Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Wakuu, habari za mwisho wa wiki. Natumai mambo yalienda vizuri.
Nakumbuka hoja ya Zitto ya kusema kwamba Pinda alikuwa akilia akiwa Mkuu wa serikali pale alipoulizwa Bungeni kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zake. Binafsi, niliguswa na chozi la Pinda nikiwa mdau wa masuala ya haki za binadamu. Awali, nilikuwa kinyume na wengi waliomshutumu Pinda kwa kufanya siasa. Hata hivyo, jana aliacha shughuli zake na kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye chakula cha Mengi na watu wenye ulemavu. Hii ilikuwa mara ya kwanza tangu Mengi aanzishe mpango huu kumuona Waziri Mkuu akiwa mgeni rasmi. Wengi huwa wanakimbia na kulidharau kundi hili.
Katika hafla hiyo, nimemsikia akiongea mengi na muhimu, akiwaonyesha kuguswa sana na watu wenye ulemavu. Wale waliomshutumu awali wanapaswa kumwomba radhi Waziri Mkuu.