Zitto alitabiriwa na sasa imetimia

wakuwaza

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
315
79
Nimekuwa nikisoma habari hizi za usaliti kw amuda mrefu kutoka kwa waandishi mbalimbali. Wengi sana, pamoja na rafiki yake Absalom Kibanda, walimtabiria zitto, na sasa utabiri wao umetimia. Mfano msome huyu hapa chini aliyeandika katika gazeti la RAI:

CHADEMA inapovamiwa na ‘duduwasha’
Ijumaa, Desemba 28, 2012 05:43
Na Egbert Mkoko

MIEZI tisa iliyopita katika safu hii, niliwahi kuandika makala kuwa Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kutoa wanasiasa mahiri ambao baadae hugeuka ‘vigeugeu’. Nilitoa mifano kadhaa. Naomba nirejee sehemu ya makala ile, na kisha mwisho wa makala hii, nitaeleza kwanini nimerudia kuelezea haya.

Sehemu ya makala hiyo ilikuwa inasema;

Sina shaka utakubaliana nami kuwa Mkoa wa Kigoma ni kitovu cha upinzani nchini Tanzania. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa kipindi cha karibu miaka 20 sasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, mkoa huu umekuwa chachu ya mafanikio katika upinzani.

Kwa haraka haraka, sina shaka wapo wanaokumbuka namna Dk. Aman Walid Kabourou alivyokisumbua Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambapo wakati huo akiwa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) alipambana vikali na Azim Premji kuanzia katika sanduku la kura hadi mahakamani.

Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, ulishuhudia Mkoa wa Kigoma ukiwa moja ya mikoa iliyotoa wabunge wengi kuwakilisha upinzani. Bila shaka ni kutokana na kile kilichoonekana kama mkoa huu kutengwa katika mipango mbalimbali ya maendeleo inayowekwa na serikali ya CCM.

Haikuwa ajabu kwa Dk. Kabourou hatimaye mwaka huo kutinga bungeni akiwakilisha CHADEMA kwani tayari alikuwa ni moto wa kuotea mbali na alionekana kama mkombozi wa kweli wa matatizo ya watu wa Kigoma mjini.

Moto huo wa upinzani mkoani Kigoma mwaka 1995 ukasambaa zaidi na kutinga jimbo la Kasulu Mashariki ambapo Daniel Nsazugwako alichaguliwa kuwa Mbunge akipitia NCCR-Mageuzi, chama ambacho kwa mwaka huo, ndicho kilichopata wabunge wengi zaidi wa upinzani kwa upande wa Tanzania Bara.

Kutokana na kukomaa huko kwa hisia za mapinduzi ya kisiasa kwa wana-Kigoma, haikushangaza kwa CHADEMA kumpa cheo kikubwa Dk. Kabourou ambaye alikuwa Katibu mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa.

Safari ya kuikomboa Kigoma kupitia upinzani iliendelea mwaka 2000 ambapo Jimbo la Kigoma Kusini lilimchagua GulamHussein Kiffu kuwa Mbunge wake na wakati huo akiwakilisha chama cha NCCR-Mageuzi. Kiffu alikuwa mmoja wa wabunge wachache sana wa NCCR ambao walichaguliwa mwaka huo wa 2000 ikiwa ni baada ya chama hicho kupigwa na kombora la kisiasa na kuanza kupepesuka. Hata hivyo, ubunge wa Kiffu ulikoma miaka miwili baadae baada ya kuondolewa na mahakama.

Mwaka 2005 Kigoma iliyumba kidogo, lakini safari hii naweza kudiriki kusema mkoa huu ulilamba dume kwa kumpata mwanasiasa kijana na machachari Zitto Zuberi Kabwe aliyechaguliw akuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA.

Moto ambao ulionekana kufifia mwaka 2005, uliwaka kwa kasi ya ajabu mwaka 2010 ndani ya mkoa huo wa Kigoma baada ya majimbo matano kuangukia mikoni mwa wapinzani. CHADEMA ikapata jimbo moja na NCCR ambao ni kama watawala wa upinzani mkoani humo wakaibuka na majimbo manne.

Kati ya majimbo ambayo wapinzani walitwaa mwaka 2010 ni pamoja na Muhambwe ambapo Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) aliibuka mbabe, Kigoma Kusini ikachukuliwa na rafiki yangu David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Zitto akiendela kutawala Kigoma Kaskazini.

Naamini hadi hapo utakuwa umekubaliana nami kuwa Kigoma ni kitovu cha upinzani hapa Tanzania. Hii ni kutokana na kila uchaguzi kuhakikisha kuwa mkoa huu haukosi mbunge ama wabunge wa upinzani tena wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe. Lakini waswahili husema ‘kwenye msafara wa mamba, hata kenge na mijusi hawakosekani pia.’

Wapinzani wengi kutoka mkoa wa Kigoma wamekuwa kama ‘vigeugeu’ huku wakileta mkanganyiko mkubwa katika siasa za Tanzania. Mkanganyiko huu umekuwa ukijitokeza ama ndani ya vyama vyao vya siasa ama hata kuhama toka chama kimoja kwenda kingine (na wengine kurudi CCM).

Dk. Kabourou, mwamba wa upinzani mkoani Kigoma katika miaka ya 90, alishika nafasi kubwa ya uongozi ndani ya CHADEMA miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Ni msomi aliyebobea. Lakini kisiasa leo hii Dk. Kabourou ni mwana-CCM shupavu. Je, huyu bwana alikuwa mpinzani wa kweli, au alikuwa anapita tu CHADEMA enzi hizo? Nauliza tu!

Nsazugwako alikuwa mwana-NCCR mzuri na aliwawakilisha vizuri wananchi wake bungeni mwaka 1995. Lakini mwaka 2005 akaibukia CCM kuwania ubunge na hatimaye akapata hadi uwaziri mdogo. Akitokea kulekule Kigoma, nauliza huyu Nsazugwako naye alikuwa mpinzani wa kweli ama pia alikuwa ana lake jambo?

Gulamhusein Kiffu naye hayuko nyuma katika mkumbo wa wenzake. Alionja ubunge kwa miaka miwili kupitia NCCR Mageuzi kabla ya Mahakama kumuondoa. Kuona hivyo akaamua kujaribu tena kurudi bungeni 2010 lakini kupitia CCM ambako hakufaulu. Nauliza tena, huyu alikuwa mpinzani halisi ama msaliti wa upinzani?

Hao ni wana-Kigoma ‘waliotesa wakiwa wapinzani’ ambao kwa sasa wote ‘wanakula bata CCM’. Wapo wale ambao bado ni wapinzani, lakini wamekuwa wakizua mkanganyiko kila uchao ndani ya upinzani.

Tujikumbushe. Rafiki yangu David Kafulila kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR mageuzi ingawa mwanzo alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA. Alifutwa katika cheo hicho na kisha mwenyewe kuamua kukimbilia NCCR. Waswahili husema ‘ Mjasiri haachi asili.’ Hata baada ya kwenda NCCR na kupata ubunge, Kafulila amekuwa na asili ile ile ya wa-Kigoma wenzake ambayo imeuweka ubunge wake (na uanachama wa NCCR) rehani hadi sasa ukisubiri wokovu wa mahakama.

Felix Mkosamali kutoka Mhambwe, naye alianza kufuata nyendo zile zile za ‘mzoefu’ Kafulila. Lakini NCCR ikamfunga ‘speed governor’ mapema na walau kwa sasa anaonekana ametulia. Labda pia na umri ulikuwa bado unasumbua.

Zitto Kabwe! Nashindwa hata nianzie wapi kuelezea. Amekuwa haishiwi vituko kila wakati tangu mwaka 2005 hadi kesho!

Nimeamua kuishia hapa huku nikiamini umepata kile nilichokieleza katika makala yangu ya miezi tisa iliyopita. Sasa kwanini nimerudia kuzungumzia jambo hii tena?

Nianzie ilipoishia. Zitto amekuwa ni mwanasiasa ambaye haaminiki sana ndani ya CHADEMA yenyewe, ilifikia hatua ya wabunge wenzake kutaka kumvua u-naibu kiongozi wa upinzani bungeni kabla ya busara za kina Dk. Kitila Mkumbo kusaidia kuweka mambo sawa.

Hivi majuzi Zitto alikuja na mkakati wake wa kuutaka urais wa Tanzania 2015 huku akidaiwa kuwa na ushiriki finyu kwenye harakati za kujenga chama kupitia M4C! Taarifa za wiki iliyopita, zimekuwa zikimhusisha Zitto na Kafulila na uanzishwaji wa Chama kipya cha siasa.

Aidha, Zitto pia akishirikiana na baadhi ya vijana wanaomuunga mkono ndani ya Chadema, wamekuwa wakituhumiwa kukivuruga chama chao kwa mbinu mbalimbali. Mbinu kubwa inayodaiwa kutumika ni ile ya ‘divide and rule’ kwa lengo la kumtayarishia njia kiongozi huyo kuwania Uenyekiti wa CHADEMA taifa katika uchaguzi ujao na kisha kuwania Urais wa Tanzania kama alivyokwishatangaza.

Kilichonisukuma zaidi kuandika yote haya, ni kauli ya mwisho aliyotoa Zitto kuwa tuhuma zote hizi ni uzushi wa kumchafulia jina lake, na kwamba kwa namna yoyote iwavyo ‘Kumchafua ama kumharibia Zitto ni kuiharibia na kuichafua CHADEMA yote’.

Ni wazi kauli hii inaonyesha kuwa ‘Zitto ndio CHADEMA na CHADEMA ni Zitto’. Majigambo haya naweza kuyaita ni ‘jeuri ya kisiasa’ ya mtu mmoja kujiona kuwa ana umuhimu mkubwa kuliko wanachama wengine wote na ndio pekee kashikilia uhai wa chama husika.

‘Jeuri ya kisiasa’ ya kiwango hiki, ni hatari kwa uhai wa chama chochote. Pia inapofikia wafuasi wa mwanasiasa huyu wanawatukana hadharani viongozi wa juu bila ya ‘bosi’ wao kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwakemea, hiyo ni hatari zaidi.

Nikiwa nafikiria haya, ndipo nikamkumbuka Dk. Kabourou aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ni Mkigoma pia, aliyeondoka chamani na kurudi CCM na chama alichoondoka kikabaki imara.

Sina Hakika kama Zitto atafuata nyayo za Dk. Kabourou au la! licha ya mwenyewe kusema haamini katika kuhamahama vyama. Lakini wanasiasa wenzake (Kafulila, Kiffu na Nsanzugwako) wanaweza kutoa picha kuwa CHADEMA ijiandae kwa lolote toka kwa mwanasiasa huyu Mkigoma kama walivyowahi kufanya Wakigoma wenzie.

Vinginevyo, huu ni wakati wa chama hicho kusafisha nyumba yake na kuondoa ‘duduwasha’ ambao wasipodhibitiwa, nyumba haitakalika.

Email: njali5@yahoo.com
 
Mods watakuja kuifagia thread sasa hivi,sijui ofisi za jf za u-mod zimehamia Mwandinga kwa muda??!!

Binafsi nshatundika threads 3 zenye reliable source kuhusu Zitto na mradi wake wa undumi la kuwili lakini haikuchukua dakika katika siku tofauti tofauti kufutwa!!
 
Umeongea kweli tupu mkuu,hili duduwasha lazima ling'olewe mapema iwezekanavyo.CDM si kichaka cha madudu washa hata kidogo!
 
zitto ataumiza bure hafukuziki chadema hakuna mwenye hiyo jeuri mtafanya mambo yote lakini hakuna mtakachopata mtaambulia aibu.
 
Zzk goo,gooo zito,
Walaaniwe wasaliti wote wa Chama cha Dekokrasia na Maendeleo.
Mungu ibariki CDM,Mungu ibariki Tanzania.
 
Amina! Umenena vyema mkuu. Siku zote mtu shupavu husimamie msimamo wake,CDM mko sahihi simamieni hapo hapo,kama huyu zitto ni kumfuta uachama kabisa. Atajisifia sana mpaka kuharibu chama kama ataachwa abaki CDM,mchawi huyu wa kuwanga kabisa siyo bure.
 
b
Comrade JULIUS MALEMA most feared polician in south africa. But now is down and out same thing will happen to ZITTO

Malema kwa south bado ana nguvu sana na tena kwa sasa kaazisha chama chake kipya na vijana wengi wana kadi zake hasa wafanyakazi wa migodini,madereva tax,dalala,wafanyakazi wa mashiriki ya umma,wanamziki,na kibaya zaidi kaanza kuibua tuhuma za mkuu wa nchi kumiliki jumba kubwa la kifahari pamoja na hayo bado ANC iko imara ajabu nadhani ni ujana tu na ile kujiona yeye ndiyo mhimili wa siasa za south africa.

Ikumbukwe j,malema ndiyo aliesababisha rais thabo mbeki kuondolewa madarakani ili rafiki yake akamate hatamu za nchi huyu ni jacob zuma ila leo zuma ndiyo anamuadabisha malema mpk kasababisha jumba lake la kihari kuuzwa kwa bei ya kutupa.

mwisho nisema anachofanya zitto sio siasa bali ni kukomoana na huo ni ushamba wa siasa za kizazi hiki kikubwa ni kukubaliana na viongozi wako wa chama ili maisha yaendelee kuliko kuonekana msaliti asbh asbh na mwisho wa siku jioni tunafunga hesabu
 
Du!! wanasiasa wa Kigoma kweli hawaaminiki ni wanafiki na wasaliti wakubwa, Kabourou pamoja na kuwa msomi na licha ya kuwa katibu mkuu wa chama enzi hizo lakini bado alitumika na kurudi CCM,huyu naye pamoja na usomi wake pamoja na kuwa naibu katibu mkuu wa chama tena akiwa na umri mdogo naye anatumika na Ma CCM kama Kabourou huku akijiandaa kurudi CCM.
 
Nimekuwa nikisoma habari hizi za usaliti kw amuda mrefu kutoka kwa waandishi mbalimbali. Wengi sana, pamoja na rafiki yake Absalom Kibanda, walimtabiria zitto, na sasa utabiri wao umetimia. Mfano msome huyu hapa chini aliyeandika katika gazeti la RAI:

CHADEMA inapovamiwa na ‘duduwasha’
Ijumaa, Desemba 28, 2012 05:43
Na Egbert Mkoko

MIEZI tisa iliyopita katika safu hii, niliwahi kuandika makala kuwa Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kutoa wanasiasa mahiri ambao baadae hugeuka ‘vigeugeu’. Nilitoa mifano kadhaa. Naomba nirejee sehemu ya makala ile, na kisha mwisho wa makala hii, nitaeleza kwanini nimerudia kuelezea haya.

Sehemu ya makala hiyo ilikuwa inasema;

Sina shaka utakubaliana nami kuwa Mkoa wa Kigoma ni kitovu cha upinzani nchini Tanzania. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa kipindi cha karibu miaka 20 sasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, mkoa huu umekuwa chachu ya mafanikio katika upinzani.

Kwa haraka haraka, sina shaka wapo wanaokumbuka namna Dk. Aman Walid Kabourou alivyokisumbua Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambapo wakati huo akiwa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) alipambana vikali na Azim Premji kuanzia katika sanduku la kura hadi mahakamani.

Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, ulishuhudia Mkoa wa Kigoma ukiwa moja ya mikoa iliyotoa wabunge wengi kuwakilisha upinzani. Bila shaka ni kutokana na kile kilichoonekana kama mkoa huu kutengwa katika mipango mbalimbali ya maendeleo inayowekwa na serikali ya CCM.

Haikuwa ajabu kwa Dk. Kabourou hatimaye mwaka huo kutinga bungeni akiwakilisha CHADEMA kwani tayari alikuwa ni moto wa kuotea mbali na alionekana kama mkombozi wa kweli wa matatizo ya watu wa Kigoma mjini.

Moto huo wa upinzani mkoani Kigoma mwaka 1995 ukasambaa zaidi na kutinga jimbo la Kasulu Mashariki ambapo Daniel Nsazugwako alichaguliwa kuwa Mbunge akipitia NCCR-Mageuzi, chama ambacho kwa mwaka huo, ndicho kilichopata wabunge wengi zaidi wa upinzani kwa upande wa Tanzania Bara.

Kutokana na kukomaa huko kwa hisia za mapinduzi ya kisiasa kwa wana-Kigoma, haikushangaza kwa CHADEMA kumpa cheo kikubwa Dk. Kabourou ambaye alikuwa Katibu mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa.

Safari ya kuikomboa Kigoma kupitia upinzani iliendelea mwaka 2000 ambapo Jimbo la Kigoma Kusini lilimchagua GulamHussein Kiffu kuwa Mbunge wake na wakati huo akiwakilisha chama cha NCCR-Mageuzi. Kiffu alikuwa mmoja wa wabunge wachache sana wa NCCR ambao walichaguliwa mwaka huo wa 2000 ikiwa ni baada ya chama hicho kupigwa na kombora la kisiasa na kuanza kupepesuka. Hata hivyo, ubunge wa Kiffu ulikoma miaka miwili baadae baada ya kuondolewa na mahakama.

Mwaka 2005 Kigoma iliyumba kidogo, lakini safari hii naweza kudiriki kusema mkoa huu ulilamba dume kwa kumpata mwanasiasa kijana na machachari Zitto Zuberi Kabwe aliyechaguliw akuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA.

Moto ambao ulionekana kufifia mwaka 2005, uliwaka kwa kasi ya ajabu mwaka 2010 ndani ya mkoa huo wa Kigoma baada ya majimbo matano kuangukia mikoni mwa wapinzani. CHADEMA ikapata jimbo moja na NCCR ambao ni kama watawala wa upinzani mkoani humo wakaibuka na majimbo manne.

Kati ya majimbo ambayo wapinzani walitwaa mwaka 2010 ni pamoja na Muhambwe ambapo Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) aliibuka mbabe, Kigoma Kusini ikachukuliwa na rafiki yangu David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Zitto akiendela kutawala Kigoma Kaskazini.

Naamini hadi hapo utakuwa umekubaliana nami kuwa Kigoma ni kitovu cha upinzani hapa Tanzania. Hii ni kutokana na kila uchaguzi kuhakikisha kuwa mkoa huu haukosi mbunge ama wabunge wa upinzani tena wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe. Lakini waswahili husema ‘kwenye msafara wa mamba, hata kenge na mijusi hawakosekani pia.’

Wapinzani wengi kutoka mkoa wa Kigoma wamekuwa kama ‘vigeugeu’ huku wakileta mkanganyiko mkubwa katika siasa za Tanzania. Mkanganyiko huu umekuwa ukijitokeza ama ndani ya vyama vyao vya siasa ama hata kuhama toka chama kimoja kwenda kingine (na wengine kurudi CCM).

Dk. Kabourou, mwamba wa upinzani mkoani Kigoma katika miaka ya 90, alishika nafasi kubwa ya uongozi ndani ya CHADEMA miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Ni msomi aliyebobea. Lakini kisiasa leo hii Dk. Kabourou ni mwana-CCM shupavu. Je, huyu bwana alikuwa mpinzani wa kweli, au alikuwa anapita tu CHADEMA enzi hizo? Nauliza tu!

Nsazugwako alikuwa mwana-NCCR mzuri na aliwawakilisha vizuri wananchi wake bungeni mwaka 1995. Lakini mwaka 2005 akaibukia CCM kuwania ubunge na hatimaye akapata hadi uwaziri mdogo. Akitokea kulekule Kigoma, nauliza huyu Nsazugwako naye alikuwa mpinzani wa kweli ama pia alikuwa ana lake jambo?

Gulamhusein Kiffu naye hayuko nyuma katika mkumbo wa wenzake. Alionja ubunge kwa miaka miwili kupitia NCCR Mageuzi kabla ya Mahakama kumuondoa. Kuona hivyo akaamua kujaribu tena kurudi bungeni 2010 lakini kupitia CCM ambako hakufaulu. Nauliza tena, huyu alikuwa mpinzani halisi ama msaliti wa upinzani?

Hao ni wana-Kigoma ‘waliotesa wakiwa wapinzani’ ambao kwa sasa wote ‘wanakula bata CCM’. Wapo wale ambao bado ni wapinzani, lakini wamekuwa wakizua mkanganyiko kila uchao ndani ya upinzani.

Tujikumbushe. Rafiki yangu David Kafulila kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR mageuzi ingawa mwanzo alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA. Alifutwa katika cheo hicho na kisha mwenyewe kuamua kukimbilia NCCR. Waswahili husema ‘ Mjasiri haachi asili.’ Hata baada ya kwenda NCCR na kupata ubunge, Kafulila amekuwa na asili ile ile ya wa-Kigoma wenzake ambayo imeuweka ubunge wake (na uanachama wa NCCR) rehani hadi sasa ukisubiri wokovu wa mahakama.

Felix Mkosamali kutoka Mhambwe, naye alianza kufuata nyendo zile zile za ‘mzoefu’ Kafulila. Lakini NCCR ikamfunga ‘speed governor’ mapema na walau kwa sasa anaonekana ametulia. Labda pia na umri ulikuwa bado unasumbua.

Zitto Kabwe! Nashindwa hata nianzie wapi kuelezea. Amekuwa haishiwi vituko kila wakati tangu mwaka 2005 hadi kesho!

Nimeamua kuishia hapa huku nikiamini umepata kile nilichokieleza katika makala yangu ya miezi tisa iliyopita. Sasa kwanini nimerudia kuzungumzia jambo hii tena?

Nianzie ilipoishia. Zitto amekuwa ni mwanasiasa ambaye haaminiki sana ndani ya CHADEMA yenyewe, ilifikia hatua ya wabunge wenzake kutaka kumvua u-naibu kiongozi wa upinzani bungeni kabla ya busara za kina Dk. Kitila Mkumbo kusaidia kuweka mambo sawa.

Hivi majuzi Zitto alikuja na mkakati wake wa kuutaka urais wa Tanzania 2015 huku akidaiwa kuwa na ushiriki finyu kwenye harakati za kujenga chama kupitia M4C! Taarifa za wiki iliyopita, zimekuwa zikimhusisha Zitto na Kafulila na uanzishwaji wa Chama kipya cha siasa.

Aidha, Zitto pia akishirikiana na baadhi ya vijana wanaomuunga mkono ndani ya Chadema, wamekuwa wakituhumiwa kukivuruga chama chao kwa mbinu mbalimbali. Mbinu kubwa inayodaiwa kutumika ni ile ya ‘divide and rule’ kwa lengo la kumtayarishia njia kiongozi huyo kuwania Uenyekiti wa CHADEMA taifa katika uchaguzi ujao na kisha kuwania Urais wa Tanzania kama alivyokwishatangaza.

Kilichonisukuma zaidi kuandika yote haya, ni kauli ya mwisho aliyotoa Zitto kuwa tuhuma zote hizi ni uzushi wa kumchafulia jina lake, na kwamba kwa namna yoyote iwavyo ‘Kumchafua ama kumharibia Zitto ni kuiharibia na kuichafua CHADEMA yote’.

Ni wazi kauli hii inaonyesha kuwa ‘Zitto ndio CHADEMA na CHADEMA ni Zitto’. Majigambo haya naweza kuyaita ni ‘jeuri ya kisiasa’ ya mtu mmoja kujiona kuwa ana umuhimu mkubwa kuliko wanachama wengine wote na ndio pekee kashikilia uhai wa chama husika.

‘Jeuri ya kisiasa’ ya kiwango hiki, ni hatari kwa uhai wa chama chochote. Pia inapofikia wafuasi wa mwanasiasa huyu wanawatukana hadharani viongozi wa juu bila ya ‘bosi’ wao kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwakemea, hiyo ni hatari zaidi.

Nikiwa nafikiria haya, ndipo nikamkumbuka Dk. Kabourou aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ni Mkigoma pia, aliyeondoka chamani na kurudi CCM na chama alichoondoka kikabaki imara.

Sina Hakika kama Zitto atafuata nyayo za Dk. Kabourou au la! licha ya mwenyewe kusema haamini katika kuhamahama vyama. Lakini wanasiasa wenzake (Kafulila, Kiffu na Nsanzugwako) wanaweza kutoa picha kuwa CHADEMA ijiandae kwa lolote toka kwa mwanasiasa huyu Mkigoma kama walivyowahi kufanya Wakigoma wenzie.

Vinginevyo, huu ni wakati wa chama hicho kusafisha nyumba yake na kuondoa ‘duduwasha’ ambao wasipodhibitiwa, nyumba haitakalika.

Email: njali5@yahoo.com

Ushamaliza na hekaya yako nenda kwa mbowe ukapokee bahasha yako
 
uliweka post hii unamatatizo yaani unafananisha power ya zitto na kaburu? Yaani nyie chadema kweli hamfikirii mnawaza maandamano tu. Yaani zito kabla kufukuzwa balaa je akifikuzwa ? Fikirieni nyie watu mnauwa chama hicho, kumfukuza zitto ni sawa na kung!oa jino bila ganzi utaumia wewe
 
Back
Top Bottom