Zitto: Amri ya Rais Magufuli kuhusu 'Mchanga wa Dhahabu' imepotezea nchi Tshs 1.8 Trilioni Capital Gains Tax

Kazi ya upinzani sasa ni kutetea maovu. Leo hii wapinzani wanataka wazungu waendelee kutuibia ili tu kuonesha Magufuli hawezi? Kwa kweli huu upinzani umekuwa kituko na hauna maslahi kwa nchi yetu maana haupo kusapoti maendeleo bali kukwamisha maendeleo.

Wapi katetea uovu? Ajatoa solutions hapo? Kasema asingezuia leo hii tungepata pesa ya kutengeneza icho kinu. Je hapo kuna uovu wowote uliotetewa?
 
Naona kama zito anatumika tu apa. Kama aliunga mkono lile tamko mara ya kwanza..leo ameanza kuligeuka tena? Mwambieni tu awamu hii atakamatwa kweupe nawanaomhonga ili kufikisha haja zao. Kama serikali imepiteza 1.8 tn..how comes mapato kwa mwezi yanaishia 1.2 trn. Huu ni upuuzi mwingine Zitto anatuletea. 2020 itabd apotee tu kwenye uongozi wa kitaifa. Hajitambui mpuuzi yule.
 
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni.
Swali langu la kwanza
  • Una uhakika kiasi gani kuwa mkataba wa mauzo kati ya Acacia na huyo mnunuzi ulikuwa lazima utimie ndani ya hiyo wiki moja hadi useme iwapo Raisi angechelewa kutoa kauli yake kwa wiki moja basi mkataba ungekuwa umesainiwa?
 
kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha
Mhe MP,Nakuombeni msilihusishe Azimio la Arusha na siasa za Tanzania, sio sahihi na ni kosa. Azimio la Arusha sio tu kama limekataliwa Zanzibar lakini lipigwa marufuku na SMZ na Muasisi mkuu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Sheikh Abeid Karume.
Alisema, kuwambiwa wananchi wa Zanzibar,tena kwenye mkutano wa Hadhara kuwa Azimio la Arusha ni marufuku Zanzibar na kama litalazimishwa basi mwisho Chumbe( kisiwa kidogo, ambacho hakikaliwi na watu karibu na Zanzibar
1.Hayati Karume ndio baba wa Taifa la Zanzibar pekee tunayomtambua
2.Tumeapa kuenzi fikira, mawazo, busara zake na kilichokufa ni kiwiliwili tu.
3.Wazanzibari kindakindaki ni waislamu na Azimio hilo la Arusha linaendana kinyume na matakwa ya Kiislamu,lazima Muislamu anatakiwa kujenga Khatima yake na jamaa(ali) zake wakati wa uhai wake, jambo linalopingana na Azimio hili batili.

Kuiburuza Zanzibar kwenye jinamizi la Azimio la Arusha ni sawa kutuuumbea tukose radhi za baba wa Taifa letu na mungu wetu tunae muamini.

Kumradhi mheshimiwa.
 
Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining.

Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali.

Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni.

Tafiti zinaonyesha kuwa gharama ya kujenga ' refinery ' ya kuchenjua dhahabu hapa nchini ni USD 800m. Hivyo mapato ambayo yangepatikana kutokana na kodi ya mauzo ya Acacia yangewezesha nchi kujenga refinery na kufikia lengo la Rais la kuwa na uchenjuaji wa mchanga ule hapa hapa nchini. Rais angetulia angeweza kuua ndege wawili Kwa jiwe moja, 1) kiwanda cha kuchenjua kingejengwa nchini na 2) mchanga usingesafirishwa tena kwenda China na Japan.

Hata hivyo Tanzania haina mchanga wa kutosha wa kushibisha hiyo refinery Kwa mujibu wa teknolojia ya sasa ( soma maelezo yangu hapa chini Kwa Mhariri wa RaiaMwema). Hivyo Rais angeweza kutumia mapato hayo Kwa matumizi mengine ya Maendeleo. Kwa mfano Bunge lilitenga kama USD 430m hivi kujenga Reli ya kisasa na tayari Serikali imeshaingia mkataba na kampuni kutoka Uturuki kujenga Reli hiyo kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro. Lakini gharama ya kipande hicho ni USD 1.2bn. Kwahiyo Rais angeweza kutumia mapato haya ya mauzo ya Acacia kuongezea kwenye kipande hiki na hivyo kuepuka kukopa kuziba nakisi ya USD 800m iliyopo Sasa na Bunge kwenye Bajeti ya 2017/18 lingetenga fedha za kuanzia Morogoro kwenda Dodoma.

Kama Mipango ya Reli ipo sawa, Rais angeweza kutumia fedha za capital gains tax kutoka Acacia kujenga vyuo vya VETA kila Wilaya na kila Kambi ya JKT na chenji ingebaki. Tanzania inahitaji tshs 750 bilioni kujenga vyuo vya VETA kila Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji nchini.

Rais angejifunza kujizuia kutoa matamko barabarani angeisaidia Sana nchi na kujisaidia yeye mwenyewe kutimiza ndoto zake kwa nchi anayoongoza. Mimi binafsi naunga mkono kuwa ni lazima tuchenjue dhahabu hapa hapa nchini badala ya kupeleka mchanga Japan na China. Lakini ni muhimu maamuzi hayo yawe na ushahidi wa kisayansi badala ya matamko holela ambayo madhara yake Kwa nchi ni makubwa mno.

Zitto Kabwe, Mb
Arusha
26/3/2017

==== maelezo yangu kwa Mhariri RaiaMwema ====

Agizo la kutosafirisha Mchanga Liende Sambamba na Kujenga Uwezo Wetu Kama Taifa Katika Uchenjuaji (Refining)

[Maoni Yangu ya Hatua ya Serikali Kuzuia Kusafirishwa kwa Mchanga Kutoka Migodini]

"Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa (economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 hivi.

Pia tunahitaji umeme zaidi ya megawati 1500 kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama fursa (potential) ya ukanda wetu ya kuzalisha huo mchanga (copper concentrates) ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region (ukanda huu). Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo.

Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio lilitolewa na Serikali litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa.

Kwahiyo AMRI hii ya Serikali itusaidie kuuleta mezani mjadala huu kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.

Lakini pia wataalamu wanaweza kukaa na kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini. Haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.

Ushauri wangu ni kwamba Serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka commitment (dhamira ya utekelezaji) ya muda maalumu wa kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.

Hii sio Zero - Sum game (Kama sio kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi".

Gazeti la [HASHTAG]#RaiaMwema[/HASHTAG] waliniuliza maoni yangu kuhusu zuio la kupeleka nje mchanga kutoka kwenye migodi ya uchimbaji madini nchini. Maelezo haya sehemu ya majibu yangu kwao ambayo yamenukuliwa na toleo la gazeti hilo, toleo namba 500 la machi 8, 2017. Kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua (refinery).

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Kibingo, Mwandiga Township
Kigoma
Machi 8, 2017
Zitto ungeweza kujilinda wasiinunue akili na mdomo wako, ukajitenga na tamaa za ajabu ajabu ungeaminika kupewa mamlaka ya juu na nchi kama nchi ingefaidika na taaluma uliyonayo.

Kwa sasa wewe ni sawa na Dubois v/s Marcus Gavey.
 
Nyie mlikubali nchi kuongozwa na akili ndogo kwa hiyo acheni twende kwa akili ndogo tuone tutaishia wapi. Tuliwaambia huyu mtu ni mzee wa kukurupuka mkabisha. Hata wewe Zitto haukuwa na haja ya kumtumia yule mama yenu ACT bali ungepambana kwa kuungana na wenzio hata kama kura zingeibiwa.

Mzee anaongoza nchi kwa stori za mitaani, eti mule kwenye mchanga kuna dhahabu imefichwa ha haaaaa haaaa. Jamaa wana hadi viwanja vya ndege mgodini wanashindwa vipi kuhamisha dhahabu mgodini na kupeleka wanakotaka kwa ndege. Pia hii process ya kupeleka mchanga wa dhahabu kwenye Smelting inafanywa dunia nzima, huyu mzee hataki hata kusafiri atajulia wapi haya mambo?
Watu kama ninyi hamna hata fact..lakini mnajiandikia tu. Tafuta kwanza facts. Ww kwa uelewa wako mdogo unazani wazungu wanasafirisha mchanga wa kufukia mabonde huko kwao. Acheni siasa zisizo na mashiko kwa taifa. Magufuli has got very interesting here.
 
Amri ya Rais kuhusu 'Mchanga wa Dhahabu' imepotezea nchi Tshs 1.8trn Capital Gains Tax

Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining.

Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali.

Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni.

Tafiti zinaonyesha kuwa gharama ya kujenga ' refinery ' ya kuchenjua dhahabu hapa nchini ni USD 800m. Hivyo mapato ambayo yangepatikana kutokana na kodi ya mauzo ya Acacia yangewezesha nchi kujenga refinery na kufikia lengo la Rais la kuwa na uchenjuaji wa mchanga ule hapa hapa nchini. Rais angetulia angeweza kuua ndege wawili Kwa jiwe moja, 1) kiwanda cha kuchenjua kingejengwa nchini na 2) mchanga usingesafirishwa tena kwenda China na Japan.

Hata hivyo Tanzania haina mchanga wa kutosha wa kushibisha hiyo refinery Kwa mujibu wa teknolojia ya sasa ( soma maelezo yangu hapa chini Kwa Mhariri wa RaiaMwema). Hivyo Rais angeweza kutumia mapato hayo Kwa matumizi mengine ya Maendeleo. Kwa mfano Bunge lilitenga kama USD 430m hivi kujenga Reli ya kisasa na tayari Serikali imeshaingia mkataba na kampuni kutoka Uturuki kujenga Reli hiyo kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro. Lakini gharama ya kipande hicho ni USD 1.2bn. Kwahiyo Rais angeweza kutumia mapato haya ya mauzo ya Acacia kuongezea kwenye kipande hiki na hivyo kuepuka kukopa kuziba nakisi ya USD 800m iliyopo Sasa na Bunge kwenye Bajeti ya 2017/18 lingetenga fedha za kuanzia Morogoro kwenda Dodoma.

Kama Mipango ya Reli ipo sawa, Rais angeweza kutumia fedha za capital gains tax kutoka Acacia kujenga vyuo vya VETA kila Wilaya na kila Kambi ya JKT na chenji ingebaki. Tanzania inahitaji tshs 750 bilioni kujenga vyuo vya VETA kila Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji nchini.

Rais angejifunza kujizuia kutoa matamko barabarani angeisaidia Sana nchi na kujisaidia yeye mwenyewe kutimiza ndoto zake kwa nchi anayoongoza. Mimi binafsi naunga mkono kuwa ni lazima tuchenjue dhahabu hapa hapa nchini badala ya kupeleka mchanga Japan na China. Lakini ni muhimu maamuzi hayo yawe na ushahidi wa kisayansi badala ya matamko holela ambayo madhara yake Kwa nchi ni makubwa mno.

Zitto Kabwe, Mb
Arusha
26/3/2017

==== maelezo yangu kwa Mhariri RaiaMwema ====

Agizo la kutosafirisha Mchanga Liende Sambamba na Kujenga Uwezo Wetu Kama Taifa Katika Uchenjuaji (Refining)

[Maoni Yangu ya Hatua ya Serikali Kuzuia Kusafirishwa kwa Mchanga Kutoka Migodini]

"Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa (economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 hivi.

Pia tunahitaji umeme zaidi ya megawati 1500 kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama fursa (potential) ya ukanda wetu ya kuzalisha huo mchanga (copper concentrates) ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region (ukanda huu). Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo.

Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio lilitolewa na Serikali litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa.

Kwahiyo AMRI hii ya Serikali itusaidie kuuleta mezani mjadala huu kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.

Lakini pia wataalamu wanaweza kukaa na kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini. Haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.

Ushauri wangu ni kwamba Serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka commitment (dhamira ya utekelezaji) ya muda maalumu wa kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.

Hii sio Zero - Sum game (Kama sio kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi".

Gazeti la [HASHTAG]#RaiaMwema[/HASHTAG] waliniuliza maoni yangu kuhusu zuio la kupeleka nje mchanga kutoka kwenye migodi ya uchimbaji madini nchini. Maelezo haya sehemu ya majibu yangu kwao ambayo yamenukuliwa na toleo la gazeti hilo, toleo namba 500 la machi 8, 2017. Kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua (refinery).

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Kibingo, Mwandiga Township
Kigoma
Machi 8, 2017
 
Sasa kama hayo mapato ndio tunapoteza kama taifa, mbon hayaonekani kwenye kodi. Nadhani mwanzoni tumeambiwa ni panya yuko kwenye tundu. Mboka kama anatoka paka???. Kiasi hicho cha hela kweli!. Mungu tusaidie
 
Sorry for my ignorance,

Mheshimiwa Zitto, mbona sijawahi kuona mchango wa haya madini, mafuta, etc kwenye bajeti ya Taifa?? Kila siku mapato ni ya kodi za walalahoi, mabenki, vilevi, sigara, magari yanayoingizwa, mashirika ya mawasiliano (VODACOM, AIRTEL, etc...) nk. Haya mapato ya madini na mafuta huwa yanaingizwa wapi na ni kiasi gani? Please, usichanganye na hela kiduchu wanazopewa halmashauri zinazohusika.

Kama nilivyosema, mimi sio msomi wa maeneo hayo, inawezekana ni umbumbumbu wangu, hivyo mtanisamehe.
 
Zitto amejuaje kama maongezi yao yangepelekea kukubaliana kuuziana hayo makampuni?

Je, hayo maongezi yangechukua muda gani mpaka makubaliano wakati wakiendelea kusafirisha mchanga wetu?

Zitto amejuaje kiasi cha pesa ambacho kingepatikana wakati walikuwa bado wanafanya makubaliano?

Kubwa zaidi, inaonekana hawa jamaa walikuwa wanapata faida kubwa sana kwenye mchanga wetu kwa sababu kama sababu ya kuvunjika kwa makubaliano ni katazo la kusafirisha mchanga.

Inawezekana hawa jamaa wanamtumia Zitto katika msingi wa delay tactics ili wapate muda wa kuficha kilichoko ndani ya makontena baada ya kugundua serikali iko mbioni kuanza uchunguzi.
 
Kitu ambacho huwa sielewi hivi wale watu huo mchanga huwa wanaiba au ni halali kutokana na mikataba?

Na wale wa mwanza aliowaambia wapewe wananchi iliishia wapi?
Hiyo ni mikataba halali ambayo kwa ridhaa yetu Pasi kushutishwa na mtutu wa bunduki tuliamua kuiridhia sasa kutoa maagizo mchanga uzuiliwe ni jambo jema linalokiuka mikataba tuliyoingia na hao mabepari jambo la hekima tulipaswa kupitia upya mikataba yao pamoja na sheria zinazosimamia rasilimari zetu pamoja na sheria za mikataba tukibaini mapungufu tuzirekebishe hizi shortcut za magufuli zitatugharimu Siku sio nyingi.

Hatua ya mh raisi inkiuka mikataba yetu kiufupi tusubiri kesi tu kama hao wenye mchanga wataamua kureact kihivyo.
 
Wapinzani walitaka serikali iliyo na uwazi na Uwajibikaji Nashangaa serikali ya JPM inafanya hivyo Lakini wanaipinga. Tatizo LA upinzani hawajiamini wanaona kwamba magufuli akifanya vizuri watafunikwa uchaguzi ujao. JPM anafanya vizuri Sana mambo ambayo watanzania tulikuwa tunayasikia Sasa tunayajua
Mfano hili la mchanga
Lingine ni Mbinu za wauza madawa
Ufisadi mwingi tu magufuli harembi ni Kiongozi anayesema ukweli. Wakosoaji wake wana hoja dhaifu
Hebu mwanaCCM mwenzangu tujadili bila mhemko..je hili la mchanga lipo katika mkataba tulioingia wenyewe..lakini pia mbona hata ukibaki hapa kwetu hauna msaada wowote na hatuna uwezo wa kuuchejua. Au tuufanyeje tushauri kama alivyoomba Mwenyekiti wetu sio kupinga au kupingana. Hatujibu hoja tunaingelea maono na madhaifu ya wapinzani wetu hata wakitukumbusha vitu muhimu..tutafakari.
 
Kitu ambacho huwa sielewi hivi wale watu huo mchanga huwa wanaiba au ni halali kutokana na mikataba?

Na wale wa mwanza aliowaambia wapewe wananchi iliishia wapi?
Tumeambiwa na wataalamu wetu kwamba hakuna kitu kinaitwa mchanga ile ni dhahabu inayosubiri kuchekechwa tu sisi ni wapumbavu ana kujifanya wapinzani wa kila kitu
 
Back
Top Bottom