Zitto amjia juu Waziri Mkuu: Aandika barua kuhoji matumizi ya "Stimulus Package"

Pole sana MDANGANYIKA mwenzangu kwani asilimi 90 ya hayo makampuni HEWA au yalikuwa yamekufa na yakafufuka kuvuta mpunga, au ni ya mfukoni.
Hivi unajau ni nani alikuwa anaidhinisha kibali kuwa hii kampuni imehathirika? I guess it was CRDB Bank, Unategemea nini kutoka kwa KIMEI?
I love Tz, no wonder kina bashe wanang'ang'ania uraia
 
Hivi ni nani vile alisema kuandika katiba mpya is very expensive?

Kwa mwendo huu naamini tutafika tu, ila namshauri zitto awe makini sana watanzania walishaanza kumuona mamluki, ndugu yangu zitto utu wako una thamani kuliko kiasi chochote kile cha pesa, usikubali kuuza utu wako kwa vijisenti, kama umeamua kujivua gamba basi endelea hivyo hivyo, halafu achana na mambo ya kupongeza pongeza ccm sio kazi yako hiyo.
 
.
Utamsababisha baba wa watu aangue kilio ooh!
Niko safarini na natumia simu laiti hii habari ingekuwa kwa namna inayowezesha kusoma kwenye simu. Nahisi ningeitafuna mpaka nituboe meno kaa mtu aliyekula nyama.
.

Fanyeni mpango nasi tunaotumia simu tuweze isome kwani tunaona mnachangia lakini hatujui(hakisomeki kwa kutumia simu) kilichoandikwa.

Nimejaribu nimeshindwa, ma-pro watusaidie, meanwhile tafuta PC bcoz iko kama PDF file.
Poleni
 
Huwa Watu hawanielewi pindi naposema kwamba,Tangu Nnji hii ipate uhuru toka kwa Bibi,haijawahi kutokea kuwa na Raisi na Waziri Mkuu Bomu.Ingawa EL alikuwa na Mapungufu yake ya kutaka kila senti inayopita mbele yake akwapue,lakini alikuwa na elements za uongozi ambazo zikuwa zinamfanya aongoze subordinates wake vizuri.Alivyoteuliwa Pinda na kujiita Mtoto wa Mkulima,hapa nilisema kuwa huyu jamaa hawezi kuwa PM.Kwanza ana nidhamu ya Uoga mbele ya Bosi wake(Jk),hasimami kwenye maneno yake,leo atazungumza hili na kesho atasahau alilozungumza jana na kulipamba lile baya la jana kuwa Zuri leo.Sasa kama mpaka leo PM hajapitia Report ya CAG,huyo Mkulo atakuwa ameipitia kweli?.Hivi,hii nchi ina viongozi wa namna gani na ni nani anawajibika kwa Wenzake katika ya Viongozi wa Serikali na Wananchi?.Kama utajivua gamba la mwili na akili ikabaki ile ile,ni sawa na akili ya Kenge kukimbilia mtoni ili akwepe kuloa Mvua.Watu wakiandamana,wapuuzi na matamko yao watakuja kusema,hawa jamaa wanataka Nchi isitawalike.Ipo siku huu upuuzi utaisha na si muda mrefu maana ishara ya Mwanakondoo kurudi tena Duniani zinaonekana.Just a matter of time
 
Halafu mnasema Pinda ni mtoto wa mkulima na makini! Mnanikera sana!! Zaidi ya uongo alionao Pinda ni fisadi mkubwa, Kikwete naye ambaye ripoti zote za CAG zinapelekwa kwake na anaona uozo wote na anakaa kimya ni fisadi pia. Nilishasema CCM wote ni mafisadi ila wanatofautiana viwango tu!! Kwenye sera yao ya kuvuana magamba wangeanza na mwenyekiti kwanza ambaye nina uhakika kila tuhuma ya ufisadi iwe ya Dowans, meremeta, Deep Green, Kiwira Coal mines, Barick Gold etc inamhusu either directly au indirectly!!
 
Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe amesema anasikitishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokuwa na taarifa za ubadhirifu mkubwa wa fedha za Mfuko wa Kuhuisha Uchumi.

Taarifa ya Zitto aliyotoa kwa vyombo vya habari jana, inasema hatua ya Pinda kuonyesha kwamba hana taarifa za upotevu wa Sh48 bilioni, inaonyesha kuwa Serikali haipo makini katika kusimamia fedha za umma.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, alitoa taarifa hiyo baada ya kutoridhishwa na majibu ya Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo, kuhusu upotevu wa Sh48 bilioni za mfuko huo ambazo zimeonyeshwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba zimepotea na Pinda kusema hana taarifa hizo.

Taarifa ya CAG inaonyesha upotevu wa Sh48 bilioni kati ya Sh1.7 trilioni zilizotolewa na Serikali. Pia inadaiwa kuwa Serikali ilimnyima majina ya watu na kampuni zilizokopa fedha hizo ili kujua iwapo zilitolewa kwenye taratibu za kawaida.
Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, alimtaka Pinda kutoa taarifa kwa umma mara moja kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha hizo.

“Vilevile Serikali ihakikishe CAG anafanya ukaguzi maalumu kwenye fedha zote za Mfuko wa Kuhuisha Uchumi, ambazo ni takriban Sh1.7 trilioni. Kuna shaka kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili hii zilitumika vibaya, kufujwa na kuibwa. Shaka hii itaondoka iwapo CAG atafanya ukaguzi maalumu.”

Alisema akiwa Waziri kivuli wa Fedha na Uchumi, ataendelea kuhoji suala hilo hadi ukweli utakapobainika na waliofuja fedha hizo wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.“Naomba umma wa Watanzania ujue kuwa fedha za mpango huu ni nyingi mno, haiwezekani kuachwa bila kufanyiwa ukaguzi ambao unatakiwa kuwekwa wazi kwa umma,” alisema.

Baada ya kutokea mtikisiko wa uchumi duniani, Serikali ilitenga Sh1.7 trilioni kwa ajili ya kampuni ambazo zilikuwa zimenunua mazao ili kuzinusuru na mtikisiko huo.

Miongoni mwa kampuni zilizopata fedha hizo ni zile zinazonunua pamba ambazo zilitakiwa kutoa fidia ya Sh80 kwa kilo ya pamba ambayo ilikuwa imenunuliwa.Hata hivyo, kwa mujibu wa Mbunge wa Bariadi Magharibi (UDP), John Cheyo hadi sasa wakulima hawajalipwa fidia hiyo.
zitto%20kabwe%201.jpg

tanzania-news-mwananchi-newspapers.jpg
 
Zitto anashanga nini ama hakupata mgao... Ma swaiba zake EL, RA wanabanwa Alishaanza kutusaliti sijui ndio gear ya kujisafisha ama hajapata percent
 
Safi sana kijana! naona unarudisha imani yetu kwako tena...kila la heri...tunachotaka ni mtu mzalendo na mchapa kazi.
 
Zitto anashanga nini ama hakupata mgao... Ma swaiba zake EL, RA wanabanwa Alishaanza kutusaliti sijui ndio gear ya kujisafisha ama hajapata percent

Acha kumpinga Zitto kwa kila jambo...akifanya kazi nzuri lazima awe na haki ya kupongezwa. Angefanya hivyo Slaa, au Mnyika, au Mdee angonekana shujaa mkubwa...lakini Zitto anaonekana 'anajikomba'! Tuache hizi mambo, tunaharibu chama chetu na tunavunja moyo wapiganaji wetu.

Good work Zitto!
 
attacks from RA and EL......wanajua nani waliopewa hizo pesa na wako wapi!!wanataka wamchafue bro wao...ili magamba wavuliwe wengi zaidi ama la wanyamaze
 
Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe amesema anasikitishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokuwa na taarifa za ubadhirifu mkubwa wa fedha za Mfuko wa Kuhuisha Uchumi.

Taarifa ya Zitto aliyotoa kwa vyombo vya habari jana, inasema hatua ya Pinda kuonyesha kwamba hana taarifa za upotevu wa Sh48 bilioni, inaonyesha kuwa Serikali haipo makini katika kusimamia fedha za umma.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, alitoa taarifa hiyo baada ya kutoridhishwa na majibu ya Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo, kuhusu upotevu wa Sh48 bilioni za mfuko huo ambazo zimeonyeshwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba zimepotea na Pinda kusema hana taarifa hizo.

Taarifa ya CAG inaonyesha upotevu wa Sh48 bilioni kati ya Sh1.7 trilioni zilizotolewa na Serikali. Pia inadaiwa kuwa Serikali ilimnyima majina ya watu na kampuni zilizokopa fedha hizo ili kujua iwapo zilitolewa kwenye taratibu za kawaida.
Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, alimtaka Pinda kutoa taarifa kwa umma mara moja kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha hizo.

“Vilevile Serikali ihakikishe CAG anafanya ukaguzi maalumu kwenye fedha zote za Mfuko wa Kuhuisha Uchumi, ambazo ni takriban Sh1.7 trilioni. Kuna shaka kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili hii zilitumika vibaya, kufujwa na kuibwa. Shaka hii itaondoka iwapo CAG atafanya ukaguzi maalumu.”

Alisema akiwa Waziri kivuli wa Fedha na Uchumi, ataendelea kuhoji suala hilo hadi ukweli utakapobainika na waliofuja fedha hizo wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.“Naomba umma wa Watanzania ujue kuwa fedha za mpango huu ni nyingi mno, haiwezekani kuachwa bila kufanyiwa ukaguzi ambao unatakiwa kuwekwa wazi kwa umma,” alisema.

Baada ya kutokea mtikisiko wa uchumi duniani, Serikali ilitenga Sh1.7 trilioni kwa ajili ya kampuni ambazo zilikuwa zimenunua mazao ili kuzinusuru na mtikisiko huo.

Miongoni mwa kampuni zilizopata fedha hizo ni zile zinazonunua pamba ambazo zilitakiwa kutoa fidia ya Sh80 kwa kilo ya pamba ambayo ilikuwa imenunuliwa.Hata hivyo, kwa mujibu wa Mbunge wa Bariadi Magharibi (UDP), John Cheyo hadi sasa wakulima hawajalipwa fidia hiyo.
zitto%20kabwe%201.jpg

tanzania-news-mwananchi-newspapers.jpg

Big up sana Zitto. Binafsi nimejuzwa jambo nyeti sana ambali sikulijua awali. Nitahakikisha ninalikumbuka hili hadi siku ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Jamani tusiwe na tabia ya kumshambulia Zitto kwa kila jambo ... iwapo analake jambo, down the road totaona na tutamrekebisha tuu. So far, ninampa pongezi nyingi sana kwa juhudi zake binafsi.
 
Zitto Big Up, kwa ahadi yako usirudi nyuma tena nasema ikibidi pata hata majina ya makampuni yaliyonuifaika na hiyo "Stimlus package". Ndg yangu uliyejuzwa swala ulilokuwa hulitambui tunaweza kushare?
 
What the hell!!!.....The PM does not know why the Tanzanians are poor, can he really know the CAG's report?.
He seems to know nothing! He does not even know that he is the PM. Poor Pinda Mizengwe.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mhe.Zitto anastahili pongezi kwa kazi nzuri. hayo mengine hayana maana kwa sasa kwani yalishajadiliwa na kuamuliwa ktk vikao vya chama (CHADEMA) kama kungekuwa na jingine la zaidi nadhani angefanya kama Shitambala. maadamu yupo na tumempa kofia 4 kubwa bungeni, (msaidizi wa mkuu wa kambi ya upinzani, mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma , waziri kivuli wa Fedha na Uchumi, mbunge wa Kigoma kzn) naona anchokifanya sasa na kutekeleza mjukumu yake hayo. tena kwa ufanisi. hebu tumuunge mkono yeye na wapiganaji wengine tuliowatuma huko. Peeopleeeee's Power !!!!!!
 
Kudos Zitto.

Mpaka kieleweke, huu ni mwendelzo wa ufujaji wa fedha za Umma, ambazo zingetumika vizuri zingesaidia uchumi raia mmoja mmoja. Hakuna na haiwezekani CCM wala serikali yake kupambana na ufisadi....uko kwenye damu yao. Ukiutoa wanakufa.

Pinda alishashindwa kazi zamani, akawa anatumia unafiki na kivuli cha woga (unyenyekevu bandia) kuwazuga watu lakini muda umefika huyu mpumbavu akae pembeni.
 
Mh. Zitto, we umethubutu kutusemea, endelea na mpaka kieleweke. Huku kwenye Cotton Industry ndo baadhi ya hizo mapesa zimeliwa na mafisadi. Kuna kampuni ambayo ninauhakika haikupata hasara lkn ililamba 3Billion, na inasemekana Riz1 ni mmoja wa wamiliki. Na PM si kweli kwamba hajui, yeye anahusika.

Pia, kuna makampuni hewa yaliundwa haraka kuzichukua hizi mapesa na tunayajua, ila hatuna pa kusemea. Gazeti la Raia mwema liliwahi kuandika hii issue lkn halikuwa na data za kutosha na mahali lilidanganywa na informers wake kwa makusudi ama pengine hawakuwa jikoni.

Huku kwenye Cotton Industry kuna akina Mkon-o, Cheng-e, Riz1, Kigwangal-a (anatumika), Mohame-d (MeTL), Steve Wassir-a na wengine wengi wababe wa nchi hii. Hivyo, Zitto kama umedhamilia kufuatilia hili "saga" unawagusa wengi na ujiandae kwa maandamano maana si rahisi kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kama unavyodai.
 
Mlangaja umesema kweli hii pesa ingetosha kutengeneza km 2,244 za barabara ya kwa kiwango cha lami. yaani barabara ya kutoka dar hadi Mbeya na nyingine kutoka Dar hadi Musoma!!
nisichoelewa ni kuwa wao walikuwa wakisistiza kuwa mdororo wa uchumi duniani haukuathiri uchumi wetu sasa hii pesa walitenga kwa ajili ya nini wakati uchumi wetu ulikuwa hauathiriki kwa namna yoyote ile na mdororo huo! wanadhani sisi ni wasahaulifu kiasi hicho? saa hizi Mkulo anadai mgawo wa umeme haujaathiri uchumi wetu, lakini kesho utasikia tumeshindwa kutimiliza malengo yetu kwa sababu ya ukosefu wa umeme. nchi hii ni usanii mtupu!! anyway Kina Zitto endeleeni kuwaumbua hivyohivyo hadi kieleweke!!
 
Back
Top Bottom