Elections 2010 Zitto ajeruhiwa na Polisi, apelekwa Hospitali

HIMO ONE

Senior Member
Sep 6, 2010
128
7
Zito kabwe mbunge mteuliwa wa kigoma kaskazini alikuwa kigoma mjini kumtetea mgombea mwenzake wa chadema huko kigoma mjini ambapo jimbo hilo lina utata na kuna dalili kuwa ccm wanataka kuchakachua kura za chadema.kundi la polisi limewavamia na kumpiga zito na kumuumiza

source channel ten kama dkk 2 zilizopita wametangaza
 
Kuna mtu kawasifia polisi punde tu. Hawa ni vibaraka tu shwaini
 
Kwani police sio watz!!! wananishangaza sana!!! familia zao si ndio hizo zenye maisha duni!!! Si ndo hao wanakaa kwenye vijumba kama vijishimo????? Hivi hawajui wabunge makini kama Zitto ndo wa kuwatetea wapate maslahi ya kuwafaaaaaaa!!!!!!
 
police wamepewa 30,000/= km hongo nchi nzima sasa zinawachanganya.sijui hawana mama na dada zao huko bush wanaoteseka? ndiyo maana kigezo cha kujiunga na polisi ni kusoma na kuandika.
 
Kituo cha chanel ten kimeeleza kuwa mbunge wa kigoma kaskazini apigwa bomu napolisi,mitaa ya kigoma mjini baada ya kwenda kumpa back up mgombea wa kigoma mjini kupitia CHADEMA,kutokana na mgombea wa thithim(CCM) kutangazwa mshindi katika ushindi unaooneka kuwa kuna uwezakano wa maji kachanganywa na petrol (kuchakachuliwa). HAPA NILIPO NIME PANIC MAANA NAONA KUNA UWEZEKANO WA NEC KUWAAMBIA WAKURUGENZI WA UCHAGUZI KUWA WABUNGE WA UPINZANI WAMETOSHA.SO WANAFANYA KILA NJIA KUIBA HAKI.
 
UUMMMHHHHHHH, if that is true, then it is terribly awful!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Well, tatizo matokeo yakiisha kutangazwa hatua inayofuata ni mahakamani tu.....hakuna njia nyingine..........maandamano au vurugu hazitabadilisha matokeo hata kama kuna dhuluma kubwa imefanyika............
 
Nakushukuru mhe zitto kulia na wanaolia. Huo ndio uongozi imara utakaokuweka katika chati kwa muda mrefu. Uongozi ni kuwa karibu na watu wako. Utawashwa kwa muda lakini unatengenezewa heshima inayodumu. Kumbuka mandela. Heko
 
Ametaka mwenyewe yeye nani kama analeta vurugu polisi wanajua kazi yao.
namshauri asitetea mtu alie shindwa wa nini?
:hippie:
 
Back
Top Bottom