Zitto alia na Polisi waliochukua simu yake, ataka wafuasi wasipokee simu zake

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Anaandika Zitto Zuberi Kabwe katika ukurasa wake wa facebook

Ndugu, Jamaa na Marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 Jeshi la Polisi walichukua Simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao. Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu.

Nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo.

1) Nawakumbusha kuwa msitumie simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na Polisi

2) Katiba ya Nchi yetu kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu sana haki ya FARAGHA kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.

Nina mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na Simu yangu muda wote huu kwa sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo. Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( cybercrime act )
 
Pole ndugu zitto ndio madikteta walivyo.ukiangalia police ya Tanzania ya awamu ya 5 inavyofanya kaz.aina tofauti kabisa na ile ya Rwanda mambo ya kunyang'anyana cm au hata laptop hayakuwepo.cku iz utaskia hata office za mawakili zavamiwa watu wamechukua laptop na documents.

Nahitimisha kwa kusema ivi "cku ya kufa nyani miti yote huteleza" Mh mtukufu,cku yako ikifka hata ufanye nn utaondoka tuu kama Mugabe Zimbabwe.
 
Mimi na marafiki zake tukimwandikia sms,wanasoma wao! Kama ana kamchepuko,kakimwandikia sms,polisy wanajua na wataitumia kumuumiza! Unachunguza nini kwenye simu kwa almost mwezi?
Kama simu haitumiki kwa mipango ovu,wasiwasi wa zitto unatoka wapi?
 
Pole ndugu zitto ndio madikteta walivyo.ukiangalia police ya Tanzania ya awamu ya 5 inavyofanya kaz.aina tofauti kabisa na ile ya Rwanda mambo ya kunyang'anyana cm au hata laptop hayakuwepo.cku iz utaskia hata office za mawakili zavamiwa watu wamechukua laptop na documents. Nahitimisha kwa kusema ivi "cku ya kufa nyani miti yote huteleza" Mh mtukufu,cku yako ikifka hata ufanye nn utaondoka tuu kama Mugabe Zimbabwe.
Siku hizi Mugabe amekuwa role model wenu!kila jambo Mugabe sio tena Tundu Lissu au kenyatta
 
Mimi na marafiki zake tukimwandikia sms,wanasoma wao! Kama ana kamchepuko,kakimwandikia sms,polisy wanajua na wataitumia kumuumiza! Unachunguza nini kwenye simu kwa almost mwezi?
huwezi kuelekeza polisi nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom