Zitto aitaka Serikali ya Mama Samia kuhakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, yuko tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, endapo serikali yake itahakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari, vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake.

Mwanasiasa huyo ametoa sharti hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumanne tarehe 23 Machi 2021, wakati anazungumzia picha rasmi ya Rais Samia, iliyotolewa na Serikali.

Rais Samia amechukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzia utawala wa Rais Samia, Zitto amesema yuko tayari kumpa ushirikiano wake, endapo masharti yake hayo yatafanyiwa kazi.

Pia, amesema kiu yake katika serikali hiyo, ni kuona demokrasia inatamalaki kwa kuwa ndiyo suluhisho la changamoto za Tanzania.

“Ninachohitaji katika nchi yetu pendwa ni demokrasia, demokrasia ni suluhisho la changamoto zetu.”

“Nitatoa msaada wangu kwa Rais endapo vyama vya siasa vitakuwa huru pamoja na kuhakikishiwa uhuru wa vyombo vya habari,” ameandika Zitto

Wito huo wa Zitto umetolewa siku kadhaa tangu Katibu Mkuu wa chama chake, Ado Shaibu kusema kwamba ACT-Wazalendo kiko tayari kushirikiana na Rais Samia.

Akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, tarehe 20 Machi 2021, Ado alisema kauli iliyotolewa na Rais Samia juu ya Watanzania kuzika tofauti zao na kusonga mbele, inaleta matumaini.

Na kwamba, anaamini mchango wa vyama vya siasa vya upinzani katika ujenzi wa nchi, utaheshimiwa kama ilivyokuwa zamani.

Rais Samia alitoa wito kwa Watanzania kushikamana na kuzika tofauti zao, tarehe 19 Machi 2021, wakati anahutubia taifa baada ya kuapishwa kushika mikoba ya Hayati Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, baada ya kupata matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita, Ijumaa tarehe 26 Machi 2021.

Mwanasiasa huyo aliiongoza Tanzania katika kipindi cha miaka mitano na miezi mitano 5 Novemba 20215 hadi 17 Machi 2021.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Kwani aliombwa kumuunga Mkono?
Ana Nini chaku Muunga Mkono nacho?
Kule zanzibar Je Ata jiondowa?
Kwani Kuna Ukoloni hapa Nchini?
ivi Hizi Siasa Zina Tujengea Nini hapa Nchini?
Mna shindwa Kujenga Office zenu Je?
Kuna faida gani yaku Endelea na Siasa na Nchi haijengwi.

Leteni Hoja za Maendeleo sio Siasa tu
Tuna Taka Tuone Maendeleo kuanza Ndani ya Chama husika.
Maendeleo ndio Habari ya mjini sio puhuzi kila wakati.
 
Hata ww unaweza kunifunza mkuu. Demokrasia inazuia vipi maendeleo bosi?
Ni wazi tu kwamba Mipango na Manunuzi ya Kitu kama ndege lazima kipitishwe na Bunge ndio Democrat way yaku jenga au kununuwa Assets za Serekali

Na ili Bunge lipitishe lazima Serekali ije na Ombi linalo Beba Maelezo yaku tosha kuhusiana na Hilo jambo inayo Taka Bunge likubali
Pia lazima benge lipewe Muda waku jirishisha na Maelezo.
Pia Gharama zote lazima zi izinishwe na Bunge pia ilo Nalo Lina Omba Muda.

Pia Kuna Michakato mingi ambayo lazima ipite kwa kitengo Husika ili jambo Lifanyike pia lazima Lipewe Muda.

Hiyo ndio Serekali ya Democrat

Sasa Serekali ya dictator ni ili
Ya Maamuzi ya Mtu mmoja au cabinet inayo Ongozwa na Dhamira za Mtu mmoja

Kiongozi Anapo amuwa Jambo fulani Lifanyike hakunaga kufuata Misingi ya Democratic way

Ni Kiongozi kusema na Cabinet Ina Tekeleza hapo hapo na Mipango Ina anzishwa
Kwaiyo utakuta jambo laku fanya kwa Miezi 3 Hadi 6 au Mwaka in Democratic way Lita Fanywa naku Anza kutekelezwa Ndani ya Mwezi mmoja ay week kadhaa in dictatorship way.

Kwaiyo kiufupi Dictator aki amuwa kuijenga Nchi ni Rais sana Kuliko Njia ya Democrats.

Sababu Kuna Wakati njii Hii ya Democrats Inaweza Kuchelewesha au ku simamisha kabisa Ujengaji au mradi wowote Iwapo Serekali itakosa Maelezo yaku tosha kuhusiana na Mradi Husika.

Pia Uongozi wa Democratic way una Mapana zaidi Hadi katika Usiano wa Kimataifa.

Kwa Mfano Mradi wa Kujenga Nyerere Hydropower station kule Rufiji Uli ingia mgogoro na Shirika la Kulinda Mazingira Duniani.
Wao Wali pendekeza naku Sema huo mradi husitishwe Mara moja sababu Eneo lile nila Hifadhi ya Wanyama na Mengine Mengi.
Lakini sababu Uongozi hauku zingatia Democracy Serekali ili Endelea na Ujenzi waki Sema kuwa ni Nchi huru na haitaki kuingiliwa.

So ni Namna Gani utaona kwamba Democracy huChelewesha Maendeleo kwa njia moja au nyingine.
Pia Utaona kuwa Dictatorship huweza kuweka speed kwenye Swala la Ujenzi wa Taifa linalo Taka Kuji kwamuwa kiuchumi.
 
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, yuko tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, endapo serikali yake itahakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari, vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake.

Mwanasiasa huyo ametoa sharti hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumanne tarehe 23 Machi 2021, wakati anazungumzia picha rasmi ya Rais Samia, iliyotolewa na Serikali.

Rais Samia amechukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzia utawala wa Rais Samia, Zitto amesema yuko tayari kumpa ushirikiano wake, endapo masharti yake hayo yatafanyiwa kazi.

Pia, amesema kiu yake katika serikali hiyo, ni kuona demokrasia inatamalaki kwa kuwa ndiyo suluhisho la changamoto za Tanzania.

“Ninachohitaji katika nchi yetu pendwa ni demokrasia, demokrasia ni suluhisho la changamoto zetu.”

“Nitatoa msaada wangu kwa Rais endapo vyama vya siasa vitakuwa huru pamoja na kuhakikishiwa uhuru wa vyombo vya habari,” ameandika Zitto

Wito huo wa Zitto umetolewa siku kadhaa tangu Katibu Mkuu wa chama chake, Ado Shaibu kusema kwamba ACT-Wazalendo kiko tayari kushirikiana na Rais Samia.

Akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, tarehe 20 Machi 2021, Ado alisema kauli iliyotolewa na Rais Samia juu ya Watanzania kuzika tofauti zao na kusonga mbele, inaleta matumaini.

Na kwamba, anaamini mchango wa vyama vya siasa vya upinzani katika ujenzi wa nchi, utaheshimiwa kama ilivyokuwa zamani.

Rais Samia alitoa wito kwa Watanzania kushikamana na kuzika tofauti zao, tarehe 19 Machi 2021, wakati anahutubia taifa baada ya kuapishwa kushika mikoba ya Hayati Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, baada ya kupata matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita, Ijumaa tarehe 26 Machi 2021.

Mwanasiasa huyo aliiongoza Tanzania katika kipindi cha miaka mitano na miezi mitano 5 Novemba 20215 hadi 17 Machi 2021.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Hatuhitaji utungaji mkono wa Zito! Asipounga mkono hakuna kitakachopungua. Akiunga mkono hakuna kitakachoongezeka!! Ajiulize je kutokumuunga mkono JPM je kitu gani kilipungua? Tatizo Zito anadhani ana umuhimu mkubwa katika Siasa za Tanzania wakati siyo!
 
Acha upotoshaji. Udikiteta ni mbaya.

Hizo United Arab Emirates unazozisema ni falme. Wafalme wa Dubai,Oman na hata Saudia siyo madikteta.
Unawafaham Saud Arabia kweli au unawachezea? Siasa kule hakuna. Ni full usultani. Ukisumbua unaweza hata katwa kichwa kwa upanga. Mimi naunga uhuru wa watu na vyombo vya habari. Huo uhuru chini ya JPM ulikuwepo, wachache waliovunja sheria waliadhibiwa halafu watu wanasema hakuna uhuru.

Nakumbuka enzi za JK Mwanahalisi lilifungiwa mazima kwasababu ya kukiuka Sheria. Vyama vya siasa vijikite katika hoja na kuja na sera mbadala na si matusi. Natamani tuwe na ushindaji wa kweli wa kisiasa za hoja na si matusi. Natamani tuwe na midahalo pia ya wagombea Urais hata wawili au watatu ambao wanaonekana wana Mvuto kisiasa. Lengo wananchi wachague mtu kwa hoja zake.
 
Nimekaa nikafikiria jambo hili sana. Ni aibu kwa nchi kuwa na chombo cha uhakika kimoja tu ambacho ni Kigogo, wengine wote kuandika ni mpaka msemaji wa Serikali ajitokeze kwanza ndio wanukuu maneno yake. Ni aibu.
 
Back
Top Bottom