Zitto aitupia kombora CCM; ataka Mshahara wa Rais uwe wazi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
858
Points
0

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
858 0
Saturday, November 24, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), amekirushia kombora Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema hakina nguvu tena ya kuendelea kutawala. Kabwe alikwenda mbali zaidi na kusema ili Tanzania iwe salama, ni lazima CCM ishindwe katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.Zitto aliyasema hayo jana, katika mahojiano ya moja kwa moja baina yake na mtandao wa kijamii wa Jamii Forum (JF), ambapo alijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa.

Kauli ya Zitto, ilikuja baada ya mmoja wa wachangiaji kutaka kujua mtazamo wake kuhusu hali ya vyama vya upinzani nchini na hatima ya CCM kuelekea 2015.

Akijibu swali hilo, Zitto alisema chama chake kina nafasi kubwa ya kushika dola na kueleza kuwa jambo muhimu ni kwa chama hicho kinachokua kwa kasi kujipanga vizuri.

"Ili Tanzania iwe salama, ni lazima CCM ishindwe uchaguzi. CCM ikishinda tena mwaka 2015 itavunja sana moyo wa wananchi na wengine wanaweza kukata tamaa.

"Lakini pia CCM imechoka na haina nguvu za kutosha kukabiliana na changamoto za nchi hivi sasa. Njia pekee ya kuisaidia CCM iweze kujipanga upya ni yenyewe kuondoka madarakani.

"CHADEMA ina nafasi kubwa sana ya kushinda na kuongoza dola. Muhimu chama kijipange na kuonekana kama chama kilichotayari kushika dola. Tuyatende tunayoyasema na tujiimarishe zaidi.

Zitto aihofia CCM
"Unalizungumziaje suala la kuwa na utitiri wa vyama vingi vya siasa vinavyokula fedha za walipa kodi, halafu havina tija wala mchango wowote kijamii zaidi ya kutufilisi.

Je, kuna umuhimu wa kuifanyia sheria mabadiliko ili kuwe na limitation (ukomo) mfano, vyama vitatu tu?", aliuliza mmoja wa wachangiaji katika mtandao huo.

Akijibu swali hilo, Zitto alisema haoni sababu ya kuundwa kwa sheria inayoweka ukomo wa idadi ya vyama vya siasa na kueleza kuwa utitiri wa vyama vya siasa ndiyo afya ya demokrasia.

"Tusiminye kabisa watu kuwa huru kuanzisha vyama vya siasa. Baada ya muda ni vyama vyenye uwezo wa kukonga nyoyo za wananchi ndivyo vitabakia. Wala hatuna haja ya kuweka sheria," alisema.

Hata hivyo, Zitto alisema licha ya hivi sasa Tanzania kuwa na vyama vya siasa visivyopungua 20, lakini mbele ya safari haoni uhai wa vyama zaidi ya vinne.

Alivitaja vyama vikubwa vitakavyosalia kuwa ni CCM na CHADEMA, ingawa alionyesha hofu kuwapo na uwezekano wa kundi moja la CCM kujitenga na kuunda chama kingine chenye nguvu zaidi ya chama chake.

"Huko mbele ninaona Tanzania yenye vyama sio zaidi ya vinne. Vyama vikubwa viwili, CCM na CHADEMA. CUF watakuwa ‘balancing party' kama ilivyo LibDems UK au Greens na Liberals Ujerumani.

Zitto ang'aka kuhusishwa na CCM
Katika mahojiano hayo, Zitto alikanusha kuwa na uhusiano na CCM, na kusema kuwa hiyo ni propaganda inayofanywa na watu wachache wenye nia ovu dhidi yake.

"Ukitaka kummaliza mwanasiasa yeyote wa upinzani hapa Tanzania, mhusishe na ama usalama wa Taifa au CCM.

"Ndivyo ilivyokuwa kwa Mabere Marando miaka ya tisini. Marando ameishia kuweka sawa historia ingawa propaganda dhidi yake zilikuwa kali sana kiasi cha kuogopwa kweli kweli. Napita njia hiyo hiyo ya Marando na wanaonipaka matope haya wataona aibu sana ukweli utakapodhihiri.

"Siku za mwisho za uhai wake ndugu Chacha Wangwe naye aliambiwa ni CCM na kwa kweli alikufa akiwa na chuki sana kuhusu tuhuma hii.

"Faida kubwa niliyonayo mimi ni kwamba, mtaji wangu wa kisiasa ulikuwa ni mkubwa mno na ndiyo maana tuhuma hizi hazijaniathiri.

"Ninaamini tuhuma kama hizi zingekuwa kwa watu wengine, wangekuwa wameshafutika kwenye historia ya siasa.

"Sijawahi kuwa mwana CCM, familia yangu yote kabisa ni waanzilishi wa CHADEMA. Sina historia na CCM. Inawezekana wanaosema mimi ni CCM wengi wao wamewahi kuwa CCM, wana familia zao ndani ya CCM na wamewahi kula matunda ya CCM. Mimi sijawahi na wala sitawahi.

"Baadhi ya watu wanapandikiza chuki hizi kwa sababu zao wenyewe. Hawanisumbui maana najua ni kikundi kidogo cha watu wachache wenye malengo yao ovu. Wajue tu kwamba hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya maamuzi yao yasiyotokana na propaganda ila kutokana na matendo ya kila mmoja.

"Onyo: Watu hao hawawezi kummaliza Zitto kisiasa bila kuiathiri CHADEMA, maana the image of Zitto is so intimately intertwined with CHADEMA that you couldn't attack Zitto without jeopardizing the image of Chadema, and vice versa," alisema.

Alalamikia vyama kukosa itikadi
"Unalizungumziaje ombwe la itikadi miongoni mwa vyama vya siasa, ambapo tangia mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaingie nchini, ni vigumu kutofautisha itikadi za vyama vya siasa?" aliuliza mchangiaji.

"Hii ni changamoto kubwa sana kwa nchi yetu, itikadi za kisiasa husaidia kunyoosha sera za vyama. Hivi sasa chama chochote chaweza kuwa na sera yoyote ile kwa kuwa hakuna uti wa mgongo ambao ni itikadi.

"Lazima vyama vijipambanue kwa itikadi zao. Kwa kukosekana kwa itikadi zinazoeleweka vyama vimekuwa kama 'electoral machines' tu.

"Kukosekana kwa itikadi kunafanya vyama kudandia masuala. Mfano juzi hapa mmesikia Mkutano Mkuu wa CCM umeazimia elimu iwe bure. CHADEMA tulisema hivi mwaka 2010, CCM wakasema huo ni uwendawazimu, kwani haiwezekani.

Rais ajaye ni wa kizazi kipya
Zitto alirejea kauli yake kuutaka urais na kusema anaamini rais wa awamu ya tano atakuwa kijana.

"Mimi ninaamini kabisa kuwa rais ajaye wa Tanzania ni lazima atokane na kizazi cha baada ya uhuru. Nchi inahitaji a fresh start.

"Hebu tazama nchi hii, asilimia 70 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 29! Asilimia 65 ya wapiga kura wapo kati ya umri wa miaka 18 – 40. Hili ni Taifa la vijana.

"Nusu ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 17! Unaweza kusema hili ni Taifa la watoto. Hawa wazee wetu walipokuwa wanachukua nchi walikuwa vijana.

"Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 39, Mzee Rashid Kawawa alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 37. Waziri Mkuu wakati huo ndio alikuwa Mkuu wa Serikali, maana Mkuu wa nchi alikuwa Malkia wa Uingereza.

"Kuna watu lazima watafsiri chochote atakachosema Zitto. Hata hili ninaloandika hapa mtasikia, watasema tu. Kuna watu wanaumwa ugonjwa wa zittophobiasis ni lazima waseme.

Mshahara wa Rais uwe wazi
Baadhi ya wachangiaji walitaka kujua iwapo ipo haja ya kuendelea kufanya siri mishahara ya viongozi wa juu wa nchi, kama vile Rais wa Jamhuri, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais.

"Sijui mshahara wa Rais na naamini ni katika vitu ambavyo walipa kodi wanatakiwa kujua. Mshahara wa Rais hautakiwi kuwa siri kwa Mtanzania yeyote.

"Inapaswa kuwa wazi kabisa na kila raia ajue. TRA watakuwa wanajua kama sio tax exempt. Nadhani tukifuatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data."

Chanzo: Mtanzania
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
84,703
Points
2,000

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
84,703 2,000
Mshahara wa Rais uwe wazi
Baadhi ya wachangiaji walitaka kujua iwapo ipo haja ya kuendelea kufanya siri mishahara ya viongozi wa juu wa nchi, kama vile Rais wa Jamhuri, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais.

"Sijui mshahara wa Rais na naamini ni katika vitu ambavyo walipa kodi wanatakiwa kujua. Mshahara wa Rais hautakiwi kuwa siri kwa Mtanzania yeyote.

"Inapaswa kuwa wazi kabisa na kila raia ajue. TRA watakuwa wanajua kama sio tax exempt. Nadhani tukifuatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data."
Yesssssss!!!

This gives me a ray of hope that someday such information will be made public record.
 

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,295
Points
2,000

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,295 2,000
JF ime influence media zote leo, nikmaanisha magazeti yaliyosomwa ktk radio, mitandao, na TV.Hofu yangu inaweza leta shida sana kama watu wataamua fanya drama ktk JF , na kulipa waandishi wa magazeti ili ziandikwe na magazeti yote ili wapate Coverage na publicity ya kutosha.
 

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
4,535
Points
0

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
4,535 0
swala la mshahara wa rais kua wazi naungana nae kabisa hapo..kama tunajua obama au david cameroun au prime minister wa ujerumani mshahara wake kiasi gani kwanini tusijue mshahara wa rais wa tanzania? tujue pension yake na anakatwa kodi kiasi gani, akisafiri safari za ndani allowance kiasi gani akisafiri nje allowance kiasi gani...lazima tujue hivi vitu kama mtu hapendi mshahara wake ujulikane basi asigombee urais
 

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225
abdulahsaf Acheni Wajameni... PESA zinaishia SAFARINI Mshahara wa RAIS hapati chochote ila Marupurup; Hauoni yeye ni MIKOPO TUUUU Hadi Mwanae CHUO KIKUU hajalipa MKOPO wake hadi SASA... labda wameambatanisha na MIKOPO ya KICHINA
 
Last edited by a moderator:

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,649
Points
1,225

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,649 1,225


Acheni Wajameni... PESA zinaishia SAFARINI Mshahara wa RAIS hapati chochote ila Marupurup; Hauoni yeye ni MIKOPO TUUUU Hadi Mwanae CHUO KIKUU hajalipa MKOPO wake hadi SASA... labda wameambatanisha na MIKOPO ya KICHINA
Wewe ndiye msemaje wa familia yake???!!
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,135
Points
1,250

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,135 1,250
Ama kwa hakika huyu kijana(ZITTO KABWE)anafaa kuwa mgombea urais na rais kabisa,anavyo vigezo,nitampa kura yangu,anafanana na obama kwa mambo mengi sana
 

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,014
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,014 2,000
Nchi nyingine waandishi wa habari wangemshupalia DHAIFU kwa swali hili, "Wananchi ambao ndio wanaokulipa mshahara hawajui unapata mshahara kiasi gani kwa mwezi. Je, kwanini mshahara wako unafanywa siri kubwa? Je ni kiasi gani unapata kama mshahara na marupurupu mengine kila mwezi." lakini nchini mwetu mwandishi kama huyo anaweza kuwekewa mizengwe ya hali ya juu hata akapoteza kazi kisa kumuuliza DHAIFU swali nyeti.
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,135
Points
1,250

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,135 1,250
Nchi nyingine waandishi wa habari wangemshupalia DHAIFU kwa swali hili, "Wananchi ambao ndio wanaokulipa mshahara hawajui unapata mshahara kiasi gani kwa mwezi. Je, kwanini mshahara wako unafanywa siri kubwa? Je ni kiasi gani unapata kama mshahara na marupurupu mengine kila mwezi." lakini nchini mwetu mwandishi kama huyo anaweza kuwekewa mizengwe ya hali ya juu hata akapoteza kazi kisa kumuuliza DHAIFU swali nyeti.
"Nadhani tukifuatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data."- ZITTO KABWE
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,135
Points
1,250

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,135 1,250


"Mimi ninaamini kabisa kuwa rais ajaye wa Tanzania ni lazima atokane na kizazi cha baada ya uhuru. Nchi inahitaji a fresh start.

"Hebu tazama nchi hii, asilimia 70 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 29! Asilimia 65 ya wapiga kura wapo kati ya umri wa miaka 18 – 40. Hili ni Taifa la vijana.

"Nusu ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 17! Unaweza kusema hili ni Taifa la watoto. Hawa wazee wetu walipokuwa wanachukua nchi walikuwa vijana.

"Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 39, Mzee Rashid Kawawa alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 37. Waziri Mkuu wakati huo ndio alikuwa Mkuu wa Serikali, maana Mkuu wa nchi alikuwa Malkia wa Uingereza.

"Kuna watu lazima watafsiri chochote atakachosema Zitto. Hata hili ninaloandika hapa mtasikia, watasema tu. Kuna watu wanaumwa ugonjwa wa zittophobiasis ni lazima waseme.
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,135
Points
1,250

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,135 1,250
Hao utumishi wazianike hadharani basi ili Watanzania tufahamu DHAIFU analipwa mshahara na marupurupu yake yote kiasi gani.
Ni vema tusiende personal bali tuutazame urais kama taasisi nadhani ndio maudhui ya ZK,Tukienda personal kwa sababu tu aliyekalia kiti sasa sio maarufu sana kwetu tutaondoa maana yote ya alichotaka kukiwasilisha ZK
 

jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
21,422
Points
2,000

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
21,422 2,000
Tanzania tuna tatizo kubwa inapokuja kwenye access to government information,hilo ni tatizo kubwa sana na ndiyo msingi wa kuwa na serikali yenye rushwa...Mfano hapo chini ni utafiti uliofanywa na global intergrity.Inaonyesha kuwa Tanzania bado tuko nyuma sana kwenye access to information.Yani kwetu ni zero ikija kwenye kupata taarifa kutoka serikalini.Tuko kwenye bottom performers,tume score 6 out of 100!Hii ina maana serikali yetu ina dalili zote za udikteta.

Public access to government information remains a key ingredient of an effective anti-corruption framework in any country, regardless of income level. In Global Integrity's 2010 sample, Peru topped the list on our access to information indicators, with the principle of freedom of information now enshrined in its national constitution. On the other end of the spectrum stand most of the African nations covered in Global Integrity's 2010 sample; mechanisms for requesting government information are virtually non-existent in Egypt, Tanzania, Somalia, Cameroon, and Nigeria.

Access to Government Information Countries Score
TOP PERFORMERS (out of 100)
Peru 93
Bulgaria 90
Argentina, Czech Republic, Poland, Russian
Federation
85
Italy 83

BOTTOM PERFORMERS (out of 100)
Somalia 17
Cameroon 8
Tanzania 6
Nigeria, West Bank 2
Egypt, Malaysia 0
http://www.globalintegrity.org/documents/GIR2010-Key-Findings.pdf
 

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,023
Points
1,225

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,023 1,225
Zitto wanakupa sifa usizostahili hasa vyombo vya habari siku watakapo kuacha njiani utayeyuka kama mshumaa jiangalie sana
 

makundi4619

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2012
Messages
486
Points
0

makundi4619

JF-Expert Member
Joined Jul 12, 2012
486 0
Serikali yoyote ile yenye matatizo ya kifisadi na rushwa kamwe haiwezi kuwa transparent as access to government information is highly correlated to the level of transparency. Just imagine miaka yote ya kutawala watu wenye kupenda amani kama watanzania bado serikali ya CCM ni miongoni mwa serikali zinazoongoza kwa hisia ya kuwa dikteta duniani!!! Hii nia aibu kubwa sana we need real change to get out of this mess! Tanzanians as a people deserve a better reflection of the people we are at global level by getting rid of the politicians who deprive us of the respect we deserve and command!!!!!
 

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,014
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,014 2,000
Hata Somalia wako juu yetu!!! Duh! Nchi ambazo tuko juu yao ni Misri, Nigeria, Malaysia na West Bank!!!
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined
Feb 25, 2006
Messages
3,348
Points
1,250

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined Feb 25, 2006
3,348 1,250
JF ime influence media zote leo, nikmaanisha magazeti yaliyosomwa ktk radio, mitandao, na TV.Hofu yangu inaweza leta shida sana kama watu wataamua fanya drama ktk JF , na kulipa waandishi wa magazeti ili ziandikwe na magazeti yote ili wapate Coverage na publicity ya kutosha.
Usiwe na shaka; inategemea nani amehojiwa na ameongea nini. This was one of the most powerful interviews a politician has ever made in TZ. Nawapongeza JF kwa kuandaa hii kitu. Tunahitaji kuwajua viongozi wetu vizuri, na namna pekee ni kuwapa fursa wazungumze.
 

Forum statistics

Threads 1,392,768
Members 528,684
Posts 34,117,507
Top