mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, ameeleza jinsi sekta ya kilimo ilivyo mbaya.
Hili hapa ni andiko lake:
Kilimo. Maamuzi. Msalaba.
Kilimo – Sekta ambayo inaajiri watu wengi ( takribani 70% ya Watanzania ) na ambayo inasisimua sana uchumi sasa inachechemea.
Waziri wa Fedha ametuambia juzi kwamba, Kilimo kimeshuka kasi ya ukuaji wake kutoka 2.5% hadi 0.6% mwaka 2016. Hii ni kasi ndogo zaidi kupata kutokea ya ukuaji wa sekta ya kilimo tangu nchi yetu ipate uhuru.
Kilimo kinatakiwa kikue kwa kasi ya asilimia 6 – 8 kwa mwaka ili kuondoa umasikini kwa kasi. Hata hivyo kiwango cha juu zaidi kufikiwa ni 4.4% katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. Hii ndio sababu ukuaji wa uchumi Tanzania hauondoi umasikini kwani sekta zinazoendesha ukuaji huo sio sekta za wanyonge.
Kushuka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo ni kiashiria kikubwa sana cha 1) kuongezeka kwa umasikini, 2) kupanuka kwa wigo wa wenye nacho na wasio nacho na 3) kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Hivi Ndio viashiria vya MAENDELEO na sio idadi ya ndege ambazo nchi inamiliki.
Kilimo kinaathiri usalama wa chakula na kadiri bei za vyakula zikiyumba, masikini wa mijini (urban poor) hali yao huwa mbaya zaidi. Kukauka kwa ghala la chakula ni matokeo ya uendeshaji mbovu wa uchumi usiozingatia hali za wanyonge na kukumbatia maonyesho ya vitu.
Unaposema kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, nani anabeba msalaba Wa makosa ya kimaamuzi na kisera yaliyofanywa na serikali na kusababisha njaa nchini?
Bajeti ya pembejeo za kilimo imeshuka kutoka shilingi 78 bilioni mwaka 2015/16 mpaka shilingi 10 bilioni mwaka 2016/17. Pembejeo hazikufika kwa wakulima kwa Wakati na zilizofika zilikuwa ghali Sana. Wakulima wengi wanyonge hawakuweza kulima kwa mbolea na ilibidi kutumia mbegu ambazo hazina ubora. Huu msalaba wa maamuzi kuhusu pembejeo anaubeba Nani? Wananchi?
Zitto Kabwe