la kushika dola na kufanya unafiki na usaliti kama wa ccm.

ni vyema hao vijana wengine wanaojifanya wazalendo wakaondoka kwenye siasa ili wakasafishe fedha zao zisizo na maelezo wakiwa nje ya siasa, na wale ambao wanafuata watu badala ya sera ni vyema wakaanza kupitia mabuku yao ili wakumbuke kozi walizosoma vyuooni ili waanze kuandika application letters sehem mbalimbali, kwani hata muelekeo hawana bosi wao akisema siasa basi wengi watabaki njia panda
 
Kwanza ingependeza saana ungefahamu ,ZZK alianza kuonywa lini juu ya mienendo yake nje ya Chama..
Pili,yakupasa ujiridhishe kua ZZK amekua na mambo ambayo ni ya Kujikweza saana yeye kama yeye.. Mfano,alitangaza kua angegombea ubunge tofauti na Jimboni kwakwe (2010) kitu ambacho sijawahi kusikia Akaavha kutetea Jimbo akaenda kutafuta Jimbo jipya..
Tatu,Akiwa kama Naibu Katibu mkuu na anaijua vyema Katiba ya Chama chake,Alikiri Kuandaa Mswada huo mbele ya CC,na akijua vyema kua hilo ni kosa kikatiba,Wewe kwa mtazamo wako Ulitaka Chadema itoe Maamuzi yapi?

Unazungumzia Zitto kuonywa lakini hausemi moja kwa moja alikuwa anaonywa katika lipi..? nafikiri ungebainisha makosa ambayo zitto ameshawahi kuyafanya ndani ya Chadema kisha na hatua ambazo chama kilimchukulia katika kila kosa husika.

lakini kuhusu la muswada nadhani hauna taarifa sahihi za kinachoendelea ndan ya chama chako.,hakuna sehemu yeyote ambayo waraka unaozunguka katika vyombo vya habari unataja ama kuthibitika kuwa unatokana na Zitto bali ni waraka ulioandikwa na wapenda mabadiliko ya kweli ndani ya chama hiko wakiongozwa na Kitila Mkumbo ambapo walianisha makosa na udhaifu wa uongozi wa sasa ndani ya chama na pia kundi hilo chini ya Mkumbo wote walikubaliana kuwa Zitto anaweza kukiendesha na kukivusha Chama hiko na kwamba ndie chagua la wapenda mabadiliko hao.
 
Angeanza hiyo hofu kwa DHAIFU NAMBA MOJA Kikwete...

Kama amekubali kuongozwa na Dhaifu Kikwete na hasemi kitu, then ni unafiki mkubwa kuona udhaifu wa watu wengine
 
Back
Top Bottom