Zitto amuomba msanii Nikki wa Pili aingie kwenye siasa

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Zitto anaamini msanii wa Hip hop nchini kutoka Arusha, Nikki wa Pili ana maono ya masuala mbalimbali hivyo angefaa kushiriki kwenye siasa.

Mbunge huyo wa Kigoma, baada ya kusoma maoni binafsi aliyoandika msanii huyo kuhusu masuala ya uchaguzi, amemsihi aingie kwenye siasa ili asaidie kujaza ombwe la maono lililopo miongoni mwa wanasiasa nchini..

Je, Zitto anahitaji wanachama wapya wenye nguvu na ushawishi kwenye chama chake cha ACT-Wazalendo?!

Msome;

"Siasa zetu zinakosa wanasiasa wenye convictions ( sijui Kiswahili chake) kwa sababu watu kama wewe mwenye misimamo ya kiitikadi hamtaki kujiunga na vyama. Njoo tufanye kazi ngumu Lakini muhimu ya kujenga siasa zinazoondoa uhodhi kwa wanasiasa.."

nikk.jpg
 
Shauri yake nikki

asije ambiwa nyimbo zake ni za uchochezi, siyo mtz, kulala polisi kila leo, mkwepaji kodi, fisadi, anatembea na wanafunzi, alifeli shule, na mengineyo

kama atayaweza haya basi ajitose tu
 
Wanasiasa bana huyo Nikki mwenyewe kakosea kuandika lakini ndo kaona anafaa kuwa anafaa kuwa mwanasiasa kweli siasa Ni ujinga
 
Niki wapili siasa haziwezi bora hata angekua niki mbishi angalau niki wapili ni miongoni mwa vijana ambao hawezi kusimamia anachokihamini
 
Sidhani kama Nikki amejiunga na chama chochote, lakini leo hii ameingia kwenye siasa za uongozi baada ya kuteuliwa kuwa DC wa Kisarawe. Mambo ya muda haya.
 
Back
Top Bottom