Zitto amjia juu Waziri Mkuu: Aandika barua kuhoji matumizi ya "Stimulus Package"

Hivi hamjui tu? Unajua hizo hela za kuweka mabango nchi nzima walizitoa wapi? Mwaka 2005 walikula EPA , mwaka 2010 walikula kwenye stimulus-Package

Kama kuna mwana CCM mwenye ubavu abishe
 
Duh hii sasa kali,babu anasikilizia kikombe cha babu Mwasapila nini maana naona kila mara anaongea gabage, then hivi hawa wanasoma alama za nyakati kweli au wanafanya mazoea, any way nathani nati zinazofungwa na hawa CDM zitafunga tu ingawaje zinajifunga kwa tabu kutokana na kutu kwenye tread zake.

Kitaeleweka watake wasitake.
 
Imekaa vizuri ndo maana ccm wanataka wawe peke yao bungeni ili waendelee kutunyonya
 
Hii inatisha sana, ni kama ya meremeta, ubovu uliopo ni kwamba baadhi ya wabunge hufurahia wakati W Mkuu akileta mzaa bungeni. sisi watanzania tunasema kitaeleweka tu.

:angry:
 
Hiyo ndiyo inayoitwa "attention to detail" ambayo wananchi wanapaswa kuwa nayo. Katika "value for money evaluation" ya CAG, je aligusia umuhimu na ulazima wa zile kampuni zilizofaidika na hizo trilioni 1.7?
 
Tunaomba mtuletee majina ya hizo kampuni na nature of business conducted in the course of time ili tuweze kuchangia na kuwabomoa kabisa, kwani kampuni nyingi zilizofaidika ni fictitious
 
Hiyo ndiyo inayoitwa "attention to detail" ambayo wananchi wanapaswa kuwa nayo. Katika "value for money evaluation" ya CAG, je aligusia umuhimu na ulazima wa zile kampuni zilizofaidika na hizo trilioni 1.7?

Soma report mkuu ya CAG alihoji kama kuna taarifa zinazoonyesha kuwa hizo kampuni zilikuwa zinahitaji kweli huo mkopo na kama kweli waliathirika na economic recession basi apatiwe kwa bahati mbaya hakupatiwa mpaka report inatoka. Ila swali ambalo CAG hakulihoji ni JE HELA ZETU WALIZOPEWA HIZO KAMPUNI KAMA MKOPO WATARUDISHA LINI !!!!
 
Thanks my comrade tuko pamoja mpaka kieleweke Mungu akutie nguvu ili uweze kuwasaidia watanzania na mwisho wa siku watanzania wakupe medali ya ushindi kwa uongozi uliotukuka na hivyo kukufikisha katika destiny yako. If you would keep on and be focused like this basi uwe na hakika utapata kila deisire of your heart kabla ya kuondoka physically kwenye hii dunia. There is no receiving without giving hii ni principle of success iliyowekwa tangu kuumbwa kwa dunia.
 
Kwa matamshi haya tu anapaswa kujiuzulu ili uchunguzi ufanyike vizuri. Nona hili ni la kuitisha maandamano nchi nzima.

Kama bei ya kuweka barabara kilomit moja ni shilingi milioni 758 hela hii ingeweza kutengeneza barabara za urefu wa kilomita 2200. Hii siyo fedha ndogo.

Ni nyingi mno.

Ni kweli kwa nchi zenya maadili mema huyu ndg aliaswa kuwajibika mara moja!
 
Haya wabunge wa CCM mnaona wezenu wa CDM wanvyo ibua mambo zomeeni na hilo.Halafu kwanye maandamano ya kujivua magamba mliseme na hilo la Stimulus Package
 
Kazi tunayo watanzania, nilimwona Pinda anajikanyaga kusema hajaona taarifa ile na ghafla aliishiwa kujiamini ambayo ni dhahiri kabisa inaonyesha alikuwa anadanganya, na inaonekana anajua hiyo concern ya CAG lakini hakuwa na jibu la papo kwa papo.
 
Inasikitisha Waziri Mkuu anasema hajaipia ripoti ya mkaguzi mkuu Srikali!!!?,ni maajabu na kwa hili la aibu kwa Waziriri Mkuu ni bora ajiuzulu au anayobiashara nyingine nje ya Serikali!!?Ni aibu kwa taifa Ila Watanzania tumezoea kupiga kelele bila vitendo yaani bilioni 48 kwishne!!!?
 
Back
Top Bottom