Zitto amjia juu Waziri Mkuu: Aandika barua kuhoji matumizi ya "Stimulus Package"

images

hahahhahahha!!!! mimi hapa ndio ninapomkubaliaga mzee mzima ZITTO KABWE , Msekwa alishasoma alama za nyakati nini ,ndio maana akaipiga JF dongo sasa MZEE MZIMA ZITTO KABWE kawapiga ccm na waziri mkuu TANGANYIKA JEKI,hatoki mtu hadi kieleweke
kaka una hatari,huyo zitto pichani ndo kawapiga t.jeki au??
 
Siku zote mimi huwa nasema na kulalamika kuwa Tanzania hatuna waziri mkuu kwa sasa bali tunaye mwigizaji tu mwenye kujua matumizi ya maneno mazuri yanayofumba macho ya wananchi. Ukweli utabaki pale pale kuwa kati ya Mawaziri Wakuu wote, huyu wa sasa ni sifuri kabisa. Mpaka sasa hakuna jambo lolote la maana ambalo mtanzania yoyote anaweza kusimama hadharani na kusema kuwa PM atakumbukwa hata vizazi vijavyo. The current PM has no impact at all. Ni heri hata ya EL maana alikuwa anauwezo wa kukemea na kutumia rungu la PM kuleta nidhamu serikalini. Huyu wa sasa hajui hata namna ya kutumia rungu la PM badala yake ni bingwa wa kulalamika eti hivi mara vile. Eti, mimi ningependa tuache kununua mashangingi, mara oooh. Huo ni ukiraza wa kutumia madaraka vizuri.

.
Utamsababisha baba wa watu aangue kilio ooh!
Niko safarini na natumia simu laiti hii habari ingekuwa kwa namna inayowezesha kusoma kwenye simu. Nahisi ningeitafuna mpaka nituboe meno kaa mtu aliyekula nyama.
.
 
JF,

This is yet another financial crime. Hii serikali kweli ni ya
kinyonyaji ni mpaka itolewe kinguvu, hivi hivi nothing will happen. They cant be bother to see what kicked off ousting of the Arab countries leaders recently?

Guys, watanzania pia tuna MADAI HALALI! from our leadership.
 
Nilisema kuwa huyu anayejiita mtoto wa mkulima ni bure tu! Hana lolote la kuwasaidia watanzania. Ni bora hata ya EL.
 
Kwa kuongezea, hizo pesa zilitolewa kama mkopo au grants?? Mbona US govt wao walitoa pesa almost zote na kuchukua stakes kwenye hizo kampuni kma GM, Citigroup ili uko mbele kampuni zikirudi kwenye mstari serikali wanapata pesa zao back. Sisi vipi?? Naomba Mh. Zitto ufuatilie na hili.

Big up Mazee Zitto
 
Hivi kweli hii hela ilikwenda wapi??

Kama ilitolewa ni kwa makampuni yapi?

Ukiangalia marekani makampuni yote yaliyosaidiwa ina maana serekali iliyanunua na kuyaweka chini ya usimamizi wake hadi hapo yatakaposimama.. Sasa hapo bongo ni vipi??
 
Samahani kuwa offpoint: kiongozi wa upinzani kutumia gmail address? Jee bunge haikupi official email address ambayo messages zinaweza kulindwa?

Kama siyo bunge basi japo Chadema tafuteni domain yenu muwe na email address zenu.
 
Hongera Zitto, trully from my heart! Do something good, utasifiwa; ukichemsha, unapakwa hii ndio JF!

Hii ina apply kwa viongozi wote bila kujali DINI; Pinda hafai, anapakwa. Sijasoma post za wale rafiki zetu, ambao kila tukimpaka JK wanaanza ooh JF kuna udini! Sasa naomba hao waseme tunampaka P.nda kwa kuwa ni Mkristu!
 
Hivi watanzania tuna waziri mkuu au tuna boya tu lililowekwa kwa faida ya mafisadi CCM? Waziri mkuu gani mnafiki hivi! lol
Anyway hongera sana broo Zitto.
 
je makampuni yaliyopewa pesa hizi hayana uhusiano na rostam, lowasa na chenge? tunaomba orodha yake hapa. ni matayarisho ya uchaguzi mkuu 2015? au zilishatumika uchaguzi wa 2010?
wanasiaisa waone huruma kwa maskini wa nchi hii. walaaniwe mafisadi

Moja ya waliokopeshwa ni pamoja na Bank ya CRDB
 
Ni barua nzito, ni kauli nzito. Naona baada ya Zitto kuona umma upo against yeye na umaarufu wake kushuka gafla, ameanza kujirekebisha. Huru ndie Zitto ninayemfahamu, ila Zitto wa kama miezi sita iliyopita alikuwa bandia nadhani:yield:

Wengi wetu humu tuliepuka mjadala kuhusu Zitto dhidi ya CDM. Uongozi unahitaji umakini na uchambuzi wa taarifa hasa zinazowahusu wananchi. Naomba tusiwatilie mashaka viongozi wetu ambao tuliwachagua kwa imani kwa vigezo vyetu. Halafu tukumbuke bado ni mwanzo tu waswahili husema mechi dakika 90; ila ni vema kukumbushana agenda tunazotaka wazisogeze mbele. Nakupongeza kwa kumu assess Mh. Zitto fairly angalau kwenye hili najua ameona mchango wako.
 
Kama ametingwa sana na mambo mengine na hili bado hajalipitia, kosa liko wapi? Ametingwa.

Kama mngekuwa makini sana na ripoti ya CAG na kuiona ni ya muhimu sana basi sheria ingesema "masaa 72 baada ya Rais kupokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu, serikali italazimika kufanya a be che de..." Au siku 72, au wiki 72. Kungekuwa na time-bound implementation strictures.

CAG ameshatoa ripoti ngapi zikachanwa na kutawaziwa?

Sheria inamruhusu anaepewa ripoti akisema sasa hivi nimetingwa, hiyo ripoti nitaifanyia kazi nitakapoifikia. Mwisho wa igizo.
 
Hiyo ndiyo inayoitwa "attention to detail" ambayo wananchi wanapaswa kuwa nayo. Katika "value for money evaluation" ya CAG, je aligusia umuhimu na ulazima wa zile kampuni zilizofaidika na hizo trilioni 1.7?

Value for money audit ni pale unapoweza kuzuia matumizi mabaya kufanyika through value for money audit. Hii ya CAG ni after effectt, money is already out of door, resources zishanyakwa na wajanja wachache, so hakuna value hapo, it is done, labda hao mabeberu wakikamatwa wazirudishe na sijui watazitoa wapi, manake zipo in form of mabango na picha za kampeni, tshirt na kofia, pilau etc.

JK alipotoa hotuba yake kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani, nilicheka sana, manake huo mtikisiko hata iweje usingefika TZ. Mtikisiko ule ulitokana na masoko ya fedha na mortgage (credit crunch), ambapo TZ haiko connected kabisa. Kama ni kutikisika kwa uchumi Tanzania mbona kila siku, sio tu unatikisika, bali unakata viuno/mayenu kila siku, loh!!

Suala hili la mtikisiko tulilijadili hapa JF kwa kirefu sana. But he managed to get away with it kwa kuwa clearly zilikuwa ni fedha za uchaguzi alikuwa anatafuta. Na hata hizo hazikutosha ndio tunaona hizi za dowans nazo ni deni linarudishwa kijanja janja. Wabunge walikuwepo, walipitisha, walijua kuna mgawo wao. Kuingia kwa Slaa kwenye kinyanganyiro kulifanya mipango mingi ibadilike, more money needed etc, na ndio maana tunaona hizi vurugu vurgu za dowans etc ni njia ya kurudisha fedha zilizochukuliwa kwa dharura ili kummaliza nguvu Slaa. Japo matrilion yalitumika, bado JK alipigwa chini, kazi kweli kweli

Kampuni zilizonufaika na mgawo huo zilifanya nini. US walitoa stimulus kwa mabenki ili yaweze kuendelea kutoa credit kwa small businesses, walipewa pia AIG etc ambayo ingecolapse kama wasingepewa fedha, pia makampuni ya magari ambayo yangekufa etc. Uchumi wa US uko connected, wall street ikipata shida, effect zake ni immedeate kwa uchumi wa US. Je Tanzania kuna kampuni gani ambayo ingecolapse na kuangusha uchumi kama wasingepewa fedha za stimulus, au kampuni ya JK ya mananasi???? Lets be serious, Kabwe please waulizie watanzania hili swali, na kuwa linataka majibu sahihi. Wajinga ndio waliwao, yaani JK kawafanya Watanzania wajinga kweli kweli, akishirikiana na Professor Ndulu, loh loh
 
Hivi hamjui tu? Unajua hizo hela za kuweka mabango nchi nzima walizitoa wapi? Mwaka 2005 walikula EPA , mwaka 2010 walikula kwenye stimulus-Package

Kama kuna mwana CCM mwenye ubavu abishe

Mimi ninabisha kwani najua walichota katika fungu jingine ikiwa ni pamoja na noti mpya bandia na ukweli wa zilikotoka fedha hizo utajulikana muda si mrefu. Watajithaidi kwama walivyofanya kwa Kagoda kuzuia uchunguzi walikotoa fedha hizo. Ukweli ni kwamba ufisadi umetawala katika serikali ya CCM licha ya kudai kujivua gamba ambayo ni hatua ya kuhujumu zaidi kwani nyoka aliyejivua gamba huwa ni mwepesi katika kile anachokijua vema-kuuma watu na mawindo yake, kujificha. Hivyo kwa CCM mbiu ni "wizi zaidi, ufisadi zaidi, na kujirusha zaidi."
 
Zitto weldone Chadema muwakabe ruba CCM na serikali waeleze zitarudishwa lini zikasaidie kujenga vyoo huko mtwara wanajisaidia kwenye nyasi
 
Kwa speed hii ni nzuri sana tutafika tu nchi ya ahadi. Vile vile mheshimiwa Zitto ungeliongeza kuwa CAG alihoji kuwa hajaonyeshwa kwanza mahitaji ya hiyo stimulus package kwa hizo kampuni zilizoomba. Pia je kama zimeathirika kweli na mtikisiko wa uchumi au ndio EPA nyengine. na mwisho kama hizo kampuni zitarudisha hizo hela maana ninavyofahamu mie katika taaluma ya uchumi stimulus package ni loan inayotakiwa irudishwe mambo yakiwa mazuri je hela yetu walipa kodi italipwa lini!!!!!!

Pole sana MDANGANYIKA mwenzangu kwani asilimi 90 ya hayo makampuni HEWA au yalikuwa yamekufa na yakafufuka kuvuta mpunga, au ni ya mfukoni.
Hivi unajau ni nani alikuwa anaidhinisha kibali kuwa hii kampuni imehathirika? I guess it was CRDB Bank, Unategemea nini kutoka kwa KIMEI?
 
Back
Top Bottom