Zitto aitesa CHADEMA, Tamko la mkoa wa Kigome hii leo hili hapa. Usalama wa Slaa wajadiliwa

Status
Not open for further replies.

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO


TAMKO LA KIKAO CHA MKOA – CHADEMA
PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
- Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama. - Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa - Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
- Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao. - Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
i. Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
ii. Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.

iii. Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.

iv. Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.

LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA


Asanteni




ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA

M/KITI MKOA 01/DEC.2013 KATIBU MKOA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442




CHADEMA MKOA KIGOMA
 
hiyo ziara ina maana gan? Kataeni wanakigoma mpaka haya maamuzi ya kijuha waliyofikia akina chadema family yarekebishwe
 
Sasa hapo Zitto kaitesa vipi Hiyo Chadema? Tatizo mpango wa Shinyanga umebumbuluka sasa mna tafuta front page za kesho , Mwigulu alipanga Kumuua Kigaila Leo kumbe hajui kuwa hayupo Kigoma ndio maana alikuwa na breaking news hapa eti Kigaila amenusurika kifo leo Kigoma ......ndio yalikuwa maandalizi ya hali ya hatari hayo........
 
Kwanini taarifa hii itolewe kwenye press kama kweli ilikuwa na nia njema? Kwanini mawasiliano yasingefanyika baina ya uongozi wa mkoa na makao makuu? nina shaka na ID ya mleta news.
 
Mh! Hali tete Nilishashauri muungwana akivukwa na nguo huchutama! Ila kama huoni soni basi tembeza kengele zako mbele za watoto.
 
  • Thanks
Reactions: FKM
kweli mbowe na slaa tamaa ztawaua! Wameg'ang'ania had chama kimefia mikonon mwao. Shame on them. Hawa ni zero brain kwel
 
Tamko la Mwenyekiti wa Matawi ya Mkoa wa Shinyanga liko wapi? Mbona halijatoka mpaka muda huu? Si unalo hapo? Tuweke nalo hapa tulijadili.....
 
Khaa!! Kichekesho sana hasa pale unaposhtakiwa kwa makosa 11 ya "SIRI". Ona sasa chama kinakufa halafu maccm si ndiyo yatakomba kila kitu kwa sababu hakuna wa kuwapigia kelele. Yote kwa sababu ya ulevi tu na tamaa ya madaraka. Shame on you CDM - CC :frusty:
 
Kigoma demokraisa imelala MBUNGE wa kwanza kutoka CDM dr aman warid Kabour alitoka Kigoma. DCM walimfukuza kafulila kisa kupingana nao eti alikuwa ana muunga mkono zito.
Km si NCCR Mageuzi kutumiwa na CCM hasa james Mbatia, tungehamia NCCR sasa tufanyeje? CCM tulishavunja ndoa tangu miaka ya 95, sasa kurudi hatuwezi. Tunaombeni zito na wapenda maendeleo watuletee chama kingine.
 
Too LOW.
Tafuteni Story nyingine ya kuweka Front page.
Hii haina mashiko.
 
kigoma demokraisa imelala mbunge wa kwanza kutoka cdm dr aman warid kabour alitoka kigoma. Dcm walimfukuza kafulila kisa kupingana nao eti alikuwa ana muunga mkono zito.
Km si nccr mageuzi kutumiwa na ccm hasa james mbatia, tungehamia nccr sasa tufanyeje? Ccm tulishavunja ndoa tangu miaka ya 95, sasa kurudi hatuwezi. Tunaombeni zito na wapenda maendeleo watuletee chama kingine.


hiki tupa kule
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom