Zitto aitesa CHADEMA, Tamko la mkoa wa Kigome hii leo hili hapa. Usalama wa Slaa wajadiliwa

Status
Not open for further replies.
ukweli anajitesa mwenyewe ameenda kwenye redio 20 kujitetea na kulia lia TV 12 ,magazeti kwa wiki mbili yameeandika habari zake katengeneza mchoro wa matamko kwa msaada wa MACCM, nadhani mwenyekiti wa CCM naye anatoa dozi ndogo ndogo kumpepea mjamaa ili akiingia CC ape ujmbe wa CC kama aliyowaweka familia yake akina Salma
 
utaratibu wa tarifa kama hizo zinatumwa makao makuu kwanin ziwekwe humu kinyume cha utalatibu?
 
oh atazomewa! mbona JK,Mkamba na Mh.Ndovu walizoewa kigoma? kuna hofu gani dr akizowa? acheni wonga wa mabadiliko...
 
Hicho ni chama cha wachaga mdhamini Mtei Mkiti mkwewe mwekahazina mkwewe Mbowe ambaye ni mwanae Mtei chama au kampuni
 
Ni mpuuzi tu kama Lema ndo anaweza kufikiria ziara ya Kigoma kwa hali ilivyo sasa

Sijui nani ni mshauri wa Dr Slaa siku hizi au ndo anaongozwa na chuki zidi ya Mh Zitto?

Hili mshalikoroga!

Sent from BlackBerry 9520
 
Mawazo ya msukumo wa BANGI!
 
Hicho ni chama cha wachaga mdhamini Mtei Mkiti mkwewe mwekahazina mkwewe Mbowe ambaye ni mwanae Mtei chama au kampuni
Jiungeni na CHAMA CHA KIGOMA CHAUMMA mnalia lia nini? ZITTO na Kafulila walishaanzisha CHAMA na kumpa Mkigoma Mwenzao si mjiunge?!! Ili muone kuwa kwa unafiki wenu kinaishia KIGOMA?
 
Mnaanzisha cha nini? CHAUMMA haiwatoshi? Zitto na Kafulila Wameanzisha Chaumma na kumpa uenyekiti mzee Hashim Rungwe.

Haya tumekuelewa unashinda humu uingize siku haya kachukue chako kwa padri
 
CCM inapokuwa na jukumu la kuratibu matamko ya CHADEMA kwenye vyombo vya habari ......

CCM haikuhusika na ugomvi wenu - hayo ni makambi yenu wenyewe tu huko, na sisi huku tunayo ya kwetu, yanatutosha! Nyie shughulikeni na makambi yenu na mikakati yenu ya kufukuzana ama kung'oana vyeo, sisi tuacheni na ya kwetu! Hayo maugomvi ya kwenye chama chenu ni ya kwenu, mmeyakoroga wenyewe, yanyweni sasa! Msitafute mchawi katika CCM. CCM ihangaike na nyie kwa sababu gani jamani? Chama chenu ni kitoto sana ukilinganisha na CCM lakini kimejaa 'uhafidhina' mkali kuliko baba ambaye amejaa uvumilivu na udemokrasia...

Ushauri wa bure: jifunzeni kuvumilia 'opposition', ndiyo afya ya taasisi. Tena kwa watu wenye hekima nyingi sana, wao wangependa zaidi kupingwa ili wajifunze mbinu mpya za kuhudumia umma na siyo kuwachukia wanaowapinga. Watu wenye hekima nyingi sana watasikia kwa umakini zaidi sauti za wachache wenye kushambuliwa kuliko za wengi waliokubaliana kuwasulubu wanyonge wachache...Msipoufanyia kazi ushauri huu, msishangae kukiua chama chenu kabla hata hakijakomaa.

Regards,
HK.
 
Mbunge Mansoor wa Kiembe samaki alifukuzwa eti kaijadili rasimu ya katiba kwa uwazi.......nawe huna hoja, umeshindwa kumng'oa Spika mpaka leo , unafiki tu umekujaaa.....eti Mtwara apelekwe RC Muislamu.....Shame........
 
Hali ni Mbaya Kigoma: Viongozi wa CHADEMA mkoani humo wazuia ziara ya Dr. Slaa wakihofiwa usalama wake

1.png

TAMKO LA KIKAO CHA MKOA – CHADEMA, PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013

- Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo.

Lengo likiwa ni kuangalia uhai wa chama.- Mambo makuu na muhimu yaliyozingatiwa:

- Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe. Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.

- Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo:-

i. Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uweze kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.

ii. Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kuwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.

iii. Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.

iv. Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.

v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.

Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu.

Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.

LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA

Asanteni
ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA 01/DEC.2013 KATIBU MKOA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442

CHADEMA MKOA KIGOMA

Chanzo.
http://www.unapitwa.com/moto/fpy8g
 
Babu slaa kwisha habari yako.....hupendwi tena kama 2010...eeh Mungu umetuepusha na mengi,kwa kuwajaza uelewa wa tz na kumkataa babu slaa 2010,japo kua ufisadi na umasikini vilikua vimeshamiri,lkn wewe Mungu ukasema HAPANA kwa kibabu hiki,ni heri umasikin na ufisadi kuliko @dr.slaa cc Ben Ritz
 
Last edited by a moderator:
Sisi wana CCM,kuwananga CDM haitatusaidia,Zito Ni mtaji mzuri kwetu atakuwa msaada mzuri2015,ikiwezekana awe mgombea wetu WA urais 2015...
 
Sultani Mbowe hana amani hata ofisini kwake
 
Attachments

  • 1386023279972.jpg
    1386023279972.jpg
    9.3 KB · Views: 87
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom