Zitto alivyofanikiwa jana kumuingiza spika kwenye mtego ambao alikuwa hawezi

Najiuliza kwanza kwamba ni jeuri ya kiasi gani mpaka sasa hawajajiuzulu hawa; AG,Waziri Muhogo na Naibu wake ,Katibu Mkuu wa Nishati na Prof. Tibaijuka-1.6bl waziri ndaani ya Baraza la Mawaziri ya Serikali inayolalamikiwa?

Sababu Mukulu aliidhinisha.
 
Kwa mapendekezi ya fisadi chenge hakuna jipya litakalofanyika na mamlaka ya uteuzi, na ndo maana huyu fisadi chenge alipendekeza hivo!
 
"BUNGE LINAPENDEKEZA WAZIRI MKUU ACHUKULIWE HATUA NA MAALAKA YA UTEUZI INAYOHUSIKA"hilo ndio lilikuwa pendekezo la Chenge Zitto aliloliunga mkono
Naomba tuijadili kauli hii moja tujielekeze kwa kujiuliza maamlaka za uteuzi wa Waziri mkuu ni zipi?kwa ufahamu wangu mdogo ni Rais na bunge,swali la pili azimio la bunge likishatoka bunge lenyewe linaweza kukubali kukiuka maazimio waliojiwekea?jibu ni hapana kwahy bunge lilikuwa linakuja kupata nguvu ya kumuwajibisha waziri mkuu baada tu ya kumaliza maazimio maana maazimio hayo yamepitishwa na bunge.kwahy hapa kama bunge lilikuwa limekwepa msimamo waliojipanga nao wabunge wa ccm pamoja na spika kuwa waziri mkuu katika maazimio wasikubali kupitisha azimio la kumsulubu.Kwahy jambo la kukumbuka hapa bunge lina nguvu na mtu mmoja tu kumuwajibisha ambaye ni waziri mkuu tu,endapo wakimuangusha waziri mkuu,waziri kama Mhongo na AG hawawezi kurudi tena na mchezo huo ulikuwa unalisaidia bunge kutoingilia mihimili mingine.Nakupongeza sana Zitto,Halima Mdee na Wenje kuona mbali ila siwalaumu wakioutegua mtego sio wao walishindwa tu kuchungulia walipopaona wenzao
 
mkuu zito anauwezo binafsi sipingi- lakini hata hivyo tayari master plan-chenge , mzee wa havard a.k.a mzee wa vijisenti tayari alikuwa kashamaliza zitto na kuwaokoa woote wakina maswi, werema, muhongo etc,

unajua kwanini???

Kwa yale maelezo ya kuframe ya chenge means tayari hawa watu woote ambao si uteuzi wa bunge,tayari walikuwa wanahamishiwa katika mamlaka iliyowateua ambayo ni raisi, na hapo ndipo wapinzani woote walikuwa wanapigwa bao, means mashitaka na ushauri wa bunge ulikuwa hauna nguvu tena kusema mbona fulani hajawajibishwa na rais maana hayo ni maamuzi yake rais akijisikia kuwawajibisha au la ni sawa, so hapa zitto aliwaza km 50, chenge akaenda 100 km but mbowe akaenda mbali zaidi yao woote 200km, coz bila hivyo tayari bunge lilikuwa halina nguvu tena kuwafuatilia watu hao. Na mbowe alimjulisha fasta Zitto kuwa hii imekula kwetu ndio maana mama makinda alipo mpa tena nafasi zitto kuongea akajifanya amechoka ili kupoteze akuwa wameshtukia hilo chezo...Na mchongo huo ccm ulipangwa ili badae raisi angepotezea tu na hakuna wakuwajibishwa wala bunge lisingekuwa na nguvu tena na watu hao kuwahoji hata kuwafuatilia tena.. So mbowe alishtuka mchezo huo... Ndio maana hata ukiwa makini kuangalia tangu mwanzo wakina simbachawene na mama kaiuruki walikuwa wanataka kumaliza mechi mapemaaaaa kabisaaa
kwa kumwambia makinda aridhie pendekezo la serikali no 7 la kusema kuwa kwa kila mteule wa raisi bunge lishauri tu kuwa watu hao wakithibitika wana makosa basi maamuzi yafanyike na mamlaka ya uteuzi, hivyo ilikuwa ni bunge linashauri tu so uamzi ungebaki kwa serikali kuchukua hatua ama la, na jk alishajipanga kupiga danadana kwa kujikita kusubiri ripoti za kimamlaka juu ya uchunguzi, na hilo lingefika hadi mwakani july bunge kuvunjwa..

sahihi sana!
 
Sio sahihi bhana nchi haindeshei kwa hisia ni kwa mujibu ea sheria hebu niambieni mlichokataa fupa limenuangukia rais ila kama wangekubaliana Zitto walikuwa wabunge wanaanza hapo hapo na waziri mkuu ambapo wabunge wangemuondia waziri mkuu junakuwa hakina serikali tena rais anabaki na Maswi tu natokeo yake wameenda kuridhiana na kuja na msimamo baridi
 
Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi:

Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema:

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na aliyekuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI, ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi (maelezo) iliyosema na Mh Chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki".

Kumbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8, 9...yalihusu kuwajibishwa Masele, Muhongo na Pinda.

Spika kwa kutokujua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka Waziri Mkuu ambaye Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote.

Spika akaona apige kura haraka haraka, kama kawaida CCM wakasema Ndiyoooo......

Punde tu Ole Sendeka ambae naye anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka, wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi, na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa, lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.

Hata wewe mwenyewe Hansen Nasli nimegundua una jicho la tatu hasa hapo kwenye blue nadhani ulikuwa umeyo maana ukawatazama hao wawili kabla hata speaker hajamtaja Zitto
 
Watu tunapenda sana kuongea mambo bila kuangalia mbali! Bunge lipi ambalo lingemwajibisha waziri mkuu? Hili bunge lenye asilimia zaidi 70 CCM? Pia asilimia kubwa ya wanaccm waliochangia walisema Waziri mkuu hausiki! Ni wazi hapa wangepiga kura ili kumwajibisha waziri mkuu, lakini nani anaamini kwamba wabunge wa CCM wangepiga kura ya kuingusha serikali yao? Hata wale waliokuwa wanaunga mkono waliohisika wawajibihswe walikuwa wansema wazi kuwa waziri mkuu hausiki. So this is just wishful thinking. Na mgomo uliofanywa na upinzani ulikuwa sahihi. Hakuna namna CCM na Makinda wangekubali waziri mkuu awajibike! In fact wangeptisha hilo azimio ingebidi liondolewe kama yalivyoondolewa yale mengine! Na wangejitetea kwamba hawakuamaaanisha na waziri mkuu awajibike!
 
Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi:

Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema:

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na aliyekuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI, ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi (maelezo) iliyosema na Mh Chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki".

Kumbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8, 9...yalihusu kuwajibishwa Masele, Muhongo na Pinda.

Spika kwa kutokujua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka Waziri Mkuu ambaye Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote.

Spika akaona apige kura haraka haraka, kama kawaida CCM wakasema Ndiyoooo......

Punde tu Ole Sendeka ambae naye anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka, wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi, na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa, lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.
MKUU,

Mimi binafsi nilimuelewa na nikashangilia kwa kupiga makofi, lakini bahati mbaya spika mlevi na mzembe akazinduliwa usingizini. HII NDIO SHIDA KUCHAGUA SPIKA KWA SIFA MOJA YA KUWA MWANAMKE!!!!!
 
We mtoa uzi si mpishi mzuri? Kampikie Zitto ugali na migebuke huko Mwandiga
 
Back
Top Bottom