Zitto aitibua CHADEMA

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.
 
hafai .... msimamo ni ule ule .... aondoke kwa manufaa ya chama .... hawataweza kuwa na mtu anayejiona mkubwa kuliko chama!
 
Nakunali kuwa kama kweli Zitto alitoa masharti hayo alikosea. Siku zote ukitaka muafaka wa kweli ni muhimu sana kusamehe au kufuta makosa yote ya nyuma. Hata hivyo nisingedhani pia suala la Zitto kutoa kauli hiyo (kama ni kweli alitoa) iwe issue ya kuchukua muda ndani ya chama, i dont see if its an issue which requires that much of the attention. Kama alivyoshiriki vikao juzi bila masharti iwe hivyo hivyo. Nasisi pia tuache kuchonganisha huo kwa kuongeza chumvi nyingi.
 
Zitto alikuwa na wajibu wa kuhakiki kama member na mwenyekiti...lakini hekima na busara zitumike kwake juu ya swala hilo CHADEMA.
 
Mwenyekiti nae anataka kutuaminisha hiki chama ni chake sasa, kwani kuna shida gani wakasameheana kujenga upinzani wenye nguvu, najua Zitto amejutia usaliti wake na sidhani kama atarudia tena, asamehewe tu.

Kuna msamaha wenye masharti?
 
Viongozi wangu Mbowe na Dr Slaa, tunawapenda sana pia tunawaamini, hebu msameheni Zitto, tunataka tuone ile triple army kama ya zamani, msameheni bila masharti.

Zitto na wewe hebu tunaomba utulie kamanda, epukana na kauli tata tujenge chama.
 
Last edited by a moderator:
Nakunali kuwa kama kweli Zitto alitoa masharti hayo alikosea. Siku zote ukitaka muafaka wa kweli ni muhimu sana kusamehe au kufuta makosa yote ya nyuma. Hata hivyo nisingedhani pia suala la Zitto kutoa kauli hiyo (kama ni kweli alitoa) iwe issue ya kuchukua muda ndani ya chama, i dont see if its an issue which requires that much of the attention. Kama alivyoshiriki vikao juzi bila masharti iwe hivyo hivyo. Nasisi pia tuache kuchonganisha huo kwa kuongeza chumvi nyingi.

Majina mliomuita ndio yanampa changamoto yaani we uitwe msaliti mroho wa madaraka, mla rushwa halafu wakwambie umesamehewa we uchekelee tu! Na kweli watamuomba radhi.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.

Habari kama hizi za kishabiki mandazi ndiyo zinazoendeleza migogoro isiyo nabtija kwenye vya vya siasa nchini, hapa hii habari haijengi chama bali inabomoa, unataka kutuaminisha malumbano yasiyo na tija yamefufuka upya alafu kibaya zaidi habari yako haina citation.

Childish post.
 
Mimi nilishituka kuona gazeti la Tanzania daima limefanya mahojiano maalumu na ZZK Hii ni dalili tosha ya kuelekea Muafaka
 
Zittoo,huyu kijana ni mshenzi sana alitufanyia kiburi yeye na Mch.msigwa pale bunge dogo dar wakati tunafatilia suala kukosa mkopo wa chuo, nikiwa na wanaharakati wangu,namshukuru mungu kwa msahada wa mama Magret 6,vijana walifanikiwa na wako vyuoni sasa.ZZk bureee kabisaaa!!!ndo anayaleta kwenye chama chetu
 
Akafie mbali kudadadadadek! One a traitor, always a traitor! Zitto haaminiki kwenye chama na uongozi utafanya kosa sana kumsamehe bila kukiomba radhi chama kwa kuuza majimbo wakati wa uchaguzi!
 
Back
Top Bottom