Zitto amwambia Makinda nipo tayari kuvua dagaa kijijini kwetu

- Uamuzi wa Mh. Zitto sio mbaya, lakini tatizo ni njia aliyotumia kuusema na kuutenda haiko sawa, kuna wabunge wengi vilema na wasojiweza sana kimaisha wanaohitaji hizo posho, njia aliyoitumia Zitto hai-justify the end! na infact in-defeat the whole good purpose aliyokuwa nayo!

- Hakukuwa na sababu za kui-politicize hiyo good act, sheria ni lazima apokee posho, HOWEVER: ni uamuzi wake namna ya kuitumia, angechukua na kuwapa wananchi bila kelele, angejijenga sana kisiasa kama the aim ilivyokuwa, maana ni wananchi ndio wangemtangaza how good he is, kuna ya kujipigia tarumbeta kisiasa, lakini this is not one of them katika nchi masikini kama yetu!

- Siungi mkono wabunge kutochukua posho zao, labda tuongelee kiwango, lakini sio kuchukua au kutochukua ni out of the line!

William @ NYC, USA.
hapo kwenye red mchungaji kapiga msumari hapa down
Fisadi hawezi jificha kwa kutumia hoja
saint naye kaongezea hapa
Saint Ivuga said:
Wataje hao wabunge tuwachangie pesa
 
- Well, neno halina maana tena kiongozi kupokea posho ya jasho lake sio ufisadi, Dr. slaa kupokea Shillingi Millioni saba kwa mwezi sio ufisadi!

Willie @ NYC, USA.

kaka mbona mnatoka nje ya topic?
Zitto hapingi kupokea posho, anachopinga ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi through the so called "Sitting Allowances". Kama unapata mshahara na per diem, kuna haja gani ya kupata sitting allowance on top of that?
 
bunge sio SACOS mkuu kama kuna wabunge vilema na wabunge vilema hawako bungeni kuwezeshwa kiuchu,u bali kutete maslahi ya umma.
kumbuka posho anayoongelea zitto ni zaidi ya wabunge lakini pia wabunge wanamisharaka minono kwa ajili ya ili jukumu lao
mbona sisi walala hoi hatupewe posho za kujikimu na hali ngumu ya maisha.

- Unajua sometimes hoja zingine zinasikitissha sana, hata kujibu inakuwa ni kaazi kweli kweli!, sasa unasema nini kwamba Serikali ianzishe tabia ya kulipa kila mwananchi hata kama hajafanya kazi? Mshahara wa wabunge wetu ni mkubwa kwa mfano gani au kulinganisha na wabunge wa wapi? Halafu Zitto amefanya utafiiti wa kisayansi na kuona wabunge wote wanaweza kuishi bila posho kama yeye?,

- Basi angeiweka hiyo research si unajua no research no right to speak! Haya ni mawazo ya kijamaa jamaa haya na Azimio la Arusha, yamepitwa sana na wakati!
- Huku US mkuu research zipo wazi kwamba Wabunge wote wa Senate ni Millioneas kwa hiyo it odes not matter kama wakipunguzwa mshahara kwa sababu hawahuhitaji, sasa Zitto angefanya haya ya utafiti na kuweka wazi uwezo wa wabunge wote na kwamba wasipolipwa hizo poshos wataishi bila tatizo, otherwise wabunge watakuwa wendawazimu sana kurukuia hii treni ya Zitto kwa mbele!

William @ NYC, USA.
 
Mkuu hapo kwenye red unaweza kutupa hicho kifungu kinachomlazimisha achukue posho? Kuna tofauti ya being entitled to posho na kulazimishwa kuchukua posho. Kama kuna sheria inayomlazimisha mbunge kuchukua poa, that law would be very absurd in deed. And what would be the punishment kwa kukataa hilo lazimisho? Nafikiri tunatafsiri vibaya ile barua ya katibu wa Bunge kwenda kwa Mh Zitto. Ile barua inasema kisheria pesa zinalipwa moja kwa moja kwa mbunge. Lakini haisemi ni lazima alipwe hizo pesa.

- Akikataa atafukuzwa bunge, wabunge wa Visiwani CUF walipogoma si waliambiwa wazi kwamba kisheria hawawezi kuchukua mshara wala posho na pia wakaishia kujifukuza bunge wenyewe au umesahau mkuu!

William @ NYC, USA.
 
kaka mbona mnatoka nje ya topic?
Zitto hapingi kupokea posho, anachopinga ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi through the so called "Sitting Allowances". Kama unapata mshahara na per diem, kuna haja gani ya kupata sitting allowance on top of that?

- What fact kutoka kwa Zito inayokufanya uamini kwamba mawazo ya Zitto yanawakilisha hali halisi ya maisha ya wabunge wote? Mambo mengine ni FACT OF LIFE!

William @ NYC, USA.
 
- Akikataa atafukuzwa bunge, wabunge wa Visiwani CUF walipogoma si waliambiwa wazi kwamba kisheria hawawezi kuchukua mshara wala posho na pia wakaishia kujifukuza bunge wenyewe au umesahau mkuu!

William @ NYC, USA.

Governor Schwazznnegger alikataa kupokea mshahara during his tenure, hakuna mtu alimlazimisha. Former governor of NJ naye pia alikataa mshahara. Mayor Bloomberg amekataa mshahara na hajafukuzwa umeya hapo mjini kwako. Sasa inakuwaje Zitto?
 
  • Thanks
Reactions: EMT

- Unasema Tanzania tunatumia sheria za US siku hizi au?

Willie @ NYC, USA.
 
- Uamuzi wa Mh. Zitto sio mbaya, lakini tatizo ni njia aliyotumia kuusema na kuutenda haiko sawa, kuna wabunge wengi vilema na wasojiweza sana kimaisha wanaohitaji hizo posho, njia aliyoitumia Zitto hai-justify the end! na infact in-defeat the whole good purpose aliyokuwa nayo!

- Hakukuwa na sababu za kui-politicize hiyo good act, sheria ni lazima apokee posho, HOWEVER: ni uamuzi wake namna ya kuitumia, angechukua na kuwapa wananchi bila kelele, angejijenga sana kisiasa kama the aim ilivyokuwa, maana ni wananchi ndio wangemtangaza how good he is, kuna ya kujipigia tarumbeta kisiasa, lakini this is not one of them katika nchi masikini kama yetu!

- Siungi mkono wabunge kutochukua posho zao, labda tuongelee kiwango, lakini sio kuchukua au kutochukua ni out of the line!

William @ NYC, USA.

Kwa kuwa kuna wabunge maskini na walemavu ndo wapewe posho ambazo hazina mantiki?

Wakati at least wao wanamshahara mkubwa na marupurupu mengine, wale maskini na walemavu mitaani wafanyeje?

Ni uzembe kutetea hoja kwa kutafuta kuonewa huruma
 
Tatizo ni kwamba hazitaki na huku anazitaka ,kwa maana kwamba anataka ziende kwenye mfuko wa maendeleo kigoma badala ya kubaki mfuko wa serikali. Zikienda kigoma maana yake amezichukua, na hapo naungana na spika kwamba azichukue halau azipeleke kigoma mwenyewe, kinyume chake fedha hizo aziache kwenye mfuko wa serikali.
 
- Under who's standards? Zitto's?

Willie @ NYC, USA.

Neville Meena, Dodoma
Mwananchi Tue 04/14/2011
HOJA ya kutaka kufutwa kwa posho za vikao za wabunge na watumishi wengine wa umma wa imechukua sura mpya baada ya jana Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba kuliambia Bunge mjini hapa kuwa suala la kufutwa kwa posho ni la kitaifa na ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali.Kauli hiyo yab Makamba ambaye pia ni Katibu wa Mambo ya Nje wa Sekretarieti ya CCM imekuja huku kukiwa na malumbano makali baina ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kuhusu suala hilo la posho za vikao vya wabunge.

Juzi, Spika Makinda alisema Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio, hatua ambayo Zitto alisema ataichukua ili asilipwe posho za vikao.

Spika alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinathibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vya bunge na kwamba kanuni zinamwadhibu mbunge kwa kumfukuza asipohudhuria mikutano mitatu. Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika kwa kusema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone, Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema.

Kauli ya jana ya Makamba pia inaonekana kutofautina na mawazo ya wabunge wengi wa CCM akiwamo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye amesema wanashabikia suala hilo wanajitafutia umaarufu.

Akichangia huo wa maendeleo wa miaka mitano jana, Makamba alionekana kupigia chapuo suala la kufutwa au kuangaliwa upya kwa posho za vikao huku akisema kwamba ni la kitaifa na ni sehemu ya mpango huo.

Makamba alisema kuwa suala la nidhamu na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma ni muhimu na kwamba mpango huo umeliona katika ukurasa wa 17 wa kitabu kilichochapishwa kwa Kiingereza na kutoa mapendekezo ya kufutwa kwa posho za vikao na zile za usafiri.

"Mpango unabainisha kwamba kuna umuhimu wa kufutwa kwa posho za vikao na usafiri hivyo iwapo wabunge mtalisikia likiwasilishwa hapa kwa mbwembwe kesho (leo), basi msije mkashangaa kwani ni sehemu ya mpango huu," alisema Makamba.

Haya sasa tuone Malecela v/s Makamba.......................................karibu Bronx nyuma ya Yankees Stadium!!
 
matusi na dharau ni kitu kibaya sana........madhumuni ya kuwa Ubunge/Uwakilishi yako wazi kabisa...........hii fani ya uwakilishi imegeuzwa kama kitega uchumi vile............element moja kubwa sana ya Uongozi ni Wito........mara nyingi viongozi wasio na wito ndio hufikiria kuganga njaa bungeni.........

Posho, Mishahara hujengwa kuzingatia mahitaji muhumu na ziada kiasi (debatable) kulingana na mazingira ya fani na hali halisi ya sehemu ya maisha husika................hivyo basi kuiita posho eti inawasaidia wabunge wasiojiweza na wenye shida za ulemavu........ina-defeat its purpose.........HAKUNA SEHEMU AMBAYO IMEANDIKWA KUWA POSHO NI KWA AJILI HIYO i.e. Ulemavu na wasiojiweza kimaisha............ulemavu/uwezo wa mtu kimaisha ni issue tofauti kabisa na posho ya uwakilishi/ubunge............

Kitendo cha Zito Kabwe kina pande mbili ambazo ni fact 1. Good Will and 2. Political Gain...............na kitendo chake kina mantiki kwa pande zote......i.e. deserve credit on both..........ni vigumu sana ku-undermine kitendo cha Zitto....the boy deserve a big round of applause..........

Iwe kwa yeye mwenyewe Zito kuchukua pesa na kupeleka kwenye foundation yake au kitendo alichokifanya......in my opinion....does not make any difference............Kijana Mo Dewji juzi "kawapiga" posho kila Mwl na 50K......na katoa pesa kibao kwa ajili ya Maji Jimboni mwake na sehemu nyingine kule Singida.......1. Good will...2.Political Gain...............Adv. Mkono same story......both deserve credit

However kitendo cha Zitto...kimekwenda beyond kutoa misaada to the needy.......kitendo chake kinazungumzia, kinatoa mwanga/Challenge kwenye discipline .......in spending of Public Fund..........which is a National disaster/dilemma/pandemic....ikiongozwa na Waheshimiwa Wabunge......
 
Zitto Muongo Mkubwa Umeshatajirika Kwa Pesa za Kifisadi, na zile ulizokomba katika Uenyekiti wa Kamati Kubwa ulioiongoza Bunge lililopita Mbona hujazirejesha, wacha siasa za Kitoto weee Watu Wanakuchekaaaaaaa

Fanya kura za haraka haraka humu JF, wangapi wanakubali na wangapi wanakataa. Utashangaa uko peke yako.
 
matusi na dharau ni kitu kibaya sana........madhumuni ya kuwa Ubunge/Uwakilishi yako wazi kabisa...........hii fani ya uwakilishi imegeuzwa kama kitega uchumi vile............element moja kubwa sana ya Uongozi ni Wito........mara nyingi viongozi wasio na wito ndio hufikiria kuganga njaa bungeni.........

Posho, Mishahara hujengwa kuzingatia mahitaji muhumu na ziada kiasi (debatable) kulingana na mazingira ya fani na hali halisi ya sehemu ya maisha husika................hivyo basi kuiita posho eti inawasaidia wabunge wasiojiweza na wenye shida za ulemavu........ina-defeat its purpose.........HAKUNA SEHEMU AMBAYO IMEANDIKWA KUWA POSHO NI KWA AJILI HIYO i.e. Ulemavu na wasiojiweza kimaisha............ulemavu/uwezo wa mtu kimaisha ni issue tofauti kabisa na posho ya uwakilishi/ubunge............

Kitendo cha Zito Kabwe kina pande mbili ambazo ni fact 1. Good Will and 2. Political Gain...............na kitendo chake kina mantiki kwa pande zote......i.e. deserve credit on both..........ni vigumu sana ku-undermine kitendo cha Zitto....the boy deserve a big round of applause..........

Iwe kwa yeye mwenyewe Zito kuchukua pesa na kupeleka kwenye foundation yake au kitendo alichokifanya......in my opinion....does not make any difference............Kijana Mo Dewji juzi "kawapiga" posho kila Mwl na 50K......na katoa pesa kibao kwa ajili ya Maji Jimboni mwake na sehemu nyingine kule Singida.......1. Good will...2.Political Gain...............Adv. Mkono same story......both deserve credit

However kitendo cha Zitto...kimekwenda beyond kutoa misaada to the needy.......kitendo chake kinazungumzia, kinatoa mwanga/Challenge kwenye discipline .......in spending of Public Fund..........which is a National disaster/dilemma/pandemic....ikiongozwa na Waheshimiwa Wabunge......
Good,but you can achieve both while your foundation(his,I mean) gets the money...now his foundation and himself are missing that money over some bull.
 
Walipomchagua Makinda kuwa Spika walidhani anauweza u-Spika. Makinda hauwezi, hajui kuchanganua hoja, wala hana uwezo wa kusoma alama za nyakati. Anachokifanya Zitto ni KAZI YAKE, kutetea maslahi ya Wananchi, akianzia na kule kijijini kwake, jimboni kwake walikomchagua, lakini akiwakilisha maoni na wananchi wote hapa nchini.

Iweje mtu anayetetea maslahi ya nchi, maendeleo ya wananchi, mbele ya Spika, aonekane ADUI? Sijawahi kusikia ati mtu anafukuzwa Ubunge kwa kukataa kupokea posho yake? Si ni "yake"? Akikataa, akikubali, nini kinaharibika?

Makinda, yaonekana wewe bado ni kinda katika kazi. Kaa chini, jifunze ku-negotiate, jifunze kutetea hoja za wananchi, wewe si DIKTETA! Utaishia pabaya, utamwumbua hata Rais wako, maana sasa unayoyafanya, inaelekea kwamba Rais amekutuma ukatae hoja ya msingi kabisa, kwamba, ati Serikali inatetea matumizi mabaya ya pesa za wananchi, kwani, hizo posho zinatokana (kimsingi) na kodi za wananchi pamoja na misaada toka kwa wafadhili. Makinda, unatuthibitishia kwamba Serikali haipo kwa ajili ya wananchi, kwani anachokifanya Zitto ni kutaka "maisha bora kwa kila Mtanzania", sera ya Rais Kikwete, ila yeye anaitekeleza kwa vitendo, si katika nadharia kama utakavyo wewe. Makinda unathibitisha unafiki wa Serikali unayoitetea, kwamba, hata wabunge wakijaribu kufanya kazi yao, watazuiwa tu, kwani HAKUKUWA NA NIA wala DHIMA ya kutimiza mipango madhubuti pamoja na Sera za Chama Tawala katika kumkomboa Mtanzania na lindi la UMASKINI, tena umaskini WA KUJITAKIA!

Sijawahi kuona mtu anaadhibiwa kwa kuitakia mema nchi yake. Ama kweli, Nabii hakubaliki kwao!

UMELIKOROGA Makinda! UMELIKOROGA kweli! Duuuuuh! Haya, mfukuze basi huo ubunge, kwani wewe si ndiye ULIYEMCHAGUA Zitto? Tuone kitakachojiri. Utaweza?

./Mwana wa Haki
 
MImi nadhani kuna mambo ya msingi hapa. Lakini kitu kimoja kinanipa mashaka ni wapi watanzania? Mbona hatutengenezi movement (vuguvugu) kubwa kudai mapitio ya utaratibu huu? Mbona suala hili linaonekana miongoni mwa wabunge wengi kuwa la kisiasa zaidi kuliko la uwajibikaji, haki ya watazania na kiuchumi zaidi? Ni nani anaweza kuwa-mobilize na kuhamasisha watanzania wengi waka-stage maandamano (yasiyoratibiwa na viongozi wa siasa) kudai moratorium kwa utaratibu huu wa ajabu? Sitting allowance???? Tanzania nchi yangu! Watanzania tuko wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom