Zitto alipuka posho za wabunge kuongezeka kimya kimya

Kwa nini watu mnapenda sana kuzungumzia WATU.. swala hapa ni ongezeko la posho lakini sioni maoni yoyote yanayohusiana na posho kwa nini zimeongezwa, lini na zimepitishwa vipi ili nasi tuelewe, lakini badala yake anazungumwa Zitto kama vile yeye ndio kaleta posho..Huyu Zitto huyu ananyima wengi usingizi eeeeh!
 
Zitto analolisema ni kweli iko siku wananchi watawapiga mawe wabunge. Nilishawahi kusema nyuma hakuna mzalendo kwenye suala la posho bungeni zaidi ya Zitto mtake msitake. Si Magamba wala magwanda wote wachumia tumbo isipokuwa Zitto peke yake. Leo serikali inachechemea kulipa hata mishahara ya wafanyakazi wake lakini inawalipa posho nono wabunge kweli nchi yetu imekosa vipaumbele kabisa.
 
[h=1]Zitto na Demokrasia[/h] Zitto na Demokrasia

[h=2]Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi[/h] with 9 comments
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
 
Mi nilidhani kwa sera ya Kilimo kwanza maafisa kiimo wa wilaya na mkoa ndio watapandishiwa hata japo kwa 20% mishahara na posho zao.

Wabunge wanatakiwa waombe kiundwe chombo huru nje ya buge kiwe na jukumu la kurevieew stahiki zao. La sivyo tutabaki tunawashangaa tu

Napenda kujua kiprotcol za kazi na majukumu na umuhimu na ukubwa ni ipi kazi muhimu kati ya
  • mbunge na afisa eimu wa wilaya au mkoa
  • mbunge na afisa maji ,mifugo, afya wa wilaya au mkoa
  • mbunge na RPC wa mkoa
  • mbuge na mhandisi wa mkoa au wilaya
 
Usanii mtupu.
Solution sio kusema posho zisipandishwa bali ni kuweka sheria itakayowakataza wabunge kujipangia posho na mishahara yao.
Mtu yeyote ukimruhusu kujipangia mshahara lazima ajipe fungu nono.
 
Zitto kashiba tele, hana haja ya vijibosho vya kibunge! Kuna magamba ambao wanamweka hapo mjini!
 
Zitto kashiba tele, hana haja ya vijibosho vya kibunge! Kuna magamba ambao wanamweka hapo mjini!
It dont matter,

Kwanini hauamini kwamba he is doing it for the people?

Regardless of the reason,we huoni ni jambo la maana sana anapotetea maslahi ya wananchi?

Ndo shida ya watanzania kila mtu mwanasiasa!
 
Jamani hili ongezeko ni kubwa mno angalia kutoka Tshs 70,000/= hadi Tsha 200,000/= kwa siku

hapa linganisha na mshahara wa mwalimu mwenye TGTS C take home yake haizidi 180,000/= kwa mwenzi

Kimsingi, katika nchi hii tumegeukana gap la wenye nacho na masikini linazidi kuongezeka mno ils " poa tu !! "
 
Huyu Zitto ndio maana wenzake wanampiga vita, watu wamepigania kuingia bungeni kwaajili ya hizo posho halafu yeye anazipiga vita. Mi naona tumuulize SUGU na WENGE kama wanakubaliana na hili.
 
Bado wananchi haijatuuma ipasavyo.Hizi posho ziendelee kupanda mpaka zaid ya mil 1 kwa siku ili wananchi ituume tuonyeshe reaction madhubuti.
 
Hata YESU alitabiri kuwa nyakati za mwisho upendo kati ya ndugu utapungua na watu watajipenda wenyewe.
 
Zitto ni Mbunge makini sana.

Mambo mengi anayopigania baadae yanakuja kumake sense ingawa mwanzoni wengi watapinga.

Hili suala la wabunge kujiongezea marupurupu tena kimyakimya, tena kabla Rais hajaridhia hayo mabadiliko
ni dhahiri linatia wasiwasi wa nia ya dhati ya wabunge wetu.

Huku mwalimu akilipwa 180,000 kwa kufundisha kwenye mazingira magumu, wao wanapokea 200,000 kwa
"kukaa" wakati mbunge tangu unapogombea unajua kabisa kazi yako kubwa ni vikao. Na mshahara wa ubunge
anaujua.

Kwa nchi zilizoendelea kama U.S., iwapo bunge litapendekeza ongezeko la mishahara au posho, basi hilo
ongezeko likishapita, linakua frozen na litaanza kutumika katika bunge lijalo(kwa maana baada ya uchaguzi mkuu
utakaofuata) hii inasaidia sana kudhibiti conflict of interest na kuhakikisha mapendekezo yanayotolewa yanaakisi
ongezeko la gharama halisi za maisha.

Nafkiri Mheshmiwa Zitto ungetusaidia sana kama ungepeleka muswada binafsi wa sheria unaokataza viwango vipya
vya mishahara/posho vitakavyopitishwa na bunge lililopo kuanza kutumika ndani ya kipindi chao, na badala yake vianze
kutumika katika bunge litakalofuatia. Hii itasaidia sana kudhibiti ulafi tulionao kama watanzania.
 
Back
Top Bottom