Zitto amtaka Waziri Mkullo apishe uchunguzi - Taarifa kwa vyombo vya habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto amtaka Waziri Mkullo apishe uchunguzi - Taarifa kwa vyombo vya habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Oct 13, 2011.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Kabwe Zuberi Zitto, Mb

  WaziriKivuli wa Fedha na Uchumi  TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI

  Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo akae pembeni kupishauchunguzi dhidi yake kuhusu Shirika la CHC.

  Katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi kulitokea malumbano makali kati ya Serikali na Wabunge wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma kuhusu kuongezwa muda wa Shirika la CHC. Wakati Waziri wa Fedha alileta Azimio la kulivunja Shirika hili lenye taarifa nyingi na nyeti kuhusu zoezi la Ubinafsishaji, Kamati ya Bunge ya POAC kutokana na uzoefu wake wa kukagua mahesabu ya Mashirika ya Umma na kufuatilia zoezi la Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma, ilipinga hatua hii na kulitaka Bunge kukataa Azimio la Serikali na kulifanyia marekebisho makubwa.

  Hatimaye Bunge liliridhia kufanya mabadiliko makubwa katika Azimio la CHC, kwa kuamuru Shirika lipewe uhai wa miaka 3 na kuagiza uchunguzi wa namna bora ya kuendesha shughuliza Shirika la Consolidated Holdings. Mapendekezo ya Kamati ya POAC ni kulifanya Shirika hili kuwa la kudumu na kulipa jukumu la kumiliki na kusimamia uwekezaji wa Serikali kwenye kampuni binafsi (National Investment Agency) kama ilivyo Shirikala Tamasek ya Singapore na Shirika la Khazana ya Malaysia. Kwa sasa Uwekezajiwa Serikali katika Kampuni binafsi unasimamiwa na Hazina na usimamizi wake nimbovu na hauleti tija kwa Taifa.

  Kitendo cha kushindwa kwa hoja Bungeni kiliifedhesha Serikali na hivyo kwa kupitia Wizara ya Fedha kuamua kulihujumu Shirika kwa kumsimamisha Mkurugenzi wake Mkuu kwa makosa ya kimajungumajungu na kwa kuzusha kwamba CHC iliwahonga wabunge ili kuitetea. Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo alilitaarifu Bunge kuwa Bodi ya CHC imeomba ukaguzi maalumu kuhusu tuhuma za ubadhirifu ndani ya Shirika hilo. Niliitaka Serikali ichunguze pia tuhuma kwamba Kamati ya POAC ilihongwa na kuahidi kuahidi kujiuzulu nyadhifa zangu zote ikithibitika.

  Katika Uchunguzi wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heabu za Serikali kwa kupitia Kampuni ya Ernest and Young walitaka kufanya mahojiano na Waziri wa Fedha juu ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili ndani ya CHC. Waziri Mkulo alikataa kuhojiwa na wakaguzi na badala yake akaandika barua (kumb TYC/B/70/2/03 ya Oktoba 8, 2011) yenye kujibu tuhuma moja, tena kwa juu juu, kuhusu yeye kuliamuru Shirika kuuza kiwanja cha Shirika bila kufuata taratibu za sheria.

  Wakati Waziri anakanusha kuliagiza Shirika kuuza kiwanja kwa mtu aliyemtaka yeye, mimi nina ushahidi tosha wa Nyaraka kutoka Hazina, kwa mfano barua TYC/A/290/13/4 ya Machi 9, 2011 ambayo inawagiza CHC kutekeleza agizo la Waziri la Fedha kuhusu kiwanja na. 10 barabara ya Nyerere. Vilevile, nina ushahidi wa mkutano uliofanyika huko Morogoro Hotel kati ya Waziri wa Fedha na Mwenyekiti wa Bodi ya CHC kuhusu jambo hilo.

  Siku mbili baada ya kumjibu CAG, Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo aliamua kutengua uamuzi wake wa kuongeza muda wa Bodi ya Shirika la CHC mpaka mwezi Disemba 2011 na hivyo kuivunja. Uamuzi huu wa Waziri una lengo la kuficha ukweli kwani CHC bila Bodi ya Wakurugenzi inaendeshwa na Hazina na hivyo taarifa ya ukaguzi itabidi ipelekwe Hazina ambayo Waziri wake ni mtuhumiwa.

  Uchunguzi wa kina
  Ninapendekeza uchunguzi wa kina ufanyike kwa kutumia vyombo vya dola na hasa TAKUKURU kuhusu tuhuma hizi dhidi ya Waziri wa Fedha na alazimishwe kisheria kujibu maswali ya wakaguzi (Auditors) kuhusu tuhuma dhidi yake.

  Wakati uchunguzi unaendelea ndugu Mustafa Mkuloasimamishwe kazi ya Uwaziri wa Fedha hadi hapo uchunguzi utakapokamilika. Kitendo chake cha kuiamuru Bodi kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kwa tuhuma za kutunga na majungu na baadaye kuvunja Bodi ya CHC wakati inasubiri taarifa ya uchunguzi kutoka kwa CAG ni kuingilia uchunguzi na pia ni matumizi mabaya ya Ofisi ya Umma ili kulinda maslahi binafsi.

  Ni dhahiri akiendelea kuwa Waziri wa Fedha ataharibu uchunguzi.
  Vilevile, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete aangalie kama anaitendea haki nchi na Uchumi wa nchi kwa kuwa na Waziri wa Fedha ambaye anasema uwongo Bungeni bila kuogopa na mwenye kutumia Ofisi yake vibaya kwa kuchukua maamuzi yanayoingilia uchunguzi unaomhusu ili kujilinda.

  Taarifa ya Uchunguzi ikabidhiwe kwa Spika
  Kutokana na ukweli kwambasuala la CHC lilianzia Bungeni na hata Waziri mwenyewe kukiri kuwa taarifa ya uchunguzi inapaswa kuwekwa wazi. Kutokana na matokeo ya sasa ambapo Waziri wa Fedha mwenyewe ana tuhuma za kujibu na kwamba hivi sasa hakuna Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika na hata itakayoundwa itateuliwa na Waziri mtuhumiwa ninashauri kuwa taarifa ya uchunguzi wa Shirika la CHC sasa ipelekwe kwa Spika wa Bunge kwa hatua zaidi.

  Kabwe Zuberi Zitto,
  Dar es Salaam, 13 Oktoba,2011.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  viongozi mbona tunao wengi tu sema ndiyo hivyo wanafumbiwa macho kwakuwa wako upinzani, kwani upinzani si watanzania, sasa JK sijui atasemaje patamu sana hapa.
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Chadema na angle nyingine,hii ndio shule hii ndiyo Tanzania inakotakiwa kwenda,kuna kawimbo kazuri sana ka kizalendo kanasema "vijana msilalela ee lalelale vijana msilale bado mapambano"taratibu mpka kwenye kona.
   
 4. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kijana fanya kazi ulitetee taifa lako. Tuko pamoja na wewe. Mungu akuwezeshe kwenye hii vita dhidi ya ufisadi
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkulo kalikoroga kitendo cha kuvunja bodi kinyemela kinadhihirisha kuna jambo limejificha nyuma yake. Ningelikuwa JK hiyo ni sababu tosha ya kumtaarifa mkulo aachie ngazi kwani tayari ameshajitia kitanzini. Inanikumbusha hadithi ya mama Meghji na barua ya Balali!!!Kazi nzuri Zitto wacha tuangalie JK atafanya nini!
   
 6. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutafika tu, wakifunika hili linafunuka lile, Kazi kwelikweli!!
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kijana akaze uzi na aseme tu
  Hii ndo serikali ya wezi wa raslimali zetu
  Mpaka kieleweke
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Masikitiko makubwa kwa watanzania ni kwamba pamoja na uozo wote anaofanya mkulo, raisi Kikwete atanyamaza as if hajui wala hakusikia kinachoendelea kati ya CHC na waziri mkulo. Atanyamaza kimya na mkulo ataendelea na nafasi yake ya uwaziri na hatimaye ataharibu ushahidi na kujinasua na kadhia hii.

  Hapa ndipo huwa tunatamani rais Kikwete atumie mamlaka yake japo kidogo tu, kuonyesha wananchi kwamba yuko kwa maslahi yao, lakini wapi bwana hili nalo litapita hivi hivi!
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kazi nzuri mh.Zitto

  Huyu mkulo tangu amekuwa waziri wa fedha tumeshuhudia hali ngumu sana ya maisha. Bei ya bidhaa inapanda kila kukicha, mishahara ya wafanyakazi wa serikali inachelewa isivyo kawaida na kubwa kuliko vyote miradi mingi ya maendeleo kama si yote imesimama kama si kufa kabisa kwa kukosa fedha.

  Kuna taarifa kwamba pamoja na kwamba bajeti ya serikali imepitishwa tangu mwezi wa sita, takriban miezi minne sasa bado taasisi na idara za serikali hazijapokea mafungu yao, hivyo kusababisha shughuli nyingi za kimaendeleo kukwama. Mkulo asipotimuliwa wizara ya fedha tujue tunapalilia janga la kitaifa.
   
 10. K

  Kyoombe JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 653
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Safi sana Kabwe. Hii ya sasa sijui watatokea mlango upi. Endeleza mapambano dhidi ya hao mafisadi.
   
 11. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ni SAHIHI kabisa,we ngoja uone,litazimwa ki style ileile ya jairo,yaani huyu rais wetu sijui yukoje,yupoyupo tu,wizara zina maovu kibao lakini yeye yupo kimya tu,mi nadhani yeye ndo anakua kawatuma kufanya hayo ndio maana anakua mzito kutake action..Solution ni kumuondoa kwa maandamo(NGUVU YA UMA) ili aje mwenye msimamo na uchungu kwa nchi na wananchi kwa ujumla
   
 12. Tshala

  Tshala JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Good job Zito! Haya sasa mmetafuniwa mezeni....
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tanzania hakuna utaratibu wa kujiuzulu kupisha uchunguzi
   
 14. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo humu tunawaamini wageni kupita kiasi, mpaka tunawapa wizara watawale. Huyu MKULO si mmalawi huyu?
  Ndo maana analeta ishu za ki-mutharika hapa anajali tumbo lake na maslahi yetu kama taifa anayaweka kapun.
  Timua mkimbizi huyu.
   
 15. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Umasikini mwingine tunajitakia waafrika kwa kukumbatia viongozi aina ya Mkulo.
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi sitasema hadi hawa nioe michango yao

  Ritz
  Faiza Foxy
  Mbopo
  Mwita25
  Ongezeni wengine hapa wakisha timia tuanze mjadala .
   
 17. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa Zitto Zubery Kabwe, pongezi kutoka moyoni mwangu. Kazi nzuri saaana. This is true reflection of what you learned.
   
 18. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakimbizi wanaotutesa.
  1. Mustapha mkullo
  2. Joseph mungai
  3. Rostam aziz
  4. Daud balali
  5. Jeetu patel
  6.
  7.
  8.
  Et al
   
 19. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo yetu macho, Mkulo ni mbabaishaji sana huwa sina imani na yeye kabisa any way NDOYO CCM ya NAPE wa magamba
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,129
  Likes Received: 6,617
  Trophy Points: 280
  Kwa hili zito hata mimi nimekukubali mkuu.
   
Loading...