Zitto alivyofanikiwa jana kumuingiza spika kwenye mtego ambao alikuwa hawezi

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
886
225
Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi:

Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema:

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na aliyekuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI, ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi (maelezo) iliyosema na Mh Chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki".

Kumbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8, 9...yalihusu kuwajibishwa Masele, Muhongo na Pinda.

Spika kwa kutokujua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka Waziri Mkuu ambaye Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote.

Spika akaona apige kura haraka haraka, kama kawaida CCM wakasema Ndiyoooo......

Punde tu Ole Sendeka ambae naye anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka, wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi, na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa, lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.
 
gsu

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
3,463
1,225
wewe unaonekana huelewi kabisa kilichokuwa kinaendelea ndani ya bunge.
 
Asa'rile

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
439
195

............ogopa vichwa.........
 
PARADIGM

JF-Expert Member
Sep 9, 2014
2,611
2,000
uko sawa kabisa. Ccm walishangilia bila kutafakari wakati hilo ndo lilukuwa anguko la raia!!
 
zegebovu1

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
414
250
Nchi ina hali mbaya bunge ni genge la wahuni, hakuna mtetezi wa wanyonge mahakamani rushwa, serikali haina nguvu makali/mamlaka, bunge mps walio wengi hawajielewi wanalitakia nn taifa hasa kwa vizazi vijavyo. Chama tawala ni uozo uozo uozo ila kuna baadhi ya wanachama wa ccm wanafaaa
 
Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
886
225
Unajua ukisema Pinda nae awajibishwe kupitia maalaka husika au za uteuzi maana yake ni wao bunge na mheshimiwa Rais kwahy unawapa nafasi ya wa bunge kumjadili Pinda na kumpigia kura ya kutokuwa nabimani nae aubkuleta azimio binafsi linaloitaji sahihi70 tu na jambo lilikuwa rahisi sana kwahy tumewafungua CCm na sasa watafanikiwa kumlinda Pinda
 
Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
886
225
Manyerere Zitto kwanza alibaini mpango wa CCM kwahy mwisho wa siku CCM ni wengi wangeshinda tu kwahy alitumia ufundi wa hali ya juu kumsulubu Pinda mmo wa kumuwajibisha Pinda ni bunge lenyewe kwahy unaruhusu azimio kumuwajibisha Pinda kwahy kama walilipitisha wenyewe ilikuwa ni lazima bunge likae kumuwajibisha Pinda kuliko kama azimio lingepita bila kusema kumuawajibisha
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,511
2,000
Huyu kijana Zitto Kabwe ni gifted, uwezo wake wa kisiasa kujadili na kuchambua hoja umethibitika katika sakata hili.
Myonge tumnyonge tu hadi afe lakini haki yake tumpe tu.
 
Ngongoseke

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
3,209
1,225
Jana sikuwa nimemuelewa ila niliposoma hapa sasa nimeelewa alichokusudia, bahati yake madam spika alistuka mchezo mzima
 
Eistein

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,107
1,195
huyu kijana zitto kabwe ni gifted, uwezo wake wa kisiasa kujadili na kuchambua hoja umethibitika katika sakata hili.
Myonge tumnyonge tu hadi afe lakini haki yake tumpe tu.

mkuu zito anauwezo binafsi sipingi- lakini hata hivyo tayari master plan-chenge , mzee wa havard a.k.a mzee wa vijisenti tayari alikuwa kashamaliza zitto na kuwaokoa woote wakina maswi, werema, muhongo etc,

unajua kwanini???

Kwa yale maelezo ya kuframe ya chenge means tayari hawa watu woote ambao si uteuzi wa bunge,tayari walikuwa wanahamishiwa katika mamlaka iliyowateua ambayo ni raisi, na hapo ndipo wapinzani woote walikuwa wanapigwa bao, means mashitaka na ushauri wa bunge ulikuwa hauna nguvu tena kusema mbona fulani hajawajibishwa na rais maana hayo ni maamuzi yake rais akijisikia kuwawajibisha au la ni sawa, so hapa zitto aliwaza km 50, chenge akaenda 100 km but mbowe akaenda mbali zaidi yao woote 200km, coz bila hivyo tayari bunge lilikuwa halina nguvu tena kuwafuatilia watu hao. Na mbowe alimjulisha fasta Zitto kuwa hii imekula kwetu ndio maana mama makinda alipo mpa tena nafasi zitto kuongea akajifanya amechoka ili kupoteze akuwa wameshtukia hilo chezo...Na mchongo huo ccm ulipangwa ili badae raisi angepotezea tu na hakuna wakuwajibishwa wala bunge lisingekuwa na nguvu tena na watu hao kuwahoji hata kuwafuatilia tena.. So mbowe alishtuka mchezo huo... Ndio maana hata ukiwa makini kuangalia tangu mwanzo wakina simbachawene na mama kaiuruki walikuwa wanataka kumaliza mechi mapemaaaaa kabisaaa
kwa kumwambia makinda aridhie pendekezo la serikali no 7 la kusema kuwa kwa kila mteule wa raisi bunge lishauri tu kuwa watu hao wakithibitika wana makosa basi maamuzi yafanyike na mamlaka ya uteuzi, hivyo ilikuwa ni bunge linashauri tu so uamzi ungebaki kwa serikali kuchukua hatua ama la, na jk alishajipanga kupiga danadana kwa kujikita kusubiri ripoti za kimamlaka juu ya uchunguzi, na hilo lingefika hadi mwakani july bunge kuvunjwa..
 
Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
855
195
dah!aisee mimi sikuusoma mchezo wa zitto...big up zitto wewe ni hazina kubwa kwa Taifa hili....
 
Target ya Zitto ilikuwa waziri mkuu, kama waziri mkuu angewajibishwa basi serikali nzima ilikuwa haipo, maana yake Rais angepanga upya baraza lake, Sasa isingekuwa rahisi tena kwa kina muhongo kurudi kwenye nafasi zao, na kama wangerudi basi CCM ndio ilikuwa inakwenda kupasuka msamba
 
Last edited by a moderator:

Eistein

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,107
1,195
Kiukweli mchezo umekuwa mgumu kama Mbowe angekubali yaishe tulikywa tumewaweza ccm
mkuu zito anauwezo binafsi sipingi- lakini hata hivyo tayari master plan-chenge , mzee wa havard a.k.a mzee wa vijisenti tayari alikuwa kashamaliza mchezo na zitto alidhani tayari kamkamata na waziri mkuu ndani ya nyavu lakini chenge mission yake ile ilikuwa ni ya kuwaokoa woote wakina maswi, werema, muhongo etc,

unajua kwanini???

Kwa yale maelezo ya kuframe ya chenge means tayari hawa watu woote ambao si uteuzi wa bunge,tayari walikuwa wanahamishiwa katika mamlaka iliyowateua ambayo ni raisi kwa kuchukuliwa hatua, na hapo ndipo wapinzani woote walikuwa wanapigwa bao, means mashitaka na ushauri wa bunge ulikuwa hauna nguvu tena kusema mbona fulani hajawajibishwa na rais maana hayo ni maamuzi yake rais akijisikia kuwawajibisha au la ni sawa, so hapa zitto aliwaza km 50, chenge akaenda 100 km but mbowe akaenda mbali zaidi yao woote 200km, coz bila hivyo tayari bunge lilikuwa halina nguvu tena kuwafuatilia watu hao. Na mbowe alimjulisha fasta Zitto kuwa hii imekula kwetu ndio maana mama makinda alipo mpa tena nafasi zitto kuongea akajifanya amechoka ili kupoteze akuwa wameshtukia hilo chezo...Na mchongo huo ccm ulipangwa ili badae raisi angepotezea tu na hakuna wakuwajibishwa wala bunge lisingekuwa na nguvu tena na watu hao kuwahoji hata kuwafuatilia tena.. So mbowe alishtuka mchezo huo... Ndio maana hata ukiwa makini kuangalia tangu mwanzo wakina simbachawene na mama kaiuruki walikuwa wanataka kumaliza mechi mapemaaaaa kabisaaa
kwa kumwambia makinda aridhie pendekezo la serikali no 7 la kusema kuwa kwa kila mteule wa raisi bunge lishauri tu kuwa watu hao wakithibitika wana makosa basi maamuzi yafanyike na mamlaka ya uteuzi, hivyo ilikuwa ni bunge linashauri tu so uamzi ungebaki kwa serikali kuchukua hatua ama la, na jk alishajipanga kupiga danadana kwa kujikita kusubiri ripoti za kimamlaka juu ya uchunguzi, na hilo lingefika hadi mwakani july bunge kuvunjwa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom