Zitto alikosea aliposema Pinda analilia Uwaziri Mkuu-Pinda have passion to Disabled

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu, habari za mwisho wa wiki. Natumai mambo yalienda vizuri.

Nakumbuka hoja ya Zitto ya kusema kwamba Pinda alikuwa akilia akiwa Mkuu wa serikali pale alipoulizwa Bungeni kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zake. Binafsi, niliguswa na chozi la Pinda nikiwa mdau wa masuala ya haki za binadamu. Awali, nilikuwa kinyume na wengi waliomshutumu Pinda kwa kufanya siasa. Hata hivyo, jana aliacha shughuli zake na kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye chakula cha Mengi na watu wenye ulemavu. Hii ilikuwa mara ya kwanza tangu Mengi aanzishe mpango huu kumuona Waziri Mkuu akiwa mgeni rasmi. Wengi huwa wanakimbia na kulidharau kundi hili.

Katika hafla hiyo, nimemsikia akiongea mengi na muhimu, akiwaonyesha kuguswa sana na watu wenye ulemavu. Wale waliomshutumu awali wanapaswa kumwomba radhi Waziri Mkuu.
 
ZITTO amekuwa mropokaji tu siku hizi, anakufa kisiasa yule bwana hana analolisimia kwa umakini.
 
Wakuu,Habari za Week end.Natumai mabo yalienda vizuri.

Nakumbuka hoja ya Zitto ya kusema kwamba Pinda alikuwa akililia uwaizri Mkuu pale alipolia Bungeni wakati akilipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zake.Mimi bainafsi niliguswa na chozi la Pinda nikiwa kama mdau wa masuala ya haki za binadamu. Nilikuwa kinyume na wengi waliodai kwamba POinda alikuwa akifanya siasa.Lakini jana aliacha shughuli zake nyingine na kukubali kuwa guest of Honour kwenye chakula cha Mengi na watu wenye Ulemavu,ni mara ya kwanza tangu Mengi aanzishe mpango huu kumuona Waziri Mkuu akiwa mgeni rasmi,wengi hukimbia na kulidharau kundi hili.Katika hafla ile nimemsikia ameongea mengi na ya muhimu akioneshwa kuguswa sana watu wenye Ulemavu.Waliomsema kipindi kile alipolia Bungeni wamuombe radhi Waziri Mkuu.

Hata mi nilimwelewa sana kwamba Pinda anahuruma mno hasa baada ya kuhutubia watu wasifanye mauaji - kabla hata kajaondoka kesho yake wameua wengine as if wanamuonyesha who are you/ hata ukiwa wewe lazima unapata hisia ambayo inakufanya utoe matamshi ambayo wengine watayaita hatarishi kwa amani.

Wengine wakasema serikali imelia bungeni, anayelia ni pinda jamani yeye ni mtu kama sisi kwa hiyo tumwelewe na dhana yake ya kukomesha mauaji ya albino.

Kuonyesha anawajali walemavu wa ngozi pamoja na matatizo waliyonayo, kaamua kukachukua katoto kamoja ka albino amekafanya kuwa moja ya familia yake, na wengine wenye uwezo mfuate mfano wa waziri wenu mkuu.

Zitto ana matatizo yake, tumwelewe tu.
 
---Kuonyesha anawajali walemavu wa ngozi pamoja na matatizo waliyonayo, kaamua kukachukua katoto kamoja ka albino amekafanya kuwa moja ya familia yake, na wengine wenye uwezo mfuate mfano wa waziri wenu mkuu.

Zitto ana matatizo yake, tumwelewe tu.

Jumla ni watatu na huenda wakaongezeka.
 
Wakuu,Habari za Week end.Natumai mabo yalienda vizuri.

Nakumbuka hoja ya Zitto ya kusema kwamba Pinda alikuwa akililia uwaizri Mkuu pale alipolia Bungeni wakati akilipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zake.Mimi bainafsi niliguswa na chozi la Pinda nikiwa kama mdau wa masuala ya haki za binadamu. Nilikuwa kinyume na wengi waliodai kwamba POinda alikuwa akifanya siasa.Lakini jana aliacha shughuli zake nyingine na kukubali kuwa guest of Honour kwenye chakula cha Mengi na watu wenye Ulemavu,ni mara ya kwanza tangu Mengi aanzishe mpango huu kumuona Waziri Mkuu akiwa mgeni rasmi,wengi hukimbia na kulidharau kundi hili.Katika hafla ile nimemsikia ameongea mengi na ya muhimu akioneshwa kuguswa sana watu wenye Ulemavu.Waliomsema kipindi kile alipolia Bungeni wamuombe radhi Waziri Mkuu.

Kwani hawa wanasiasa nani haongei mazuri? Usidanganyike na mlo wa siku moja, hauwezi kumsaidia mlemavu.
 
Tulimweleza Zitto mapema ndani humu ila kama yeye hasikii sasa haya ni mambo yake na pia watu wa leo sio wale kwa kipindi kile cha mwaka 2000 hivi basi anapaswa kuchukua tahadhali kuwa sana
 
Jamani ukweli semeni, Pinda aliposema watu wachukue sheria mkononi kwa wanaoua maalbino ili alikosea, hapa upendo na huruma yake ilipitiliza kiasi cha waziri mkuu kutoa statement kama ile!

Pinda ana huruma, lakini kipindi kile si Zito peke yake alisema wengi sana tulisema, sijajua Zito hapa anaingiaje?

are you inferior kwa Zito? je Zito hakosei? Zito ni standard? is he SI unit? kwa nini unajishusha kuwa obsessed na Zitolism kiasi hiki? kwa nini usiseme waliosema pinda analilia uwaziri mkuu waombe msamaha? However. politics goes with time! tatizo nchi yetu kila kitu ni matatizo siyo albino tu, tuna vibaka, wabakaji, majambazi, n,k PM kutoa ile statement alikuwa anaruhusu wahalifu wowote wauawe hata wasio wahalifu kweli, nikizusha tu kamuua albino, basi lazima afe!.That was his worse statement from PM!

Achana na uzitolism, utashindwa kuona mbali, unajidharaulisha kuwa katika watanzania mil.40 zito tu ndio alisema hivyo?

jamani lets move forward lets discuss an issue! wewe umegundua lini kuwa pinda ana moyo mzuri? baada ya kwenda kwa Mengi? msimamo wako kipindi kile ulikuwa ni nini? je leo baada ya Pm kuhudhuria sherehe ya Mengi, unafikiri waliosema kuwa analilia uwaziri mkuu wameonaje? si wamejifunza kama wewe ulivyojifunza?

hatuwezi kujadili maada humu mpaka Zito awemo? au unafikiri thread yako ichangiwe lazima uweke neno zito? haya si matusi kwa sisi wengine?

ebu badilikeni, Tanzanian are many than single person called Zito! yeye ni binadamu ana mawazo, nia, kama wengine, sijaona mahali tunamtaja kama malaika!
 
Kwani hawa wanasiasa nani haongei mazuri? Usidanganyike na mlo wa siku moja, hauwezi kumsaidia mlemavu.

Ngekewa nadhani hujanielewa. Hoja hapa sio mlo na kwa taarifa yako chakula hiki hakijaandaliwana Pinda ni chakula cha Mengi na huwa anafanya hivi kila mwaka.Hoja hapani huruma za Pinda kwa watu wenye ulemavu. Soma hoja ujibu hoja.
 
Nilijua tu kama utajibu. Ukweli lazima usemwe na utabaki kuwa ukweli siku zote.

Kumbe mna yenu? please be careful kuweka mjadala wa wengi kama una beef na mtu, aibu hii!

your thread is real annoying! can you change the head at least? mkuu katika maisha yako yoote , ulisema sentensi zilizo correct, na pale ulipogundua uko wrong, kuna mtu alikuandika? can you post us any refernce ya kuwa Zito aliposema hivyo , wewe binafsi ulimpinga?

umekosea mkuu! neno zuri ninaloweza kusema kwa sasa, waaambie mods waitoe hii thread, is too low for us kujadili issue za nani alisema hivi miaka 5 iliyopita, leo yuko wrong!!
 
Ha ha! Waberoya kulikoni? Sina beef na mtu yeyote yule humu ndani ila ni hofu zako tu ndo zinakudanganya. Nilihisi huyu jamaa atajibu kwani kila thread inayomtaja Zitto ni lazima ajibu negatively asif Zittosi mwanadamu kwamba hakosei. Kama thread haina mashiko kwako achana nayo kwani umelazimishwa kijibu?
 
zitto alililia uenyekiti wa chama, baada ya kuukosa anaanza visa. mara JK aendelee, mara namsapoti kafulila, mara mimi si mwanasiasa, na mengine tusiyoyajua. kijana ni smart ila ajipange tu. uenyekiti si ishu
 
Back
Top Bottom