Zitto alazwa Dar es Salaam

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, baada ya hali yake ya afya kuzorota ghafla.

Hali hiyo imetokea siku moja baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Bagamoyo ambako yeye na wabunge wengine wa Chadema walikutana kwa siku tatu kwa ajili ya `semina elekezi’.

Katika semina hiyo, Zitto alikuwa mmoja wa watoa mada na mwezeshaji katika `kuwafunda’ wabunge wengine wa chama hicho ambao pamoja na wale wa Viti Maalumu, jumla yao inakaribia 50.

Habari za uhakika kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa mwanasiasa huyo zilizopatikana jana, zilikuwa zikieleza kuwa, mwanasiasa huyo machachari alifikishwa katika hospitali hiyo jana majira ya saa 8 mchana.

Ingawa awali hakuweza kuzungumza kutokana na kuzungukwa na jopo la madaktari, baadaye ilifahamika kuwa alikuwa anaugua malaria kutokana na vipimo vyake kuonesha ana vijidudu viwili vya ugonjwa.

Lakini baadaye alipotembelewa tena katika chumba namba 357 alikokuwa amelazwa, Zitto hakuwa tayari kuzungumza lolote kuhusu afya yake zaidi ya kusema anachofahamu ni kwamba alikuwa amepumzishwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri akisubiri kuruhusiwa wakati wowote.

Baadhi ya rafiki zake wa karibu ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema Mbunge huyo aliugua ghafla jana na wanadhani hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na uchovu au mshtuko kutokana na taarifa zisizo rasmi zinazosikika mara kwa mara juu ya `mpasuko’ baina yake na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Hivi karibuni Zitto aliingia kwenye msukosuko wa kisiasa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya Bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akilihutubia kwa mara ya kwanza Bunge la 10 mjini Dodoma hivi karibuni.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alikaririwa hivi karibuni akisema kuwa hali ya kisiasa ndani ya Chadema ni shwari na hakuna mtafaruku utakaotokea kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Hadi tunakwenda mitamboni ilielezwa kuwa, afya yake ilikuwa inaendelea kuimarika.
 

Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,021
2,000
Tunamwombea kwa Mungu apone na akishapona aache unafiki ndani ya Chadema na aombe msamaha kwa watanzania wazalendo.Zitto Mganga njaa hivyo tuwe makini nae,asipo itisha mkutano na waandishi wa habari kuuomba msamaha umma wa wataka haki zito afukuzwe uanachama
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,610
2,000
Namtakia ahueni atoke mapema maradhi ni kitu cha kawaida kwa binadamu! People's Power:whoo:
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Bado hawajaanza wimbo kwamba akina Mbowe ndiyo sababu ya ugonjwa wake? Kwamba wamemtilia sumu ili afe kwa sababu alikataa kutoka nje ya Bunge?

Wimbo wa kipuuzi kama huo ulikuwapo kwa Chacha Wangwe!
 

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,221
1,225
Ndio tatizo letu watanzania kudharau kufanya check up za afya zetu mara kwa mara wengine hupuuzi sana kufanya check up za mara kwa mara jamani huwa inasaidia ukifanya check ya mwili wako,

Sasa bwana Zitto utakuta anamrundiko wa magonjwa tele mwilini mwake bila ya yeye kujua mpaka kagonjwa kamoja kaibuke ndio kanazua na mengine
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,071
2,000
KijaNA mdogo afya mgogoro au ndio presha ya kuwekwa kiti moto? ajiudzuru tuu arudi CCM.

Kuna wakati alishutumiwa kuwa alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mbunge mwenzie aliyekuwa mke wa mtu ambae ni marehemu sasa; isije ikawa ngoma ndio inaanza kulia halafu mkasingizia kuwa amelishwa sumu!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Kuna wakati alishutumiwa kuwa alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mbunge mwenzie aliyekuwa mke wa mtu ambae ni marehemu sasa; isije ikawa ngoma ndio inaanza kulia halafu mkasingizia kuwa amelishwa sumu!!

Umeniwahi mkuu. Nami nilikuwa na mawazo along those lines!!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Mtanzania wameandika eti kanyweshwa sumu bagamoyo,ni sumu gani hiyo?

Hilo gazeti la Rostam ndiyo lilikuwa kinara mwaka juzi katika kueneza eti Chacha Wangwe aliuawa na viongozi wa Chadema. Sitashangaa kjwa kuandika kitu kama hicho hivi sasa.

By the way si tulisikia kwamba gazeti hilo limeanza kujirekebisha na sasa linaandika habari za kuuzika -- imekuwaje tena? Kweli mtu mwongo haach asili!!!!
 

Cecy10

Member
Nov 2, 2010
7
0

Maradhi ni kawaida, kama malaria ni ugonjwa ambao unafahamika na kama ni mengine hayo ambayo wanasema mshutuko, mimi sioni kama hiyo ni mshutuko huo ni uzushi tu watu ili kutumiza malengo yao. Yeye kama ameambiwa kuna moja, mbili, tatu ajibu tu vizuri kama anaona kuna utata anaruhusiwa kumwaga manyanga na kwenda anakokuta siyo kuzusha maswali mengi yatakayokosa majibu.
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Mtu mwenyewe anaanzisha mjadala mkubwa halafu anashindwa kujibu na kufafanua, badala yake anakimbilia kuumwa! Unapoanzisha jambo uwe tayari kulitetea, au kusema 'sorry' siyo kukiweka chama katika mtihani mkubwa bila ya sababu yoyote ya maana. Chama ni kikubwa kuliko yeye, anapaswa kutambua.
 

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,275
1,195
RIP Chadema


Sarkofagus_Lux_Coffin.jpg
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,844
1,225
JEYKEYWAUKWELIJoin Date Fri Sep 2010 Posts 192 Thanks 8
Kibaraka wa ccm wala hatukushangai,na hilo jeneza la makamba na ccm yake!!!
 

matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,055
1,195
Maxelo naomba umnyamazishe kwanza Jeykeywaukweli anapolute sana. Mtu anaumwa halafu yeye analeta picha ya jeneza? ni utamaduni/uadui gani tulionao watanzania. Kilimasera Congrat kwa kuleta straight details
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,254
2,000
Kuna wakati alishutumiwa kuwa alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mbunge mwenzie aliyekuwa mke wa mtu ambae ni marehemu sasa; isije ikawa ngoma ndio inaanza kulia halafu mkasingizia kuwa amelishwa sumu!!

Iliwahi kujadiliwa HAPA na mjadala ukafungwa.

Ugua pole Mheshimiwa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom