nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Israel Mgussi,Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, amekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapatia vijana nafasi katika uongozi wa sektretarieti na kamati kuu ya CCM.
Akichangia hoja ya muswada wa marekebisho ya sheria ya mauzo ya nje (EPZs) na maeneo maalumu kiuchumi (SEZs) bungeni jana, Zitto alisema vijana ndio mhimili wa maendeleo ya kwa nyanja zote kwa taifa lolote duniani.
Nianze kwa kusema,nimefurahishwa na mabadiliko katika Chama Cha Mapinduzi,nimefurahi vijana kupewa fursa ya kushika nyadhifa hizo kubwa katika chama," alisema Zitto na kuongeza,
....Sisi Chadema tulishaanza hilo muda mrefu, vijana ndio wanapewa nafasi kubwa ya uongozi katika Chama maana ndio mhimili wa maendeleo, nampongeza Januari Makamba, Nape Nnauye kwa nafasi walizochaguliwa, naahidi sisi Chadema tutashirikiana nao katika kuhakikisha tunaliletea taifa hili maendeleo.
Katika mchango wake wa muswada wa marekebisho ya sheria ya SEZs na EPZs, Zitto alisema ni vizuri kwa sheria hiyo kuwaangalia watu wanaozalisha bidhaa maalumu kama saruji kwa kuwaondolea kodi ya kusafirisha bidhaa hizo hadi kwa mlaji.
Mbali na hilo alisema suala la vivutio kwa wawekezaji ni muhimu, lakini akapinga kitendo cha mwekezaji kupewa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 akisema hiyo haina tija kwa faida, maana wawekezaji hao huzalisha ajira ndogo kwa wazawa na kwamba taifa hupoteza mapato bure.
Vivutio wanavyopewa wawekezaji viangaliwe kama vina faida, mwekezaji anaposamehewa kodi ya mapato kwa miaka 10,msamaha wa kodi ya mapato kwenye gawio, riba na pango kwa miaka 10, misamaha wa ushuru wa forodha, VAT na kodi nyingine kwenye malighafi na mitambo ya uzalishaji haina faida kwa nchi, maana mwekezaji anaweza kuondoka mara tu miaka 10 inapoisha," alisema Zitto.
Kauli ya Zitto iliungwa mkono na mbunge wa Jimbo Sorwa(CCM), Ahamed Salum ambaye pamoja na mambo mengine yeye alitaka serikali iviwezeshe viwanda vidogo vidogo vya ndani kupitia SIDO.
Mbuge huyo wa Sorwa alisema endapo viwanda vya ndani vitapewa fursa na misamaha hiyo ya kodi wanaopatiwa wawekezaji wakubwa iwe pia kwa wawekezaji wadogo, wazalishaji wa ndani wanaweza kutoa tija kubwa kwa taifa.
Salum alisema hata nchi ya China ambayo kwa sasa inaonekana uchumi wake kukua kwa kasi, asilimia 70 ya wazalishani ni kutoka viwanda vidogo vidogo na wawekezaji wakubwa ni asilimia 30 tu.Alisema ni vema kama Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuviwezesha viwanda vya ndani na kwamba kauli ya kilimo kwanza iendani na uwekezaji wa ndani katika viwanda vidogo vidogo..