Zitto amtaka Waziri Mkullo apishe uchunguzi - Taarifa kwa vyombo vya habari

Maisha ya bongo ni noma kishenzi maana hawa watu wa Tazania ni viongozi wa kifalme juha sana , ZIIIIIIIIIIIIITOOOOOOOOOOOO tia kibeririti hao ili tuone jeuri yao hapa mjini
 
Wakimbizi wanaotutesa.
1. Mustapha mkullo
2. Joseph mungai
3. Rostam aziz
4. Daud balali
5. Jeetu patel
6.kINANA
7. Idd Simba
8
9
Mkuu hapo kuna mtu umemsahau # 8 HUSSEIN BASHE # 9 Yule Mbunge aliyepanda jukwaani na BASTOLA kwenye kampeni.
 
This is what I expected Zitto to do... scrutunising the malfunctions za Hazina na sio kufanya kazi za shadow minister wa wizara zingine. Hazina ina matatizo makubwa sana na sijui Mkullo anaweza kusema anafanya nini kuhusu kushuka kwa thamani ya Shillingi yetu.
 
KUNA HAWA WENGINE
waziri wa nishati(ngeleja)
msinziaji hodari(wasira)
lukuvi
.
.
.
.
etc
 
mkulo hana data hata kama nchi yetu inapolomoka thamani ya fedha yake,yeye anachojua ni kwamba uchumi unapaaaaaa kwa kasi
 
Kabwe ZuberiZitto, Mb



WaziriKivuli wa Fedha na Uchumi




TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI




Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo akae pembeni kupishauchunguzi dhidi yake kuhusu Shirika la CHC.
Katika Mkutano wa Nne waBunge la Kumi kulitokea malumbano makali kati ya Serikali na Wabunge wajumbe wa Kamati yaHesabu za Mashirika ya Umma kuhusu kuongezwa muda wa Shirika la CHC. WakatiWaziri wa Fedha alileta Azimio la kulivunja Shirika hili lenye taarifa nyingina nyeti kuhusu zoezi la Ubinafsishaji, Kamati ya Bunge ya POAC kutokana nauzoefu wake wa kukagua mahesabu ya Mashirika ya Umma na kufuatilia zoezi laUbinafsishaji wa Mashirika ya Umma, ilipinga hatua hii na kulitaka Bungekukataa Azimio la Serikali na kulifanyia marekebisho makubwa. Hatimaye Bungeliliridhia kufanya mabadiliko makubwa katika Azimio la CHC, kwa kuamuru Shirikalipewe uhai wa miaka 3 na kuagiza uchunguzi wa namna bora ya kuendesha shughuliza Shirika la Consolidated Holdings. Mapendekezo ya Kamati ya POAC ni kulifanyaShirika hili kuwa la kudumu na kulipa jukumu la kumiliki na kusimamia uwekezajiwa Serikali kwenye kampuni binafsi (National Investment Agency) kama ilivyo Shirikala Tamasek ya Singapore na Shirika la Khazana ya Malaysia. Kwa sasa Uwekezajiwa Serikali katika Kampuni binafsi unasimamiwa na Hazina na usimamizi wake nimbovu na hauleti tija kwa Taifa.

Kitendo cha kushindwa kwahoja Bungeni kiliifedhesha Serikali na hivyo kwa kupitia Wizara ya Fedha kuamuakulihujumu Shirika kwa kumsimamisha Mkurugenzi wake Mkuu kwa makosa ya kimajungumajunguna kwa kuzusha kwamba CHC iliwahonga wabunge ili kuitetea. Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo alilitaarifuBunge kuwa Bodi ya CHC imeomba ukaguzi maalumu kuhusu tuhuma za ubadhirifundani ya Shirika hilo. Niliitaka Serikali ichunguze pia tuhuma kwamba Kamati yaPOAC ilihongwa na kuahidi kuahidi kujiuzulu nyadhifa zangu zote ikithibitika.

Katika Uchunguzi wakeMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heabu za Serikali kwa kupitia Kampuni ya Ernest andYoung walitaka kufanya mahojiano na Waziri wa Fedha juu ya tuhuma mbalimbalizinazomkabili ndani ya CHC. Waziri Mkulo alikataa kuhojiwa na wakaguzi nabadala yake akaandika barua (kumb TYC/B/70/2/03 ya Oktoba 8, 2011) yenye kujibutuhuma moja, tena kwa juu juu, kuhusu yeye kuliamuru Shirika kuuza kiwanja cha Shirikabila kufuata taratibu za sheria. Wakati Waziri anakanusha kuliagiza Shirikakuuza kiwanja kwa mtu aliyemtaka yeye, mimi nina ushahidi tosha wa Nyarakakutoka Hazina, kwa mfano barua TYC/A/290/13/4 ya Machi 9, 2011 ambayo inawagizaCHC kutekeleza agizo la Waziri la Fedha kuhusu kiwanja na. 10 barabara yaNyerere. Vilevile, nina ushahidi wa mkutano uliofanyika huko Morogoro Hotelkati ya Waziri wa Fedha na Mwenyekiti wa Bodi ya CHC kuhusu jambo hilo.

Siku mbili baada yakumjibu CAG, Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo aliamua kutengua uamuzi wakewa kuongeza muda wa Bodi ya Shirika la CHC mpaka mwezi Disemba 2011 na hivyokuivunja. Uamuzi huu wa Waziri una lengo la kuficha ukweli kwani CHC bila Bodiya Wakurugenzi inaendeshwa na Hazina na hivyo taarifa ya ukaguzi itabidiipelekwe Hazina ambayo Waziri wake ni mtuhumiwa.

Uchunguzi wa kina
Ninapendekeza uchunguzi wakina ufanyike kwa kutumia vyombo vya dola na hasa TAKUKURU kuhusu tuhuma hizidhidi ya Waziri wa Fedha na alazimishwe kisheria kujibu maswali ya wakaguzi (Auditors) kuhusu tuhuma dhidi yake.

Wakati uchunguziunaendelea ndugu Mustafa Mkuloasimamishwe kazi ya Uwaziri wa Fedha hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.Kitendo chake cha kuiamuru Bodi kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kwatuhuma za kutunga na majungu na baadaye kuvunja Bodi ya CHC wakati inasubiritaarifa ya uchunguzi kutoka kwa CAG ni kuingilia uchunguzi na pia ni matumizimabaya ya Ofisi ya Umma ili kulinda maslahi binafsi. Ni dhahiri akiendelea kuwaWaziri wa Fedha ataharibu uchunguzi.Vilevile, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete aangalie kama anaitendea haki nchina Uchumi wa nchi kwa kuwa na Waziri wa Fedha ambaye anasema uwongo Bungenibila kuogopa na mwenye kutumia Ofisi yake vibaya kwa kuchukua maamuziyanayoingilia uchunguzi unaomhusu ili kujilinda.

Taarifa ya Uchunguzi ikabidhiwe kwa Spika
Kutokana na ukweli kwambasuala la CHC lilianzia Bungeni na hata Waziri mwenyewe kukiri kuwa taarifa yauchunguzi inapaswa kuwekwa wazi. Kutokana na matokeo ya sasa ambapo Waziri waFedha mwenyewe ana tuhuma za kujibu na kwamba hivi sasa hakuna Bodi yaWakurugenzi ya Shirika na hata itakayoundwa itateuliwa na Waziri mtuhumiwaninashauri kuwa taarifa ya uchunguzi wa Shirika la CHC sasa ipelekwe kwa Spikawa Bunge kwa hatua zaidi.

KZZ
Dar es Salaam, 13 Oktoba,2011.
wewe ni rais wetu wa 2020
 
Kama mambo yenyewe ni haya na viongozi wenyewe tulionao Serikalini kila mmoja ni mmbovu,nnadhani mpaka ifike 2015 hali ya uchumi Wa nchi yetu hii itakuwa mbaya sana.
 
kichwa cha nazi ya bagamoyo kinapochagua maembe ya morogoro
Hahaaaaaaaaa....... Mkuu unakumbuka siku ile wakati wa kikao cha Bunge kujadili Budget ya Wizara ya Ulinzi, Huyu Mkullo aliwatisha Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowaambia kwamba

" Msipopitisha Budget hii ya Wizara Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa humu Bungeni hapatakalika" hakuna hata Mbunge mmoja aliyeomba mwongozo kukemea kauli hiyo. Kuna tetesi kwamba pale kwenye Wizara ya Mkullo kuna Mke wa wapiga SALUTE wakuu Duniani, ndiyo maana anajawa na kiburi anafanya kila atakalo kwa sababu hakuna wa kumgusa.

Japokuwa inasemekana kuwa ni mtu wa MALAWI. Ngoja tuone hii issue, kwa JK itakuwa ni sawa na kuzima umeme kwa kupuliza balbu kwa mdomo.
 
Hii ngoma ingekuwa Kenya kwa Mzee Kibaki yaani by the time Mhe Zito anamaliza kusoma ripoti yake Mkulo hana kazi
 
[h=6]WOTE wanatuhuma za UPORAJI MALI ZA umma mafisadi PAPA ninani atamwajibisha mwenzake SHERIA YA kunyonga mafisadi kama china NDIO inayo weza kupunguza na kumaliza umasikini TANZANIA!! (BENJAMIN mkapa ENDREW chenge GREY mgonja RAJAB maranda FARIJALA maranda BAZIL mramba NAZIL karamagi IBRAHIM msabaha ROSTAM ziz EDWARD lowasa BAZIL mrindoko EDWARD hosea DAUDI balali JEETU patel YUSUPH manji ZAKIA megji LAWRENCE masha WILIAM ngereja PIUS msekwa!!) jakaya KIKWETE mustapha MKULO ezekieli MAIGE!!......SHERIA YA KUNYONGA WAHUJUMU UCHUMI itapunguza na kumaliza kabisa tatizo la umasikini TANZANIA!![/h]
 
mkulo hatufai hatutaki viongozi wababaishaji,wahongo na vigeugeu,ondoka tumekuchoka
 
Tujifunze kuwa na subira hizo ni tuhuma tuchangie zaidi asimamishwe nafasi ya uwaziri halafu tupime matokeo ya ripoti ya uchunguzi ndipo tuanze kusema kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uchunguzi uliofanyika
 
yeees!!!!!! well done Zitto. Tanzania inauona mchango wako. keep it up.hakuna kulala...................
 
Viongozi wa Tanzania hawapo tayari kirahisi rahisi kuachia madaraka
Wajifunze Uganda hapo
 
This is what I expected Zitto to do... scutunising the malfunctions za Hazina na sio kufanya kazi za shadow minister wa wizara zinginge. Hazina ina matatizo makubwa sana na sijui Mkullo anaweza kusema anafanya nini kuhusu kushuka kwa thamani ya Shillingi yetu.

Huu ni uthibitisho mwingine kwamba mkulo hana uwezo wa kuongoza wizara ya fedha. Kimsingi hastahili hata kuwa naibu waziri.

Binafsi nakubaliana na msemakweli kuhusu tuhuma za mkulo kuwa shule hakuna amefoji vyeti tu na kumsaidia kubebwa hadi kufika hapo alipo.

Haiwezekani mtu mwenye elimu yake aache nchi inaingia kwenye crisis huku akifanya jitihada za kuhujumu shirika na mali ya umma badala ya kufanya jitihada za kuuinua uchumi wetu.
 
tujifunze kuwa na subira hizo ni tuhuma tuchangie zaidi asimamishwe nafasi ya uwaziri halafu tupime matokeo ya ripoti ya uchunguzi ndipo tuanze kusema kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uchunguzi uliofanyika

Mkuu inawezekana una macho ya kinyonga, lakini wengine tunapata shida na hii rangi unayotumia.
 
Back
Top Bottom