kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, baada ya hali yake ya afya kuzorota ghafla.
Hali hiyo imetokea siku moja baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Bagamoyo ambako yeye na wabunge wengine wa Chadema walikutana kwa siku tatu kwa ajili ya `semina elekezi.
Katika semina hiyo, Zitto alikuwa mmoja wa watoa mada na mwezeshaji katika `kuwafunda wabunge wengine wa chama hicho ambao pamoja na wale wa Viti Maalumu, jumla yao inakaribia 50.
Habari za uhakika kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa mwanasiasa huyo zilizopatikana jana, zilikuwa zikieleza kuwa, mwanasiasa huyo machachari alifikishwa katika hospitali hiyo jana majira ya saa 8 mchana.
Ingawa awali hakuweza kuzungumza kutokana na kuzungukwa na jopo la madaktari, baadaye ilifahamika kuwa alikuwa anaugua malaria kutokana na vipimo vyake kuonesha ana vijidudu viwili vya ugonjwa.
Lakini baadaye alipotembelewa tena katika chumba namba 357 alikokuwa amelazwa, Zitto hakuwa tayari kuzungumza lolote kuhusu afya yake zaidi ya kusema anachofahamu ni kwamba alikuwa amepumzishwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri akisubiri kuruhusiwa wakati wowote.
Baadhi ya rafiki zake wa karibu ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema Mbunge huyo aliugua ghafla jana na wanadhani hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na uchovu au mshtuko kutokana na taarifa zisizo rasmi zinazosikika mara kwa mara juu ya `mpasuko baina yake na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Hivi karibuni Zitto aliingia kwenye msukosuko wa kisiasa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya Bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akilihutubia kwa mara ya kwanza Bunge la 10 mjini Dodoma hivi karibuni.
Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alikaririwa hivi karibuni akisema kuwa hali ya kisiasa ndani ya Chadema ni shwari na hakuna mtafaruku utakaotokea kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Hadi tunakwenda mitamboni ilielezwa kuwa, afya yake ilikuwa inaendelea kuimarika.