Zitto amjia juu Waziri Mkuu: Aandika barua kuhoji matumizi ya "Stimulus Package"

nahavache

JF-Expert Member
Apr 3, 2009
871
246
Zitto-stimulus-Package_Page_1.jpg

Zitto-stimulus-Package_Page_2.jpg


Mmeiangalia hii jamani? Imekaaje?
 
Huyu ndiye Zitto haswa! Bravo mkuu; lakini tunataka feedback kama serikali itatoa majibu au la na hatua gani zinafuatia toka kwako na chama chako.
 
Hii sasa kali ina maana PM hajui CAG amekagua nini na maeneo yapi yana matatizo.
 
Kazi nzuri sana anafanya Zitto tumuunge mkono na kumsaidia

Hili liserikali linatisha kwa kufuja
 
CDM wanatakiwa kumshtaki kwa UMMA huyu mzee maana sasa uongo wake umezidi kiwango haiwezekani yeye kila wakati anasema uongo.Hawezi kuwafanya watanzania mataahira, haiwezekani PM asione ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali.ina maana kazi yake ni nini, anakula kodi zetu bure huyu babu.
 
Kwa matamshi haya tu anapaswa kujiuzulu ili uchunguzi ufanyike vizuri. Nona hili ni la kuitisha maandamano nchi nzima.

Kama bei ya kuweka barabara kilomit moja ni shilingi milioni 758 hela hii ingeweza kutengeneza barabara za urefu wa kilomita 2200. Hii siyo fedha ndogo.

Ni nyingi mno.
 
PM Pinda ameshikalia nafasi yake kwa kukariri utaratibu uliotumika na watangulizi wake kwa kusema uongo daim.Yeye hajajitambua kuwa yuko kipindi cha dot.com.kipindi hiki uelewa wa jamii ni mkubwa kuzidi uelewa wa serikali na watumishi wake.Wananchi ni waelewa sana, babu Pinda anaakiwa aamushwe kwa maandamano ya kulaani misimamo yake
 
Kila jambo tujaribu kulipa muda, Zitto sasa anaonekana vema.

Kiongozi yeyote bora huwa hakurupuki, bali hutafiti kwa kina japo jamii huwa na hamu/shauku ya kuona na kusikia tamko toka kinywani mwa mkuu fulani.

Nakupongeza Mh.Zitto kwa uyafanyayo, Mola muweza akuongezee HEKIMA, SUBRA & UPEVU wa mambo.
Keep it UP.

Mpevu.
 
Kwa speed hii ni nzuri sana tutafika tu nchi ya ahadi. Vile vile mheshimiwa Zitto ungeliongeza kuwa CAG alihoji kuwa hajaonyeshwa kwanza mahitaji ya hiyo stimulus package kwa hizo kampuni zilizoomba.

Pia je kama zimeathirika kweli na mtikisiko wa uchumi au ndio EPA nyengine. na mwisho kama hizo kampuni zitarudisha hizo hela maana ninavyofahamu mie katika taaluma ya uchumi stimulus package ni loan inayotakiwa irudishwe mambo yakiwa mazuri je hela yetu walipa kodi italipwa lini!!!!!!
 
bravo Zitto, naona umerudi baada ya kambi ya lowasa kulega ndani ya ccm!
 
Kwa majibu ya PM imeonyesha jinsi gani uwezo wake ulivyo. Speed ya Zitto katika kulishughulikia hili baada ya majibu ya PM imenifurahisha sana na kunifanya nizidi kuwadharau wale wenzetu wanaotumia nafasi tuliyowapa kuingia bungeni kwa kupiga makofi na kuzomea. Heko Zitto na wenzako,heshima yenu huku nje ya mjengo inapaa kwa kasi ya ajabu.
 
Ni barua nzito, ni kauli nzito. Naona baada ya Zitto kuona umma upo against yeye na umaarufu wake kushuka gafla, ameanza kujirekebisha. Huru ndie Zitto ninayemfahamu, ila Zitto wa kama miezi sita iliyopita alikuwa bandia nadhani:yield:
 
Tunaotumia simu tunashindwa kuisoma report hii muhimu.
Wakuu kama inawezekana mtufanyie namna ya kuweza kuisoma.
Jf inaogopwa na ccm na serikali yake kuliko mnavyofikiri. BIG UP!!
.
 
Yaani watu wamesha jilia kale ka-kuku chote, sasa wanatafura ustaarabu wa kitoweo kingine ndio tunashtuka. Yeah we are kind of slow aminia nikisema hawa jamaa wa CCM hawana trick ya kumuibia mtu yoyote they're not a clever bunch.

Only that we are kind of slow.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom